Wednesday, October 15, 2014

JIFUNZE KUPIKA KITUMBUA CHENYE MCHANGANYIKO WA UNGA WA NGANO NA UNGA WA MCHELE

 RECIPE SAFI KABISA YA KUPIKA KITAFUNWA AINA YA KITUMBUA KWA MCHANGANYIKO WA UNGA WA MCHELE NA UNGA WA NGANO OOOHH LADHA SAFI SANAA
 
MAHITAJI
250 gram unga wa ngano
120 gram unga wa mchele
1kijiko kidogo cha chai hiliki ya unga au unaweza saga mbegu ikawa chenga chenga
120 gram sukari
120 gram maji ya vugu vugu
nusu kijiko kidogo cha chai amira ya chenga
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
Chukua maji ya vugu vugu changanya na amira ya chenga, sukari pamoja na hiliki.

 
Chukua unga wa ngano na unga wa mchele changanya pamoja

 
Chukua mchanganyiko wa maji mimina kwenye mchanganyiko wa unga wa ngano na mchele na kisha tumia mwiko kukoroga pole pole mapaka ichanganyike vizuri. 

 
Kama mchanganyiko wako ni mwepesi sana basi unaweza tumia mayai au ukaongeza maji au maziwa kiasi hakikisha mchanganyiko huu usiwe mwepesi kabisa na usiwe mzito sana ubora uwe kama unavyoona kwenye picha hapo juu.

 
Chukua kikaango cha vitumbua kisha weka mafuta ya kupikia kijiko kimoja kidogo cha chai.
 

 
Mafuta yakisha pata moto mimina mchanganyiko wako wa unga wa mchele kwenye kikaango.
 

 
Ukishaona rangi ya kahawa kwa chini basi geuza upande wawili na weka mafuta tena. mpatie mlaji chakual kikiwa cha moto atafurahi sana. 

 
 
HUU NI MUONEKANO SAFI KABIS AWA KITUMBUA HIKI CHENYE MCHANGANYIKO WA UNGA WA AINA MBILI SAFI SANA KWA KITAFUNWA CHA NYUMBANI NA RESTAURANT PIA. 
 


No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako