Friday, October 5, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA SALAD YA PASTA AINA YA PENNE

 
SALAD YA PASTA NI RAHISI KUTENGENEZA NA INAPENDEZA SANA LICHA YA KUA SALAD UNAWEZA KULA KAMA MLO KAMILI
 
MAHITAJI
 
170 grams Penne Pasta, 
170 grams cherry tomatoes, 
170 grams Matango, menya na katakata
2 majani ya vitunguu
100 gram maharage
3 kijiko kikubwa cha chakula Olive Oil
60 gram Limao juice
1 fungu fresh Basil chop chop
5 gram chumvi
5 gram kitunguu swaumu
5 gram pili pili manga
55 grams Feta cheese,
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : dakika 15
Muda wa mapishi : Under 15 min
Idadi ya walaji : 2
 
 
Muonekano katika maandalizi

 
Pika pasta kwa kuafata maelezo katika paketi. Chemsha pasta ziive kisha chuja maji moto na poza kwa maji baridi kisha chuja tena na ziweke pembeni.

 
Kwenye bakuli kubwa weka mchanganyki wa vitu hivi ukiwa umevikatakata vipande vidogo Nyanya, matango, majani ya kitunguu mabichi, maharage.

 
Weka pasta kwenye mchanganyiko wa mboga na kisha changanya vizui. 
 
 
Chukua bakuli leney mfuniko na kisha changanya olive oil, juice ya limao, majani ya basil, kitunguu swaumu, chumvi, na pili pili manga.

 
Funika na mfuniko kisha tikisa vizuri.

 
Kisha mwagia juu ya pasta na uendelee kuchanganya vizuri;

 
Muonekano baada ya kuchanganya vizuri.

 
Funika mchanganyiko wa salad na uache katika friji kwa masaa 2 pia inaweza kukaa masaa 24

 
Wakati wa kumpatia mlaji weka juu feta cheese. Unaweza kula kama mlo mwepesi wa mchana auusiku pamoja na mkate.

 
RECIPE SAFI KWA WEEKEND HII
 


4 comments:

  1. Hi Habari,
    Mimi nimekuwa nikiangali blog yako na kuifurahia sana. Nimeifahamu sio muda mrefu. Maoni yangu ni naona ni vema ukaweka vyakula vinavyohitaji katika mapish fulani pamoja na picha.. Ukiweka picha tu inakuwa ngumu kujua vyote sababu vingine vinaonyeshwa kama vimechanganywa. Mfano ni hii salad kuna mchanganyiko uko kwenye bakuli hauelezi ni hasa umeweka humo.

    ReplyDelete
  2. kaka issa uwe unaweka maeleza ya jinsi ya kuandaa hatua kwa hatua ili iwe rahisi kupractice nyumbani
    Mdau wa mapishi

    ReplyDelete
  3. Hongera kwa kazi nzuri sana kaka! nadhani ni kwa recipe hii na hiyo ya viazi ndo hujaweka mahitaji na maelezo ya picha. Ningependa ungeedelea na mtindo uliokuwa nao mwanzo. Kazi njema

    ReplyDelete
  4. Good work bro.naungana na wadau hapo juu recipe bro itakamilisha kazi yako iwe juu zaidi

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako