KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KEKI HII YA MAZIWA AINA TATU
MAHITAJI
240 gram unga wa ngano
1-½ kijiko kidogo cha chai Baking Powder
¼ kijiko kidogo cha chai Salt
5 yai zima, kisha tenganisha ute wa njano na mweupe
240gram Sukari, gawa nusu pembeni
1 kijiko kidogo cha chai Vanilla
30 gram maziwa ya maji
1 kopo la Evaporated Milk
1 kopo la Sweetened au Condensed Milk
60gram za cream nzito kabisa ( Heavy Cream)
KWAJILI YA ICING:
1 kijiko kikubwa cah chakula Heavy Cream, kwajili ya kupambia
3 kijiko kikubwa cha chakula sukari nyeupe ya unga
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEKEZO HAPO CHINI
Muda wa maandalizi : 1 mpaka masaa 2
Muda wa mapishi : 30 dakika mpaka saa 1
Ukubwa na Idadi : utapata cake 2
Muda wa mapishi : 30 dakika mpaka saa 1
Ukubwa na Idadi : utapata cake 2
Washa kwanza oven kwa moto wa 350 degrees. Kisha chukua tray yenye size hii 9 x 13 inch unaweza paka siagi au ukaspray. Kisha chukua unga changanaya na baking powder pamoja na chumvi katika bakuli kubwa.
Kisha chukua bakuli safi na kavu weka ute wa yai wa njano pamoja na sukari 180 gram piga kwa kutumia mchapo kwa nguvu sana au kama unatumia mashine basi weka spidi kali.
Hakikisha inakua muonekano huu baada ya kupiga na mshine unapata rangi ya cream.
Kisha chukua yale maziwa ya maji pamoja na vanilla kisha chukua mwiko huo na changanya pole pole mpaka vyote vichanganyike vizuri.
Kisha chukua ute mweupe wa yai (egg whites) piga tena kwa kutumia mashine kwa spidi kali mpaka uone imetoa mapovu kabisa na kuongezeka.
Baada ya kutoa povu basi chukua sukari 60 gram na mimina katika mchanganyiko huo wa ute mweupe wa yai.
Endelea kupiga tena kwa kutumia mashine kwa spidi kali hakikisha imekua laini kabisa kama mapovu lakini isikwe kavu.
Unaona muonekano baada ya kua katika kiwango safi na imetengeneza kama milima miwili?
Chukua ule mchanganyiko mweupe wa yai changanya pamoja na mchanganyiko ule wa unga.
Hakikisha unachanganya pole pole
Mpaka ichanganyike vizuri kabisa.
Kisha mimina mchanganyiko wako kwenye tray ulioandaa kwajili ya kuokea hakikisha unasambaza vizuri.
Choma kwa dakika 35 mpaka 45 au mpaka toothpic ukitoa inabaki kavu. Mara yangu ya kwanza kuipika keki hii nilifungua oven zaidi ya mara 100 ambayo ni kosa sababu ya harufu nzuri ilioenea jikoni kila muda nahisi labda imeshaiva! Nadhani ndio maana keki yangu ilinywea hahahahaaaa! usifanye kosa hili ingawa taste yake ilikua YUMMO!
Keki yako tayari inarangi safi sana ya kahawia kisha chukua condensed milk, evaporated milk pamoja na heavy cream changanya.
Hakikisha unachanganya pole pole mpaka ichanganyike vizuri.
Baada ya keki yako kuiva weka pembeni ili ipoe na ikishapoa, Chukua uma na uitoboe pole pole .
KIsha chukua mchanganyiko huo wa nmaziwa na cream mwagia juu ya keki na uruhusu ipoe kwa dakika 30. Weka kwenye friji ili ipate ubaridi kabisa isisumbue unapoipamba na icing. Chukua heavy cream na vijiko 3 vyasukari kisha piga pamoja.
Hakikisha unapiga mpaka inalainika kabisa.
Hakikisha unapakaza vizuri icing yako juu ya keki yote ili kuongeza ladha, ingawa mimi huwa nagawa nusu napaka na nusu sipaki maana sio watu wote wanapenda cream. Umeona muonekano baada kukata kipande? Unaona muonekano wa maziwa sehemu tuliokata kipande cha keki? maziwa unayoweka katika hii keki hayatabadiklisha sana keki yako iwe tepe tepe bado itakua na hali ya sponji.
Keki hii asili yake ni nchi ya spain wao wanapenda sana kupambia kwa juu matunda aina ya peaches na cherries. Kwakua ilikua ni msimu wa maembe mi nikaona kwanini nisipambie maembe ?!
Baada ya kupaka cream kwa juu kisha pamba na maembe na kata vipande kama muonekano katika picha.
Ukitafuna utaona sponji safi kabisa na ladha safi
Pia hata hotelini unaweza kuuza keki hii kama chakula kitamu baada ya mlo kamili
Waandalie nyumbani waweze kufurahia keki hii kwa chai ya jioni au baada ya chakula.
Waandalie nyumbani waweze kufurahia keki hii kwa chai ya jioni au baada ya chakula.
Hi,
ReplyDeleteTunashukuru sana kwa kutusaidia kuboresha mapishi yetu, Ila tunaona POicha tu ingawa juu umeandika fatilia na maelekezo chini, Je kuna maelekezo au ni pc yangu??? Tungefurahi kama tungepata vipimo na maelekezo..
Issa...great work you are doing. But some of us are really not that good and we shall appreciate getting measurements of each item i.e. how many cups of sugar, flour etc etc
ReplyDeleteKaka, mbona ombi langu umeliweka kapuni? Niliomba msaada kujua jinsi ya kupika nyama nzuri ya kukaanga lakini mpaka sasa hujanijibu ama wataka niachwe na shemejiyo? tafadhali nisaidie kaka.
ReplyDeletemaelezo mkuu...
ReplyDeletetunasubiri kwa hamu kubwa sna hayo maelezo ..usikawie kutuwekea
ReplyDeleteTunaomba basi usiwe unakawia kuweka maelezo kwenye recipe, au kusiwe na interval kubwa ya muda baada ya picha na kupost maelezo, otherwise mvuto unakwisha. ni ushauri tu
ReplyDeleteNimefuatilia kwa makini hatua kwa hatua nimeona namna ulivyoelekeza upikaji wa keki Nimejaribu na imetoka bomba ingawa haikufanana na ya kwako lakini Tamu sana. ASANTE CHEF endeleA kutuelimisha
ReplyDelete