JIFUNZE KUANDAA KEKI HII SAFI KABISA YA BILA MAYAI KWA MTINDO NA LADHA TOFAUTI NI RAHISI NA NAFUU KWA GHARAMA
MAHITAJI
300 gram unga wa ngano
240 gram sukari ya unga
1 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
3 kijiko kikubwa cha chakula cocoa powder
1/3 cup vegetable oil ( corn oil au olive oil)
1 kijiko kikubwa cha chakula siki au vinegar
1 kijiko kidogo cha chakula vanilla essence
240 gram majibaridi safi na salama
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI
Muda wa mapishi : dakika 15
Cook Time: Dakika 30
Ujazo : Keki moja yenye vipande 7"
Chukua unga wa ngano, sukari ya unga, chumvi na baking powder chekecha katika chujio vizuri kisha hifadhi katika bakuli
Kisha changany vizuri uchanganyike
Katika bakuli tofauti safi chukua maji, vegetable oil, vinegar na vanilla essence tumia mchapo na changanya vizuri
Chukua mchanganyiko wako wa maji na mafuta kisha mimina pole pole kwenye mchanganyiko wenye unga na hakikisha huweki mabonde.
Pole pole mpaka unapata mchanganyiko safi na mzito
Kisha paka mafuta na mwagia unga chombo chako la kubekia lenye upana na inchi 7.
Mimina katika chombo chako cha kubekia
Choma katika oven iliyokwisha washwa kwa moto wa 360F kwa muda wa dakika 30 au mpaka utakapo choma tooth pickkati kati ya keki na itoke safi. Pia baada ya kupika kwa dakika 30 utaona kabisa keki yako inaanza kuachia chombo cha kubekia.
KIsha toa keki yako katika ovena na iache nje ipoe kwa dakika 1. Kisha geuza chini juu chombo cha kubekia juu ya waya au wavu iache hapo ipoe.
Usiogope kuona keki yako imeungua au kua na rangi mbaya kwa chini hii inatokana unga uliomwagia wakati unataka kumimina mchanganyiko wa keki yako
Pia keki hii unaweza weka katika friji kwa matumizi ya baadae
Mimi na familia yangu huwa tunapenda kukata vipande na tunamwagia sukari yaunga juu
Kipande cha keki kinavyoonekana na ni sponge bombastick kabisa kwa matumizi halali ya chai jioni au asubuhi au wakatai wowote majumbani na mahotelini
sukari ya kawaida haifai?
ReplyDeleteyummy yummy me ni mpenzi sana wa keki sema zile za kununua wanaweka sukari sana na ice-sugar...
ReplyDeleteubarikiwe kaka kwa mapishi hivi unasaidia sana familia zetu kwa mlo bab'kubwa
nitaleta picha