Sunday, October 27, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA KEKI HII YENYE MCHAGANYIKO WA MATUNDA

RECIPE SAFI KABISA YA KEKI HII YA TUNDA AINA YA CHUNGWA 
MAHITAJI
420 gram unga wa ngano
240 gram Sukari
2 kijiko kidogo cha chai Baking Powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
120 gram siagi au Vegetable Oil
240 gram juice ya chungwa
1 chungwa kwaruza ganda lake
2 pc ute mweupe wa yai
2 kijiko kikubwa cha chakula Icing sugar
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Chukua bakuli safi kavu kisha weka unga wa ngano, sukari, baking powder pamoja na chumvi



Kisha weka juisi ya machungwa pamoja na vegetable oil au siagi itategemea unachopenda au aina ya mafuta uliyonayo tumia mchapo piga mpaka ilainike.


Chukua bakuli nyingine safi na kavu weka ute mweupe wa yai kasha piga mpaka ilainike na upate povu kama muonekano katika picha.


Kisha chukua ule mchanganyiko wa chungwa mwagia pole pole kwenye povu la ute mweupe na tumia mwiko kukoroga pole pole ichanganyike fanya hivyo mpaka mchanganyiko wote umalizike.


Paka mafuta mazito pembeni mwa chombo cha kuokea keki yako na kasha mwagia mchanganyiko wako wa keki kwenye chombo cha kuokea.


Bake kwa muda wa saa 1 kwenye oven ambayo tayari inamoto wa wastani, kama huna uhakika tumia toothpick choma kati kati ya keki ikitoka kavu basi kekei imeiva na ikitoka na uji basi bado haijaiva ongeza muda.


Ikishaiva toa nje ya chombo cha kuokea kwadakika 10, kisha mwagia kwa juu icing sugar



MUONEKANO MZURI WA KEKI FURAHI NA FAMILIA


1 comment:

  1. CHEF
    apa ina mana umekamulia juice ya machungwa au umesugua ganda la chungwa katika ngano?

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako