Wednesday, March 24, 2010

JINSI YA KUPIKA MACARONI, PEENE PASTA AU SPAGHETI

CHAKULA HIKI NI KIZURI SANA NA NIRAHISI SANA KUPIKA HUTUMIA MUDA KIDOGO SANA WA MAANDALIZI NA GHARAMA NAFUU. SIO WATU WAZIMA TU HATA WATOTO HUPENDA SANA KULA CHAKULA KITAMU NA CHENYE MUONEKANO WA TOFAUTI UNAWEZA PIKA KWA MTINDO HUU AINA YEYOTE ILE YA PASTA.




Hii ni white sauce mahitaji na jinsi ya kutengeneza angalia chini mwisho wa picha.


Hii ni penne pasta ichemshe katika maji yaliyo chemka weka chumvi na mafuta ya kupikia kidogo yasaidie zisishikane wakati unachemsha pia kumbuka kuzikorogo koroga wakati unachemsha.


Ukisha chemsha kwa dakika 7 hadi 10 zitoe katika maji zisiendelee kuiva lazima uwe umeshaanda white sauce yako safi kabisa ziweke kwenye sahani



Kaanga kitunguu kasi kilainike vizuri kumbuka kuweka na chumvi kidogo



Kisha mwagia juu ya pasta hiyo white sauce mhhhh inapendeza safi sana


Kisha juu yake weka vitunguu vya kukaanga mhhh inaharufiu safi sana na ni tamu kweli kweli unaweza fanya mchanganyiko wa mboga kama karoti na pilipili hoho na kitunguu au ikabaki kitunguu peke yake yote sawa.




MAHITAJI YA KUTENGENEZA WHITE SAUCE

150 gram Unga wa ngano
200gram Blue band au butter
1 lita maziwa
1/4 kijiko cha chai kungu manga
2 mbegu za karafuu kavu
1 kikubwa kitunguu chop chop

JINSI YA KUTENGENEZA
weka blue band au butter katika kikaango au sufuria acha iyeyuke kiasi kisha weka kitunguu chop chop kaanga kilainike.



Kisha weka unga wa ngano koroga uchanganyike vizuri na mafuta kisha chukua mchapo wa chuma (Whisker) ili utumie kukorogea wakati unaweka maziwa.



Anza kumimina pole pole mziwa huku ukikoroga na mchapo mapaka upate rojo zito kabisa endelea kumimina maziwa mapaka upate rojo laini kabisa kama maziwa yamekuishia basi ongezea hata maji kiasi. kisha weka kungu manga na karafuu kuongeza ladha safi kabisa.



7 comments:

  1. issa, mbona hakuna maelezo....na miss uondo..Da Lucy

    ReplyDelete
  2. maelezo ndugu ni muhimu.

    ReplyDelete
  3. sijaelewa bora weka maelezo

    ReplyDelete
  4. Kaka kama vile ulikuwa kwenye mawazo yangu nilikuwa nataka kukuomba utuandikie mapishi ya pasta, asante sana tunasubiri maelezo. mimi ni mpenzi sana wa pasta

    ReplyDelete
  5. Asante kaka.
    Yani nimeletewa makaroni makubwaaaa kama yai, nilikuwa nawaza niyapike vipi.
    Nikawaza labda nipike na jumbo prowns, asante kaka sasa nimepata njia.
    Nitapika kama hivi na sauce yake, then nitakroast prawns au nitapika ile fillet ya kuku uliyotufundisha kwa wali.
    Najua mwanangu atafurahia.


    disminder.

    ReplyDelete
  6. Asante sana Chef, nimepika huu mlo wa paste na umetoka bomba,Thank you again kwa ufundi.

    Liz

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako