Friday, October 25, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI CHA MCHANGANYIKO WANDIZI MBIVU MGANDO NA CHOCOLATE

KWA RECIPE NA UPDATE ZA MAPISHI CLICK LIKE active chef kwenye facebook.com
 KITAFUNWA HIKI CHA MCHANGANYIKO WA NDIZI MBIVU MGANDO NA CHOCOLATE NA MCHANGANYIKO WA KARANGA NI RAHISI SANA KUANDAA
 
MAHITAJI
 
 3 pc ndizi mbivu
240 gram Semi-Sweet Chocolate Chips ( Vipande vya chocolate)
2 Kijiko kikubwa chachakula siagi iliyoyeyushwa
3 Kijiko kikubwa chachakula mchanganyiko wa karanga aina yeyote utakayokuanayo mfano (Almonds, Pistachios, Pecans, Hazelnuts, Walnuts, karang au korosho), weka zote au chagua uzipendazo tu.

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPA CHINI
Muda wa maandalizi : Dakika 15
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 4 vipande 15 hadi 20

 
 
Kata kata ndizi katika vipande vidogo vidogo mfano kama muonekano kwenye picha.
 
 
Chukua alluminium foil kisha ifunike katika sahani pan au tray vizuri na upande juu yake vipande vya ndizi mbivu vilivyokwisha katwa.
 
 
Kisha chukua cocktail forks au uma ya plastic zinapatiana katika supermarket pia unaweza weka chochote kitakachokua rahisi kushika . Kisha zigandishe kwenye friza kwa masaa 2 au mpaka zitakapo ganda tu toa.
 
 

Wakati unaweka katika friza muda huo huo anza kukaanga pamoja karanga za mchanganyiko ulionao .
 
 
Zikaange tu kwa wastani zinukie harufu safi kisha zitoe na uzikate kate katika vipande vidogo na ziweke pembeni  zipoe.
 
 
Baada ya ndizi kuganda sasa Chukua sufuria dogo weka maji robo kisha chukua akuli ya kioo kubwa na uweke juu yake acha maji yachemke kisha weka mchanganyiko wa siagi na chocolate chips ndani ya bakukuli ya kioo juu ya sufuria. Kumbuka kuendelea kukoroga mpaka siagi yote iyeyuke na chocolate yote iyeyuke na kua laini safi kabisa.

Pia unaweza tumia njia mbadala ambayo ni microwave lakini unatakiwa uwe mzoefu sana kwani unaweza zidisha muda wa kuyeyusha ikawa mbaya.
 
 
Toa ndizi zilizoganda katika friza, chovya kwenye mchanganyiko wa siagi na chocolate.
 
 
Kisha toa unaweza mwagia mchanganyiko wa karanga kwa juu yake au unaweza kuroll
 
 
KIsha unairudisha kwenye ile sahani ya badidi mpaka ikauke vizuri.
 
 
Kumbuka pia unaweza tumia chocolate hata zapaketi kama utakosa chocolate chips. Endapo itakua imebaki chocolate sauce unaweza itunza kwa kufunika na kuweka jikoni katika kabati kwa muda wa mwezi mmoja na isiharibike na sio kwenye  fridge. Waandalei familia watafurahia au tengeneza kwa biashara.
 

No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako