Monday, August 19, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA KUKU WA KUKAANGA PAMOJA NA CHEESE NA SAUCE SAFI

 
KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KUKU HUYU WA KUAANGA PAMOJA NA CHEESE NA UNGA WA MIKATE
 
MAHITAJI
 
240 gram shredded Parmesan cheese
3 vifua vya kuku
480 gram unga wa mkate wa kahawia au bread crumbs
300 gram mtindi uliochanganywa na 100gram vitunguu swaumu vingi, limao, pili pili mbuzi, asali na soya sauce kidogo
1 lita ya mafuta kwa kukaangia
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
 
JINSI YA KUANDAA FATILI APICHA NA MAELEZO HAPO CHINI 
 
 
Jinsi ya kukaausha unga wa mikate unatakiwa kuweka katika oven au kwenye jiko la mkaa na unatakiwa kua makini isiungue iwe ya kahawia tu kish saga katika blenda na  chekecha upate unga safi na laini.

 
Katik picha kushoto ni mchanganyiko wa mtindi ya kitunguu swaumu cha kutosha na kulia ni unga wa mikate kumbuka kuchanganya humo chumvi na pili pili manga.


 
Hatua za maandalizi kwanza chukua kifua cha kuku na kasha kata vipande vya wastani mfano katika picha hapo juu. Chukua vipande hivyo na chovya katika mtindi halafu chovya katika unga wa mkate hakikisha unga wa mkate unapakaza kote safi kabisa.
 

 
Weka mafuta katika kikaango yapate moto wa wastani ikiwa ya moto sana itaungua.

 
Tupia vipande vyakuku katika kikaango na enelea kukaanga

 
Hakikisha unakua makini kugeuza ili isiungulie  hii itatokana na ubora wa kikaango chako au moto ulioweka kwajili ya kukaangia.

 
Hakikisha rangi iwe safi y kahawia ili kukuwako abaki na ladha safi asiungue. Chakula hiki unaweza kula kama mlo kamili nyumbani au unaweza wafungashia watoto wakiwa wanakwenda shule wakala hata ikiwa imepoa badoinakua na ladha safi sana hasa ukila na salad.
 
 

1 comment:

  1. Long time sana kaka. we are anxiously waiting kwa maelezo. I loveee your blog..usipotee sana plsss

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako