Monday, December 31, 2012

JIFUNZE KUTENGENZA WALI HUU WA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI KOROSHO NA NYAMA

 
JIFUNZE KUANDAA WALI HUU WA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI NA KOROSHO PIA UNAWEZA KUCHANGANYA NA NYAMA YA NGOMBE, MBUZI, KUKU AU SAMAKI MFANO PRAWNS NA INAPENDEZA SANA SANA
 
MAHITAJI
 
1 kilo ya wali uliokwisha pikwa
1/2 ya mchanganyiko wa mboga majani zozote upendazo
2-3 Spring Onions au majani mabichi ya vitunguu katakata
120 gram korosho
400 gram sawa na 1 kopo la uyoga au fresh
5 gram kitunguu swaumu cha kusagwa
1 Tangawizi mbichi osha na katakata ndogo ndogo sana
4 kijiko kidogo cha chai mafuta ya ufuta
2 kijiko kikubwa cha chakula Soy Sauce
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
500 gram ya nyama au kuku au prawns kama utapenda kuchanganya

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAP CHINI

Muda wa maandalizi : Dakika 15
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji  Watu 2
 
 
Ili kufanya mapishi yangu yawe rahisi mimi huwa natumia mchanganyiko wa mboga majani zilizogandishwa tayari ukienda katika supermaket utazikuta huwa kuka mchanganyiko wa carrot, maharage, njegere na mahindi ya njano. Huwa nachemsha kwa dakika 2 tu katika maji moto sana. kisha toa katika sufuria na uzijchuje ziweke pembeni

 
Unatakiwa kuaanda kila kitu na kiwe karibu na kiaango chako kisha washa moto mkali weka kiaango kipate moto. Kikishapata moto tu, weka mafuta ya ufuta kisha pata moto weka korosho na kaanga ziwe na rangi nzuri ya kahawia toa ziweke pembeni. Kama utatumia nyama ya ngombe, mbuzi, kuku au prawns unaweza zikaanga pamoja na korosho hizi ili ziive pamoja.

 
Katika kiaango hicho hicho weka majani mabichi ya kitungu, tangawizi, na kitunguu swaumu kaanga kwa sekunde 6 hadi 7 utapata harufu safi sana.

 
Kisha ongezea ule mchanganyiko wa mboga ulizozichemsha na kisha ukazichuja kaanga kwa sekunde 5 hadi 6.

 
KIsha ongezea uyoga ulioukata kata. kaanga pia kwa sekunde 10 tu.

 
Sasa ni zamu ya kuongeza soy sauce pia kama ni mpenzi wa pili pili unaweza ongezea  chilli sauce pia unakaanga kwa sekunde 10 hadi 15 tu.

 
Sasa ni zamu ya kuongezea ule wali wako uliopo tayari

 
Koroga vizuri uchanganyike na unaweza kuongezea soya sauce ili kuongeza ladha.

 
Hapa unaongezea korosho pia kama unatumia nyama ongeza pamoja na nyama

 
endelea kuchanganya ichanganyike vizuri

 
Unaweza mwagia kwajuu ya wali wako majani mabichi ya kitunguu au chaives au majani ya giligilani korienda kwa kuongeza ladha na muonekano wa rangi tofauti.
 

Inapendeza sana na chakuala hiki ni kitamua hasa huu ni muonekano baada ya kuivaio
 
Jaribu kuchanganya nyama ya ngombe na ya kuku
 
au changanya nyama ya kuku na prawns katika wali huu na utajifunza kitu muhimu sana
 
au nyama ya mbuzi na ya kuku kwali mchanganyiko huu ni safi sana sana

 
 
CHAKULA HIKI NI KITAMUA SANA NA NI NAFUU SANA KUANDAA WAANDALIE FAMILI WAONE TOFAUTI MWAKA 2013 
 


Saturday, December 29, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA KEKI HII NDOGO YA MCHANGANYIKO WA CREAM NA MATUNDA FERSH

 
KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KEKI HII NGUMU NA MCHANGANYIKO WA MATUNDA NA CREAM
 
MAHITAJI
    MAHITAJI YA KUPAMBIA
2 kg matunda ya Strawberries
6 Kijiko kikubwa cha chakula Sukari
500 gram Whipped Cream
    MAHITAJI KWAJILI YA KEKI
    500gr Unga wa ngano
    5 Kijiko kikubwa cha chakula Sukari
    1 Kijiko kikubwa cha chakula Baking Powder
    1/2 Kijiko kidogo cha chai Salt
    8 Kijiko kikubwa cha chakula unsalted Butter ya baridi
    1 Yai kubwa, Piga piga
    1 Kijiko kikubwa cha chakula maziwa ya maji
    1 yai ute mweupe, piga piga
                           JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : 30 dakika mpaka saa 1
Muda wa mapishi Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 6
Idadi ya keki : Utapat 6 mpaka 8  Shortcakes

 
Toa vikonyo katika matunda ya strawberries.

 
Chukua robo tatu ya matunda ya strawberries weka katika bakuli safi kisha ponda ponda kwa kutumia potato masher.

 
Ponda ponda mapaka upate mchanganyiko laini na safi kabisa. Hii itasaidia kuunganisha shortcakes pamoja.

 
Kisha katakata nusu kwa nusu matunda yaliyobakia.

 
Kisha tupia matunda katika mchanganyiko ulioponda ponda pia changanya na sukari. Kisha changanya pole pole na uiache ipoe kwa dakika 30.

 
Wakati unaendelea, Chukua oven rackiweke mstari wa chini kabisa na uwashe oven kwa joto la nyuzi  425 F. Katika bakuli changanya, unga, 3 Kijiko kikubwa cha chakula sukari, baking powder na chumvi.

 
Kisha kwangua butter kwenye unga. mimi na kwangua hii siagi kwakua natumia mikono kukandai lakini kama unatumia food processor, basi kata vipande vidogo vidogo, Kama unatumia mikono kanda mapaka ichanganyike na kama unatumia mashine basi washa ichanganye mpaka ichanganyike vizuri.


Mimi pia natumia njia nyepesi ya whisk kwajili ya kuchanganya butter na unga

 
Huu ni muonekano baada ya kuchanganyika vizuri.

 
Kwenye bakuli nyingine tumia measuring cup, Changanya mayani yaliopigwa pigwa na maziwa.

 
Kisha changanya unga na maziwa pamoja .

 
Tumia rubber spatula endelea kuchanganya vizuri.

 
Kisha  hamishia mchanganyiko wa unga wako kwenye meza na . KANDA KWA DAKIKA 3 TU USIZIDISHE.

 
Tumia mikono yako kukandamiza mpaka iwe flat kabisa. Kisha tumia biscuit cutter and kisha kata vipande 6 dough rounds.

 
Kisha weka kwenye baking tray, brush tena kwa juu ya biscuti na ute mweupe wa yai

 
Mwagia sukari kwajuu na kisha weka kwenye friji ipoe kwa masaa 2 hours kabla ya kuoka

 
Kisha oka kwenye oven na iwe na rangi ya golden brown, chonma kwa dakika 12 hadi 15. Tumia wire rack weka keki zako na poza kwa dakika 10.

 
Sasa andaa whipped cream. Tumia mashine kwa kupiga na mchapo au mashine.

 
Sasa unaanza kuziunganisha, kata keki katika vipande viwili. Ukishakata tumia kipande cha chini kwa kupanga matunda.

 
Kipande cha chini weka matunda na kisha weka cream kisha funika kipande cha juu.
 
 
 Kisha unaweza kupanba kwa vipande viwili vya strawberries kwajuu ya keki yako na pamba jani la mint kwa kuboresha rangi.
 


JIFUNZE KUTENGENEZA PILAU YA VIAZI ULAYA

 
KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KUFUNGIA MWAKA YA PILAU YA VIAZI ULAYA
 
MAHITAJI

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI













 
 
 
 
 


Tuesday, December 25, 2012

KHERI YA MWAKA MPYA 2013

 
WAPENZI WOTE WA BLOG HII YA CHAKULA BORA NA SALAMA NAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA 2013
 
MWAKA 2012 UMEKUA NI WAMAFANIKIO SANA, MWENYEZI MUNGU AMENIJAALIA MWANZO WA MWAKA KUANZISHA RESTAURANT NYUMBANI TANZANIA KWA MAFANIKIO MAKUBWA KABISA PIA MWISHO WA MWAKA MWENYEZI MUNGU AMENIJAALIA NIMEPATA MTOTO MZURI SANA WA KIKE AMEEN
 
HAIKUA KAZI NDOGO KUANZISHA RESTAURANT NA KUHAKIKISHA WALAJI WOTE WAWE KATIKA MIKONO SALAMA NA WAFURAHIE CHAKULA.
 
KWASASA NIPO MAPUMZIKONI NITAJITAIDI SANA NIWEZE KUWEKA RECIPE ZOOTE KATIKA PICHA PIA NIWEKE RECIPE MPYA MUWEZE FURAHIA MWAKA MPYA.
 
NAIMANI TUTAUANZA MWAKA 2013 KWA FURAHA, AFYA NJEMA NA MAFANIKIO
 
HUKU NI BARIDI SANA  
 
 
NAWATAKIA SIKU NA KAZI NJEMA
 
CHEF ISSA