Tuesday, January 1, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA MAPISHI HAYA TOKA KWA CHEF ANNA LUSINDE NA CHEF AZIZA JAFARI

 
JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI HII YA MCHANGANYIKO WA MATUNDA KUTOKA KWA CHEF ANNA LUSINDE
 
MAHITAJI
 
1pc parachichi
3pc tunda pasheni
1 pc embe
1 pc karoti
 
FATILIA PICHA NA MAELEZO CHINI JINSI YA KUANDAA
 
 
menya matunda yote pamoja na karoti kama muonekano katika picha

 
Kisha weka katika blenda na usage

 
Saga wastani kwa spidi ya kawaida kisha chuja hakikisha mbegu zisisagike

 
Chuja kwa chujio pole pole

 
Huu ni muonekano wa jusi baada ya kuchujwa

 
Pata juisi hii pamoja na chakula kumbuka mchanganyiko wa matunda hayo unasukari ya kutosha waandalie familia wafurahie
 
 
JIFUNZE KUTENGENEZA VIAZI MCHANGANYIKO WA MBOGA NA SAUSAGE TOKA KWA CHEF AZIZA JAFARY
 
MAHITAJI
 
1 kg viazi ulaya
5 pc sausage
2 pc pili pili hoho
2 pc carrots
2 pc vitunguu maji
4pc kitunguu swaumu kidogo na bizari nyembamba, mafuta kidogo na chumvi basi
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
chemsha viazi kwa maji na chumvi tu usiweke mafuta

 
weka mafuta katika kikaango acha ipate moto kisha weka mchanganyiko wa mboga zote pamoja na sausage endelea kukaanga utapata harufu safi sana

 
Kisha chukua mchanganyiko wa sausage na umwagie juu ya viazi, chef Aziza Jafary alikunywa koka pamoja na chakula hiki safi sana kwa afya ya mlaji.
 
 


No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako