Monday, December 31, 2012

JIFUNZE KUTENGENZA WALI HUU WA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI KOROSHO NA NYAMA

 
JIFUNZE KUANDAA WALI HUU WA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI NA KOROSHO PIA UNAWEZA KUCHANGANYA NA NYAMA YA NGOMBE, MBUZI, KUKU AU SAMAKI MFANO PRAWNS NA INAPENDEZA SANA SANA
 
MAHITAJI
 
1 kilo ya wali uliokwisha pikwa
1/2 ya mchanganyiko wa mboga majani zozote upendazo
2-3 Spring Onions au majani mabichi ya vitunguu katakata
120 gram korosho
400 gram sawa na 1 kopo la uyoga au fresh
5 gram kitunguu swaumu cha kusagwa
1 Tangawizi mbichi osha na katakata ndogo ndogo sana
4 kijiko kidogo cha chai mafuta ya ufuta
2 kijiko kikubwa cha chakula Soy Sauce
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
500 gram ya nyama au kuku au prawns kama utapenda kuchanganya

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAP CHINI

Muda wa maandalizi : Dakika 15
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji  Watu 2
 
 
Ili kufanya mapishi yangu yawe rahisi mimi huwa natumia mchanganyiko wa mboga majani zilizogandishwa tayari ukienda katika supermaket utazikuta huwa kuka mchanganyiko wa carrot, maharage, njegere na mahindi ya njano. Huwa nachemsha kwa dakika 2 tu katika maji moto sana. kisha toa katika sufuria na uzijchuje ziweke pembeni

 
Unatakiwa kuaanda kila kitu na kiwe karibu na kiaango chako kisha washa moto mkali weka kiaango kipate moto. Kikishapata moto tu, weka mafuta ya ufuta kisha pata moto weka korosho na kaanga ziwe na rangi nzuri ya kahawia toa ziweke pembeni. Kama utatumia nyama ya ngombe, mbuzi, kuku au prawns unaweza zikaanga pamoja na korosho hizi ili ziive pamoja.

 
Katika kiaango hicho hicho weka majani mabichi ya kitungu, tangawizi, na kitunguu swaumu kaanga kwa sekunde 6 hadi 7 utapata harufu safi sana.

 
Kisha ongezea ule mchanganyiko wa mboga ulizozichemsha na kisha ukazichuja kaanga kwa sekunde 5 hadi 6.

 
KIsha ongezea uyoga ulioukata kata. kaanga pia kwa sekunde 10 tu.

 
Sasa ni zamu ya kuongeza soy sauce pia kama ni mpenzi wa pili pili unaweza ongezea  chilli sauce pia unakaanga kwa sekunde 10 hadi 15 tu.

 
Sasa ni zamu ya kuongezea ule wali wako uliopo tayari

 
Koroga vizuri uchanganyike na unaweza kuongezea soya sauce ili kuongeza ladha.

 
Hapa unaongezea korosho pia kama unatumia nyama ongeza pamoja na nyama

 
endelea kuchanganya ichanganyike vizuri

 
Unaweza mwagia kwajuu ya wali wako majani mabichi ya kitunguu au chaives au majani ya giligilani korienda kwa kuongeza ladha na muonekano wa rangi tofauti.
 

Inapendeza sana na chakuala hiki ni kitamua hasa huu ni muonekano baada ya kuivaio
 
Jaribu kuchanganya nyama ya ngombe na ya kuku
 
au changanya nyama ya kuku na prawns katika wali huu na utajifunza kitu muhimu sana
 
au nyama ya mbuzi na ya kuku kwali mchanganyiko huu ni safi sana sana

 
 
CHAKULA HIKI NI KITAMUA SANA NA NI NAFUU SANA KUANDAA WAANDALIE FAMILI WAONE TOFAUTI MWAKA 2013 
 


No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako