Wednesday, September 14, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA BAMIA NA MCHUZI MZITO WA MTINDI

KAA TAYARI KWA KUJIFUNZA KUTENGENEZA MCHUZI HUU MZITO WA BAMIA NA MTINDI KWA NJIA RAHISI NA NYEPESI FAMILIA WAFURAHIE

MAHITAJI


480 gram mtindi halisi (plain Yogurt)
2 kijiko kikubwa cha chakula Channa flour (unga wa dengu)
10 bamia kubwa (Ladies finger)
1/4 kijiko kidogo cha chai ungwa wa Turmeric
1/2 kijiko kidogo cha chai sukari
5 gam chumvi
1 kipande cha mdalasini (Cinnamon Stick)
3 mbegu za karafuu (Cloves)
1 kijiko kidogo cha chai mbegu za binzali nyembaba (Cumin Seeds)
1 pili pili nyekundu ya kukauka (Dried Red Chillies)
5 gram pili pili manga
1 kjiko kidogo cha chai samli
Majani ya giligilani kwa kupambia
 

MUDA WA MAANDALIZI

Muda wa kuandaa : Dakika 15

Muda wa kupika : dakika 30
Idadi ya walaji  : Watu 2

JINSI YA KUANDAA FATILIA MAELEZO NA PICHA HAPO CHINI


Chukua mtindi kisha uchanganye na maji 480 gram piga mpaka ichanganyike vizuri.


Katika bakuli nyingine ndogo changanya unga wa dengu na mtindi kidogo hakikisha hauweki mabonge bonge.


Chukua mchanganyiko wa unga wa dengu kisha changanya katika mchanganyiko wa mtindi pamoja na pili pili manga na unga wa tumeric ichanganyike vizuri.



Kisha chukau mchanganyiko huo wa mtindi na weka katika kikaango hakikisha moto ni mdogo sana na endelea kukoroga lasiivyo mtindi utaunguklia kwa chini.



Kisha chukua kikaango kingine na weka kijiko kimoja cha mafuta na ukaange bamia pamoja na chumvi.



Chukua kifuniko na funika bamia ili ziive haraka lakini hutakiwi kufunika zaidi ya dakika 2 lasiivyo zitaiva sana na kupondeka kama hujiamini katika kukadiria muda basi acha wazi usifunike kikaango pika wazi.



Mpaka iive na iwe na rangi nzuri ya kahawia ya wastani.



Kumbuka kuendelea kukoroga mtindi katika kiakaango kingine na ukiona inaanza tu kuchemka zima
jiko.



Kisha chukua zile bamia ulizopika na zimwagine katika huo mchuzi wa mtindi.

 

Pia unaweza ongenea binzali nyembamba na majani ya giligilani na pili pili kavu nyekundu wakati bamia inachemka pamoja na kijiko kimoja kidogf cha chai mafuta ya samli.



Mpatie mlaji ikiwa ni ya moto unaweza kula na chapati, mkate au wali na familia ikafurahia sana sana


 

No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako