Friday, October 18, 2013

NAMSHUKURU ALLAH NIMEPATA TUZO NYINGINE YA HESHIMA YA MAFANIKIO KATIKA MAPISHI YA KIAFRICA

 
NAFURAHI SANA KUWAFAHAMISHA NDUGU ZANGU KUA NIMETUNUKIWA SARAFU YA HESHIMA YA KUTAMBUA MCHANGO WANGU JUU YA MAFUNZO YA CHAKULA KWA LUGHA YA KISWAHILI PAMOJA NA KUENZI MAPISHI YA KIAFRICA.
 
NILIPATA TUZO HII TOKA KATIKA MASHINDANO YA KUMTAFUTA CHEF BORA WA MWAKA 2014 KWENYE NGAZI YA NUSU FAINALI KATIKA MJI WA LINGKOPING NA FAINALI ITAFANYIKA MJINI STOCKHOLM TAREHE 7/2/2014 UKUMBI WA WATERFRONT.
 
TUZO HII  NILIPATIWA NA ALIEKUA JAJI MKUU WA MASHINDANO HAYO SIKU HIYO Chef Markus Aujalay PIA ALIFANIKIWA KUWACHEF BORA WA SWEDEN MWAKA 2004 PIA NI CELEBRITY Chef ANAEMILIKI RESTAURANT NA AKIONGOZA KIPINDI MAARUFU CHA MAPISHI KATIKA TV SWEDEN MASTERCHEF.
 
 
Safari ilikua ni ya masaa 3 kutoka mji ninaoishi mpaka mji uliokua mashindano yanafanyika namshukuru Allah nilikwenda na kurudi salama amiin.

 
Katika picha hapo juu Chef Issa nikiendelea kutathmini Chefs wakiendelea kupambana
 
 
Huyu ndio alikua Jaji mkuu wa mashindano hayo ya nusu fainali siku hiyo anaitwa Chef Markus Aujalay Chef bora wa mwaka 2004 wa Sweden.

 
Ilitengwa sehemu maalumu ya sisi waalikwa kutathmini vyakula baada ya kupangwa katika sahani na majaji kuonja na kutoa alam a ushindi.

 
Chef waalikwa wakiendelea kupata taswira za vyakula toka kwa chef washindani

 
Walijitaidi sana kwakweli kuonyesha ubora wao, safari bado ni ndefu na mashindano ni magumu sana

 
Taswira ya ukumbi toka kwa juu

 
Taswira ya meza kuu toka kwa juu

 
Taswira hii inakuhakikishia kua chef Issa alikua mweusi pekee katika mashindano haya hivyo ilikua heshima kubwa sana kwangu na kwa taifa langu kutambulika kwa uwezo wangu na mchango wangu na utaifa wangu mhhh Viva Tanzania.

 
Utaratibu ulikua ukimaliza kuandaa chakula unaenda mbele ya kamera na kuanza kujieleza kwa majaji na watazamaji waliokua wanaangalia live aina ya chakula ulichotengeneza na mbinu ulizotumia
 
 
Upande wa pili ilikua ni maonyesho y vyakula ya chef waliopo huoni wenye umri wa kuanzia miaka 13 mpaka 16. Pia makampuni maarufu y chakula na yanayojihusisha na vyombo vya jikoni kama Electrolux, Santamaria, Arla na mabingwa wa visu duniani Global pia walikuwepo kutangaza bidhaa zao.

 
 ALHAMDULILAH HII NDIO TUZO YA HESHIMA NLIOTUNUKIWA.

 


14 comments:

  1. Hongera sana chef Issa...Lucy Mbuya

    ReplyDelete
  2. hongera sana chef issa. mungu azidi kukubariki. tunakupenda na kukuombea mafanikio mema

    ReplyDelete
  3. Hongera sana ndugu yetu kwa medali ya heshima uliyotunukiwa!!
    mie sina medali lakini nilishakutunuku heshima ya mapishi siku nyingi--Jua hata nyumbani unawatu wanakuheshimu kwa mchango wako---huwezi jua umeokoa ndoa ngapi ambazo zingeweza kuwa matatani kwa suala la weredi wa mapishi!!
    Ubarikiwe na uzidi kung'ara!!

    ReplyDelete
  4. Hongera Sana, kwa kurudisha heshima nyumbani. Stella

    ReplyDelete
  5. i remember to meet this guy in Mtwara ....Maisha Club, i really enjoyed the food. Hongera sana brother and all the best. RAY

    ReplyDelete
  6. Hongera sana, kwa kweli umeonyesha uwezo mkubwa juu ya machef wengine na hii ni sifa kubwa kwako na familia yako pamoja na Taifa zima la Tanzania.

    Nakutakia kila la here Mungu awe pamoja nawe na ukawe mshindi namba moja. Amen

    Jacqueline Ayoub

    ReplyDelete
  7. HONGERA SANA KAKA YETU KWA KUPATA HESHIMA KUBWA HUKO ULAYA HATA SISI WATANZANIA UMEONYESHA KWAMBA TUNAWEZA
    MUNGU AKUBARIKI KAKA ISSA KIPANDE. DADA YAKO ANNA

    ReplyDelete
  8. hongera sanaa chief mimi nimefurahi sana kuona umeitangaza tanzania kwa moyo wako wote.ila tunaomba utuandalie mashindano ya master chief junior mapish ya watoto wenzetu kenya wameanza siku nyingi sisi bado maana nimehangaika kutafuta mahali pakumpeleka mtoto wangu ajifunze mapishi sijui hata nianzie wapi.

    ReplyDelete
  9. Hongera kaka ......Rehema Kayumbo

    ReplyDelete
  10. Hongera sana kaka ..... Rehema wa Holland

    ReplyDelete
  11. That's wonderfull, hongera sana kaka you deserve the best na umeiwakilisha vizuri Tanzania! Proudly Tanzanian. By chef Kilawe.

    ReplyDelete
  12. hongera sana kaka Issa,Mungu aendelee kukuongezea maujuzi
    nimejifunza mengi kutoka kwako

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako