Monday, February 13, 2012

JIFUNZE KUPIKA KITAFUNWA HIKI CHA MCHANGANYIKO WA UNGA WA MCHELE NA DENGU


NI RAHISI SANA NA NAFUU JIFUNZE KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI CHA MCHANGANAYIKO WA UNGA WA MCHELE NA UNGA WA DENGU

MAHITAJI

480 gram unga wa mchele (laini vizuri na hakikisha hauna mawe)

2 kijiko kikubwa cha chakula unga wa dengu
2 kijiko kikubwa cha chakula siagi (butter)
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga

JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO NA PICHA HAPA CHINI

Muda wa maandalizi : dakika 30
Muda wa mapishi : Dakika 15
Kiasi : Utapata vipande 10 hadi 15

 

Chukua siagi na uiyeyushe kiasi kisha chukua vitu vyote na uchanganye kwa mara moja.



Unaweza ongeza maji kiasi kama mchanganyiko wako bado ni mgumu.



Tunaanza kutumia kifaa chenye nyota moja tu pia unaweza tumia kifaa chenye nyota 2 kama huna kifaa basi unawz tumia mikono kunyonga vipande vidogo na ukapika.


Kata kipande cha unga uliochanganyika kisha weka katika mashine. Pia unaweza tumia hata mshine ile ya kutengenezea biscuti na ni rahisi kupatikana katika maduka ya vifaa vya chakula kila kona mjini.


Funga kifaa chake kwa juu.



Kandamiza kifaa hiki kisha zungusha ili kupata mduara mzuri na itakua na umbo la nyota.



Unaweza tengeneza mduara wa ukubwa unaotaka.



Kisha weka katika mafuta yamoto ili kukaanga.



Hahahhahaaaa kwa mara ya kwanza sio rahisi kuweza kuutunza mduara lazima utabonyeza na kuaharibu kiasi shepu yake. Mara ya pili na kuanedelea utakua mkono umezoea na utapata mduara mzuri. Hata ikibongea usijali maana ladha itabaki baabkubwaaa!


Kwa kutumia kifaa hiki cha nyota tatu pia unaweza ukatengeneza umbo la ajabu kweli lakini ladha itabaki kua safi sana. Kadiri unavyoendelea kutengeneza ndio na mkono wako utaweza kuzoea.


Endelea kukandamiza ili upate mzunguko mkubwa na umbo la kitafunwa chako.


Umeona muonekano wa umbo hili?.



Pia unaweza kutengeneza moja kwa moja kwenye mafuta endapo sasa utakua umezoea na mkono umeweza kuwa na ujasiri. Zungusha tu kama mwanzo na utapata umbo safi la kitafunwa chako



Hakikisha unakaanga kwa kiwango unachopenda wewe unaweza kaanga ikawa light brown au  golden brown.



Ukishatoa katika mafuta unakausha afuta kwa kuweka juu ya towel au juu ya napkin za karatasi ili inyonye mafuta.



Acha zipoe kisha weka na uifadhi katika kontena



Unaona muonekano wa maumbo safi ya duara






Huu ni mchanganyiko wa miduara na maumbo ya zig zag ila ladha ni moja




WAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE KITAFUNWA HIKI


 

4 comments:

  1. inaelekea ni kitafunwa kitamu, lkn tunaomba maelezo kaka.... Kazi njema

    ReplyDelete
  2. Hivyo vifaa vya kutengeneza shape vinapatikana wapi?

    ReplyDelete
  3. nilikula hivi vitu (sikumbuki Jina) nilipewa na rafiki yangu Mhindi walipikiwa na mama yao wakati wa Deepevali

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako