Sunday, September 30, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA VIAZI VYAKUKAANGA NA BINZARI NYEMBAMBA

 
NIRAHISI SANA UTENGENEZAJI WAKE PAMOJA NA GHARAMA NAFUU NA MUDA WA MAANDALIZI NI MCHACHE
 
MAHITAJI
 
500 grams viazi ulaya
1 kijiko kimoja kidogo cha chai binzali nyembamba
1/4 kijiko kidogo cha chai manjano
1/2 kijiko kidogo cha chai pili pili ya unga (Chilli Powder)
5 gram maji ya limao au Lemon Juice
5 gram chumvi
5 gram majani ya korienda
 
JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi Dakika 15
Muda wa mapishi Dakika 15
Idadi ya walaji :  Watu 2
 
 
 Mimi nimetumia viazi ulaya vyekundu wewe unaweza tumia viazi ulaya vyovyote vile pia na binzali nyembamba.

 
 Kata kata viazi katika vipande vidogo vidogo

 
Washa moto na kisha weka kikaango katika moto na kijiko kimoja kikubwa cha samli au blue band. kisha weka binzali nyembamba na manjano unga wa pili pili na uendelee kukaanga
 
 
 
Kabla viungo havijaungua weka viazi na chumvi kisha endelea kukaanga.

 
Hakikisha unakoroga vizuri vichanganyike kabisa

 
KIsha mwagia maji na ufunike na mfuniko. Maji yanasaidia kuivisha viazi vizuri. Koroga kidogo ili viazi visishike chini.
 
 
 
Inachukua kama dakika10 hadi 12 bonyeza viazi na kidole au mwiko ukiona vimekua laini, basi jua vimeiva. Kisha mwagia majani ya gili gilani na maji ya limao kuongeza ladha safi.
 

 
Mpatie mlaji chakula hiki kikiwa chamoto unaweza kula na wali, pialu au chapati na mchuzi wa nyama.


 
CHAKULA HIKI KINAMUONEKANO SAFI SANA
 


7 comments:

  1. ahsante kaka kwa pishi... lakini tunaomba utuwekee maelezo na mahitaji ili tukapike w'end hii kwani kwa picha inaonekana ni tamu sana! Ahsante

    ReplyDelete
  2. Bado tunasubiria mahitaji na maelekezo, w'end ndo imeanza kaka

    ReplyDelete
  3. Kweli nimejaribu hili pishi naona limetoka kushinda hata la mpishi mwenyewe, kweli nafurahia sana hii blogu. Aendelea kutupa aina za mapishi kaka yetu. Asante sana.

    ReplyDelete
  4. kaka mbona hauweki mahitaji na maelezo jamani? bado tunasubiria

    nawasilisha

    ReplyDelete
  5. Anonymous Sunday, October 14, 2012 6:48:00 AM

    umelipikaje? mie mwenzio limenishinda na kaka yetu hataki kutuwekea maelezo, viazi vinachemshwa au vinakaangwa, tafadhali niambie ikiwezekana nipikie wageni kesho coz nina wageni

    ReplyDelete
  6. duuh kweli pish zuri,,lakin cjui nikaange au nichemshe maana picha siielewi hata jamani kaka

    ReplyDelete
  7. DU JAMANI WADAU WENZANGU HAPO HIVI MNAFATILIA KWA MAKINI KWELI JAMANI,MBONA MIMI NINAMULEWA VIZURI SAANA,SOMA MALEKEZO KWA UTULIVU ACHENI PAPARA.AU PANIK.AMESEMA UKISHA KATA VIAZI VDGOVDGO UNANZA WEKA MAFUA KWAKIKANGO EITHER IWE BLUEBAND AU SAMLI,THEN YAKIPATA MOTO UNAWEKA BINZARI NYEMBAMBA NA NA MANJANO NA PILPIL MANGA UNAKANGA KDGO THEN UNAMWAGIA VIAZI ULOKWISHA KATAKTA PEMBENI UNAKOROGA KDGO UNATIA VOMAJI KIDGO SIO MIMAJI KIBAO,THEN WAFUNIKA SIMPLE VIKASHAIVA UNACHUKUA KIMOJA WABONYEZA UKIONA KIMELAINIKA UJUE TAYARI MLOWAKO, NADHANI MMEMUELWA.MH KAZI IPO KUELWA WATU WAZITO DUH.

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako