Thursday, December 26, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI CHA KARANGA NA CHOCOLATE


 RECIPE SAFI KABISA YA KITAFUNWA HIKI CHA KARANGA NA CHOCOLATE
 
MAHITAJI
360 gram peanut butter
1 kg high quality chocolate chips, milk chocolate nzuri kwa family

 360 gram sukari ya unga ( icing sugar)
 6 kijiko kikubwa cha chakula siagi iliyoyeyushwa
Cooking Spray
Mini Cupcake Papers
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

 
Haya ni maandalizi ya vitu vyote unavyohitaji kwakutengeneza kitafunwa hiki
 

 
Yeyusha siagi kwenye microwave. Kisha chukua peanut butter weka kwenye bakuli safi na kisha changanya na icing sugar pamoja na vijiko 4 vya siagi liyoyeyushwa. ukiona bado ni kavu sana ongeza vijiko viwili vilivyobakia. endelea kukoroaga upate mchanganyiko laini.
 

 
Yeyusha chocolate kwenye microwavehakikisha unaikoroga koroga mara kwa mara mpaka itakapo yeyuka nikiwa na maana weka dakika 1 toa koroga kisha rudihs kwenye microwave kwa dakika 1 toa koroga mpaka iyeyuke na kua laini safi kabisa.

 
Panga hizo cupcake papers kwenye tray ya kuokea baking sheet paka mafut ya siagi hizo cupcake zote mimi huw anatumia spray special. Chukua chocolate iliyoyeyuka kisha mimina kijiko kimoja tu kwenye cupcake papers, hakikisha imeenea vizuri kwa chini. tumia kidole chako kuisambaza vizuri na uhakikishe imeshika saf kabisa. fanya hivyo kwa cupcake zote na hakikisha mchanganyiko wa chocolate umebaki pembeni kwajili ya matumizi mengine.
 
 
Baada ya kumaliza oezi hili, chukua trayweka kwenye friji poe kwa dakika 5 hadi 10
 

 
baada y dakika 5 hadi kumi utapata muonekano huu na chocolate itakua imeganda

 
Chukua piping bag au mfuko wa nailoni na kisha tumia glasi kwa kukusaidia kumiminia mchanganyiko wao wa peanut butter kwa urahisi tumbukiza mfuko wako ndni ya glasi na kisha anza kumimina mchanganyiko wa peanut butter


 
kisha anza ku Pipe au unaweza kutumia kijiko kuweka mchanganyiko wa peanut butter kwenye chocolate cupszilizotoka katika friji.Tumia piping bag ni nafuu na haraka zaidi!

 
Huu ndio muonekano baada ya kuweka peanut butter katika chocolate cupcakes
 
 
Tumbukiza kijiko chako kwenye maji na kisha kandamiza moja baada ya nyingine kutengeneza umbo zuri. Chukua chocolate iliyobakia iliyokwisha yeyushwa na mimina juu ya peanut butter na urudishie tray kwenye friji kwa dakika 30 iweze kuset completely. Recipe nzima inaweza kutoa vipande 55 mini peanut butter cups.

 
Baada a dakika 30 itakua imeset safi kabisa na tayari kuliwa
 

 
Ukitoa kwenye cup cakes utapata muonekano huu safi saaafi sanaaaaa
 

 
Ukiuma na kuikata katikati utapata muonekano huu na ladha safi sana ya hali ya juu mchanganyiko wa peanut butter na chocolate.


Unaweza ongezea urembo juu yake............….lakini......….from the bottom of my heart….I have to say….these are D E L I C I O U S ! ! ! !  The peanut butter filling is soooooooo creamy and each splendid little bite is the perfect ratio of chocolate to peanut butter.
Hopefully that wasn’t too hard watengenezee watoto nyumbani na watu wazima watafurahia candy hii ya aina yake.

ENJOY!

 

7 comments:

  1. katika kipengere hiki naomba unisaidie kwa kuorodhesha mahitaji yake hapo chini maana nimekuwa nafuatilia sana mafunzo haya lakini hili limenipita pembeni kwa kushindwa kuelewa mahitaji.

    ReplyDelete
  2. Maelezo ya mahitaji yapo wapi, picha pekee haitoshi

    ReplyDelete
  3. mbona maelezo yake yamechelewa sana?

    ReplyDelete
  4. mbona maelezo yake yamechelewa ninahamu sana ya kujaribu kupika

    ReplyDelete
  5. Yani kwa kweli hii kitu inaniboaaaa sijui nikwambieje. Picha then kaa tayari kwa maelezo halafu husemi kitu. Mbona mwanzo hukuwa hivi? Huku nimejifunza mambo mengi ila sasa hivi kwakweli hakina kitu. Hii iko kiroho safi tu, yani naweza kaa miezi sasa sijaingia humu tofauti na mwanzo ilikuwa daily

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako