Sunday, January 29, 2012

JIFUNZE KUPIKA KEKI HII YA MAZIWA AINA TATU


KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KEKI HII YA MAZIWA AINA TATU

MAHITAJI

240 gram unga wa ngano
1-½ kijiko kidogo cha chai Baking Powder
¼ kijiko kidogo cha chai Salt
5 yai zima, kisha tenganisha ute wa njano na mweupe
240gram Sukari, gawa nusu pembeni
1 kijiko kidogo cha chai Vanilla
30 gram maziwa ya maji
1 kopo la Evaporated Milk
1 kopo la Sweetened au Condensed Milk
60gram za cream nzito kabisa ( Heavy Cream)


KWAJILI YA ICING:


1 kijiko kikubwa cah chakula Heavy Cream, kwajili ya kupambia
3 kijiko kikubwa cha chakula sukari nyeupe ya unga
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEKEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : 1 mpaka masaa 2

Muda wa mapishi : 30 dakika mpaka saa 1
Ukubwa na Idadi : utapata cake 2 


Washa kwanza oven kwa moto wa 350 degrees. Kisha chukua tray yenye size hii 9 x 13 inch unaweza paka siagi au ukaspray. Kisha chukua unga changanaya na baking powder pamoja na chumvi katika bakuli kubwa.

Kisha chukua bakuli safi na kavu weka ute wa yai wa njano pamoja na sukari 180 gram piga kwa kutumia mchapo kwa nguvu sana au kama unatumia mashine basi weka spidi kali.

 

Hakikisha inakua muonekano huu baada ya kupiga na mshine unapata rangi ya cream.



Kisha chukua yale maziwa ya maji pamoja na vanilla kisha chukua mwiko huo na changanya pole pole mpaka vyote vichanganyike vizuri.


Kisha chukua ute mweupe wa yai (egg whites) piga tena kwa kutumia mashine kwa spidi kali mpaka uone imetoa mapovu kabisa na kuongezeka. 



Baada ya kutoa povu basi chukua sukari 60 gram na mimina katika mchanganyiko huo wa ute mweupe wa yai.


Endelea kupiga tena kwa kutumia mashine kwa spidi kali hakikisha imekua laini kabisa kama mapovu lakini isikwe kavu.



Unaona muonekano baada ya kua katika kiwango safi na imetengeneza kama milima miwili?



Chukua ule mchanganyiko mweupe wa yai changanya pamoja na mchanganyiko ule wa unga.



Hakikisha unachanganya pole pole

 


Mpaka ichanganyike vizuri kabisa.


Kisha mimina mchanganyiko wako kwenye tray ulioandaa kwajili ya kuokea hakikisha unasambaza vizuri.

 

Choma kwa dakika 35 mpaka 45 au mpaka toothpic ukitoa inabaki kavu. Mara yangu ya kwanza kuipika keki hii nilifungua oven zaidi ya mara 100 ambayo ni kosa sababu ya harufu nzuri ilioenea jikoni kila muda nahisi labda imeshaiva! Nadhani ndio maana keki yangu ilinywea hahahahaaaa! usifanye kosa hili ingawa taste yake ilikua YUMMO!



Keki yako tayari inarangi safi sana ya kahawia kisha chukua condensed milk, evaporated milk pamoja na heavy cream changanya.


Hakikisha unachanganya pole pole mpaka ichanganyike vizuri.

 

Baada ya keki yako kuiva weka pembeni ili ipoe na ikishapoa, Chukua uma na uitoboe pole pole . 


KIsha chukua mchanganyiko huo wa nmaziwa na cream mwagia juu ya keki na uruhusu ipoe kwa dakika 30. Weka kwenye friji ili ipate ubaridi kabisa isisumbue unapoipamba na icing. Chukua  heavy cream na vijiko 3 vyasukari kisha piga pamoja. 

 

Hakikisha unapiga mpaka inalainika kabisa.


Hakikisha unapakaza vizuri icing yako juu ya keki yote ili kuongeza ladha, ingawa mimi huwa nagawa nusu napaka na nusu sipaki maana sio watu wote wanapenda cream. Umeona muonekano baada kukata kipande? Unaona muonekano wa maziwa sehemu tuliokata kipande cha keki? maziwa unayoweka katika hii keki hayatabadiklisha sana keki yako iwe tepe tepe bado itakua na hali ya sponji.



Keki hii asili yake ni nchi ya spain wao wanapenda sana kupambia kwa juu matunda aina ya peaches na cherries. Kwakua ilikua ni msimu wa maembe mi nikaona kwanini nisipambie maembe ?!


Baada ya kupaka cream kwa juu kisha pamba na maembe na kata vipande kama muonekano katika picha.



Ukitafuna utaona sponji safi kabisa na ladha safi
 


Pia hata hotelini unaweza kuuza keki hii kama chakula kitamu baada ya mlo kamili
 



Waandalie nyumbani waweze kufurahia keki hii kwa chai ya jioni au baada ya chakula.

Wednesday, January 25, 2012

JIFUNZE KUPIKA PANCAKE YA MBOGA MAJANI


RECIPE YA PANCAKE NA MBOGA MAJANI

MAHITAJI

480 gram unga wa ngano
120 gram maziwa ya maji
5 gram chumvi
50 gram sukari
2 mayai ya kuku
50 gram mafuta ya maji

1 kitunguu kikubwa katakata vipande vidogo
1 nyanya kubwa katakata vipande vidogo toa mbegu za ndani2 pili pili mbichi kata kata vipande vidogo (sio lazima)


majani ya gili gilani kwajili ya kupambia


JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO NA PICHA HAPO CHINI

Muda wa kuandaa : Dakika 15

Muda wa kupika : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 2
Idadi ya pancake : Kiasi cha 4 mpaka 6



Chukua unga, sukari, chumvi, maziwa, na mafuta ya maji pamoja na mayai changanya kwa pamoja kwa kutumia mchapo kisha weka pembeni unga wako, Kisha katakata pilipili, nyanya na kitunguu kama uonavyo katika picha.



Chukua kikaango kisha weka mafuta kiasi na sambaza vizuri kisha pata moto mimina kati kati ya kikaango unga wako na usambaze uenee kwenye kikaango chote.



Hakikisha unga ni wakutosha katika kikaango ili pancake yako iweze kua nene na mboga majani ziweze kutosha iache iive kwa dakika 3 kwa moto wa wastani, Ikishaanza tu kutoa kama mapovu kwa juu kuonyesha dalili ya kua itakua imeiva chini na inaendelea kuchemka kwa juu basi tupia vipande vya nyanya, korienda na kitunguu kisha geuza chini kuwe juu.



Baada ya kuigeuza utaona rangi ya kahawia upande ule uliokua chini inamaa imeshaiva upande wa kwanza pia upande wa pili ambao unamboga pika kwa dakika 3 na kisha toa itakua imeiva pia unaweza mwagia mafuta kiasi kw apembeni ili yaingie chini ya pancake yako na isiweze kuungua na kushika katika kikaango.



Baada ya dakika 3 itoe itakua imeiva na itakua na harufu safi sana ya kuvutia hakikisha unamapatia mlaji ikiwa yamoto.



Pancake hii unaweza kunywa na chai asubuhi au jioni saa 10 kama kitafunwa tu cha kawaida. Pia unaweza kula kama mlo kamili kwa mchana au usiku pamoja na chuzi wa nyama samaki au hata maharage ya nazi na familia ikafurahia sana sana.

Monday, January 23, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA BISKUTI ZA UNGA WA NGANO NA VIAZI VYA KUCHEMSHA


BISKUTI ZA UNGA WA NGANO NA VIAZI VYA KUCHEMSHA
MAHITAJI

480 unga wa ngano ( self raising unapatikana katika maduka mengi tu)

3 kijiko kikubwa cha chakula siagi au butter, iache wazi katika joto la chumba ili iyeyuke
5 gram chumvi
1 kijiko kikubwa cha chakula fresh dill ichop chop vizuri kabisa ( sio lazima)
2 viazi vikubwa ( vichemshe katika maji moto kisha viponde ponde)
3 kijiko kikubwa cha chakula maziwa ya maji

 
JINSI YA KUANDA FATILIA PICHA NA MAELEOZ HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : Dakika 30

Muda wa mapishi : Dakika 30
Idadi ya biscuti : Kiasi cha biscuti 20 mpaka 25


Chukua unga wako weka katika bakuli safi na kavu kisha washa oven kwa moto wa 450F.



Kisha changanya siagi, chumvi, unga na majani ya dill, Hakikisha unachanganya vizuri na ichanganyike safi kabisa.



Kisha chukua vile viazi vya kupondwa pondwa na uchanganye katika unga pamoja na maziwa ya maji na uhakikishe inachananyika vizuri kabisa.

 

Kwa kukanda pole pole na kwa umakini kwa dakika 5 tu utaona mchanganyiko wako upo safi kabisa na muonekano ndio huu.



KIsha unaanza ku roll kwa kutumia mpini  huo mchanganyiko wako wa unga hakikisha juu ya meza unayosukumia umeweka unga wakutosha ili mcnganyiko uweze sukumima vizuri na usinatie kwenye meza.



Kisha kata maumbo aina yeyote upendayo kwa kutumia cutter.



Baada ya kukata hakikisha unatoa miduara yako na kuiweka pembeni kisha unaliunganisha lile unga lililobakia na kusukuma tena na unendelea zoezi la kukata kisha unarudia zoezi hili mpaka utakapo malizia mchanganyiko wa unga wote.

 

Paka kwa juu mafuta katika tray unayotaka kuokea kisha ziweke biscuti juu yake na uchome katika oven. Kwa wale wanaopenda sukari basi vunja mayai kwa pembeni au unaweza tumia maziwa ya maji na ukatukmia brush unapaka yale mayai au maziwa kwa juu ya biscuti kisha unanyunyizia sukari kwa juu na biscuti zako zikiiva zitakua na ladha ya sukari.

 

Kisha choma katika oven kwa dakika 20 mpaka 25 au mpaka zitakapo kua na rangi ya kahawia.



Ni rahisi sana au sio? Kitafunwa safi kabisa mhhh , Kitafuna hiki kitakuafanya kila ukipita karibu yake unatupia mdomoni kipande kimoja au viwili.

 

Muonekano safi kabisa wa biscuti hizi na unaweza zihifadhi kwa muda mrefu kwa matumizi ya baadae na bila ya kuharibika.



Sio lazima uweke dill unaweza hata kutumia maji ya machungwa, maganda ya limao, au ladha ya vanila.



WAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE KITAFUNWA HIKI RAHISI KW AKUANDA NA GHARAMA NAFUU.


 

JIFUNZE RECIPE ZA CHAPATI, MAANDAZI NA SAMOSA

HABARI WAPENZI WA BLOG MCHANA WA LEO HII NITAWEKA RECIPE YA VYAKULA VYOTE HAPO CHINI PAMOJA NA VINGINE VIPYA

PIA KWA WALE WANAOPENDA KUPIKA CHAPATI NA NYAMA YA MBUZI UNAWEZA CLICK LINK HII HAPO CHINI



NA WALE WANAOPENDA KUPIKA MAANDAZI YA LADHA YA NAZI NA HIRIKI CLICK LINK HIYO HAPO CHINI KWA MAFUNZO ZAIDI


WAPENZI WA SAMOSA PIA UNAWEZA CLICK LINK HIYO HAPO CHINI NA UTAONA JINSI YA KUANDAA KWA UFASAHA


CHEF ISSA


Sunday, January 15, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA MUFFIN YA MATUNDA NA NAFAKA KWA LADHA SAFI KABISA


HAPA CHINI NI MUFFIN YA MATUNDA NA NAFAKA

MAHITAJI

360 gram unga wa ngano

120 gram zabibu kavu
1 kijiko kikubwa cha chakula  Baking Powder
5 gram chumvi
1/2 kijiko cha chai unga wa Cinnamon
3 apple au Pears chop chop vipande vidogo 
60 gram chop chop korosho au walnuts
180 gram ya maziwa ya maji
1 kijiko kidogo cha chai vanila essence
2 kijiko kikubwa cha chakula olive au corn Oil
sukari nyeue ya unga kwajili ya kupambia

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : dakika 30

Muda wa mapishi : dakika 30
 Idadi ya walaji : 4
Idadi ya chakula : 12 muffins


 
Kaanga korosho au walnuts mpaka zinukie kwa dakika 6 hadi 8. Pia unaweza tumia Oven kwa moto wa 350F kwa dakika 5 hadi 6.



Chukua gram 120 za korosho na weka katika blenda kisha ongeza kijikokikubwa cha chakula 4 maji safi baridi na kisha saga na weka pembeni.

 

Katika bakuli safi na kavu weka unga wa ngano, sukari, baking powder, chumvi na cinnamon kisha changanya.



KIsha ongeza zabibu kavu, vipande vya apple au pears pamoja na korosho zote zilizobakia na uendelee kuchanganya mchanganyiko wako uchanganyike vizuri .



Kisha katika bakuli nyingine changanya vanila essence, zile korosho ulizosaga pamoja na maziwa ichanganyike vizuri pamoja na olive oil.




Chukua ule mchanganyiko wenye maziwa na korosho kisha umwagie ndani ya ule mchanganyiko wa unga na uendelee kuchanganya vizuri.

 

Hakikisha unachanganya pole pole mpaka mchanganyiko wako unachanganyika vizuri ( mchanganyiko huu utakua unanasa nasa). usichanganye muda mrefu utaharibu.

 

.Washa oven yako kwa moto wa 400F.Kisha weka karatasi kama zionekanzo kwenye picha ni maalumu kwajili ya kuokea muffin ziwe 12 kisha tumia cooking spray. Kwa kutumia Spray itafanya urahisi wa kutoa wakati ikishaiva kama huna spray basi tumia mafuta ya siagi.




Hakikisha unagawa sawa kwa sawa ili ziweze kutosha vikombe 12 vya muffin.



Nyunyizia kwa juu sukari yakutosha unaweza tumia ya unga au ya kawaida pia inaweza kua nyeupe au ya kahawia ni pendekezo lako tu.



Choma katika oven kwa dakika 20, Au mpaka ukichoma kwa kijiti kati kati kinatoka kisafi bila unga mbichi.



Toa katika pan ya kuokea , kisha zipoze katika wire rack. Maffin yako itakua kavu (crusty)  na crunch nyingi toka kwa korosho kila unapotafuna. Na mapears au apple yanaweka unyevu ndani kwakua ni malaini. Ile korosho ya kusagwa inafanya muffins yako iweze kutafunika kilaini. Hakikisha unampatia mlaji zikiwa zamoto kwani ndio zinapendeza sana kwa ladha pia unaweza kula wakati wa chai ya saa10 jioni au chai ya asubuhi.



Unaweza tengeneza mchanganyiko huu kisha ukahifadhi katika friji kwa matumizi ya kesho asubuhi endapo umeandaa usiku au ukahifadhi kwenye friza kwa matumizi ya mwezi au wiki na ukapata ubora ule ule.



WAANDALIE FAMILIA YAKO KWA KITAFUNWA CHA ASUBUHI ILI WAANZE SIKU KWA FURAHAA.