Sunday, April 1, 2012

JIFUNZE JINSI YA KUPIKA PILAU YA MBOGA MAJANI


KAA TAYARI KABISA KWA KUJIFUNZA KUPIKA PIALU HII YA MBOGA MAJANI

MAHITAJI

250 gram mchele wa basmati
1 kijiko binzali nyembamba (cumin seeds)
1/2 kijiko kidogo cha chai garam masala
1/2kijiko kidogo cha chai coriander powder
1/4 kijiko kidogo cha chai turmeric powder
60 gram njegere za kuchemshwa
1 kitunguu maji chop chop
3 nyanya za kuiva nazo chop chop
1 kijiko kidogo cha chai tangawizi ya kusagwa
1kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kusagwa
2 pili pili mbuzi, kisha kata vipande vidogo vidogo
60 gram korosho au karanga za kukaanga (sio lazima)
1 kijiko kidogo cha chai siagi au mafuta ya samli kwa ladhamajani ya giligilani na majani ya mint kwa kupambia na kuongeza ladha


JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI


Muda wa maandalizi : Dakika 15
Muda wa mapishi : Dakika 30
Idadi ya walaji : Watu 2

 

Kwenye kikaango weka kijiko kimoja cha mafuta ya kupikia kama ni samli au siagi, kisha graham masala, unga wa manjano, binzali nyembamba na unga wa corienda kaanga kidogo kisha weka kitunguu swaumu, kitunguu maji, tangawizi, pilipili mbuzi na nyanya zote ziwe chop chop vipande vidogo kama inavyoonekana kweny picha. Kisha weka chumvi, karafuu na pili pili manga endelea kukaanga.



UKisha pata harufu ya kunukia saafi imeenea jiko zima hahahahaaaa !! na mboga zako ziwe zimeanza kuiva na hazijaregea basi anza kumimina mchele kidogo.



Endelea kukaanga wali wako na ukiuchanganya uchanganyike vizuri kabisa na mboga kwa dakika 2 au 3inategemea na moto wa jiko lako au ubora wa sufuria yako.



Kisha weka gram 600 za maji ni sawa na nusu lita na 100 gram za maji kisha koroga na funika na mfuniko acha iive kwa dakika 10 kwa moto wa wastani.



Baada ya dakika 10 itakua imekaribia kabisa kuiva, kisha weka njegere za kuiva na koroga kidogo ichanganyike kisha pika kwa dakika 2 tena.


Baada ya pilau yako kuiva basi juu yake rushia majani ya mint au giligilani kuongeza uzuri wa rangi, ladha na harufu safi sana katika pilau yako.


Mwisho kabisa pia ukiwa mpenzi wa siagi mwagia kwajuu kiasi au unaweza mwagia samli hii nikuongeza harufu nzuri na ladha zaidi.



Usisahau kwajuu kabisa mwagia karanga au korosho za kukaangwa.  Kumbuka kuaandaa mchuzi mzito kabisa pembeni kwajili ya kulia chakula chako. Kwamapishi haya haya unaweza pika ikawa pilau ya nyama ya kuku, mbuzi au ng'ombe kumbuka kuikata kata nyama na unaiweka mwanzo kabisa wakati unakaanga viungo itaiava sambamba na wali wako na itapendeza sana.


7 comments:

  1. kaka nakuomba utuwekeye viungo vya pilau angalau tuone picha,mie hayo majina ya viungo yananisumbuwa sana naomba kaka yangu uniwekey picha ya viungo vya pilau ili nami nijitaidi kupika pilau inanisumbua sana kwa sababu sifaham viungo,tunashkuru sana kaka kwakujitoley kwako kutufunza mambo mengi ya mapishi,capati nilishajuw kwasababu yako kaka unatusaidiya mno mno kabisa kila la kheri kaka yangu.

    ReplyDelete
  2. Hallo Chef..
    nimekua nikitembelea sana blog yako n nzuri na nmefurahi sana cos napenda kufaham kupika chakula ambacho hakiishi ham, yan ukiuliza familia niwapkikie nn utaskia kile cha siku ile haha!...
    swali langu ni, Je siwezi tumia mchele mwingine kuandaa pilau hii ya mboga n lazima kutumia Basmati? tafadhali nijibu nimependa sana pishi hili

    ReplyDelete
  3. asante sana. inavutia sana , nitajaribu.garam masala ikikosekana je?

    ReplyDelete
  4. HII INAVUTIA SANA NITAIPIKA WEEKEND INSHAALLAH.

    TWEETY

    ReplyDelete
  5. asante sana,naipenda blog yako na nnashauri wengine waitumie mana wengi tunajua vya kawaida ila mafunzo yako ni noma....

    ReplyDelete
  6. asante sana kutufundisha, nimepika hii pilao, ni tamu sana jamani. namshukuru sana. tatizo sikuwa na camera. nitatafuta next time.
    Mungu akubariki

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako