Thursday, August 22, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA WALI WA MCHANGANYIKO WA NYAMA YA KUKU NA CHEESE

 
JIFUNZE KUTENGENEZA WALI WA MCHANGANYIKO WA NYAMA YA KUKU NA CHEESE
 
MAHITAJI
4 vifua vyakuku (kata kata vipande vidogo)
 360 gram ya maji
5 gram kitunguu swaumu
1 kijiko kikubwa cha chakula graham masala
1 nyanya ya kopo
500gram sawa na nusu kilo ya mchle
240 gram shredded cheddar cheese
1 kopo la mtindi halisi usio na ladha
1 parachichi au avocado safi lilioiva
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAEEZO HAPOCHINI
 
 
 
Weka kikaango katika jiko kasha pata moto wa kutosha mwagia vipande vya kifua cha kuku na kasha weka kitunguu swaumu, chumvi, pili pili manga na kama unamajani ya giligilani au parsley mwagia kuongeza ladha zaidi ila sio lazima na mafuta ya kukaangia.

 
Endelea geuza geuza isishike chini na kuungulia ndani ya dakika 5 tu itakua imeshaiva kabisa

 
Kisha mimina maji kwenye kikaango ay sufuria, weka graham masala kasha weka nyanya ya kopo na mwisho miminamchele na koroga vizuri funikia chakula kiendelee kuiva.

 
Hakikisha umefunika vizuri chakula kiendelee kuiva pole pole nivizuri kabla maji hayajakauka ukaonja chumvi na kuongezea

 
Hapa maji yote yameshakauka na wali wetu na mchanganyiko wa kuku umeshaiva safi kabisa

 
Wali bado ukiwa wamoto mwagia cheese kwa juu itayeyuka mara moja na kutengeneza mvuto kwa macho na harufu safi sana na ladha ya kipekee mdomoni

 
Ukichota wali kwa chini huu ndio muonekano wake

 
 Baada ya kupakua unaweza mwagia juu mtindi pamoja na parachichi na ukaendelea kufaidi zaidi na family yako.
 


2 comments:

  1. Nimependa hicho chakula Chef hadi mate yani mate yanitoka, tupia maelezo yake nasi tujue kujipikilisha

    ReplyDelete
  2. graham masala ndio garam masala?ama ni vitu viwili tofauti ?

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako