Monday, March 1, 2010

MAFUNZO YA KUPANGA CHAKULA KATIKA SAHANI KIPENDEZE

KAMA NI MAMA NYUMBANI KUMBUKA KUA MUONEKANO WA CHAKULA PIA UNASAIDIA SANA KUHAMASISHA WALAJI AIDHA MUMEO AU MTOTO HAPENDI KULA UNAWEZA MSHAWISHI KWA KUNAKSHI CHAKULA CHAKO NA KIKAMVUTIA USIAMINI FATA MAFUNZO HAYA UTAFUARIA KWA KUONA MABADILIKO YA ULAJI KWENYE FAMILIA YAKO SIO LAZIMA KILA SIKU UPAKUE KWENYE MAHOT POT WASHANGAZE SIKU MOJA MOJA KWA KUPAMBA SAHANI.



Pika pilau yako safi  pakua kwa kutumia chombo chochote chenye umbo zuri hata kikombe kisha chukua jani la salad ( lettuce) weka pembeni kidogo kisha juu yake weka kachumbali safi kisha pakua nyama iliyopikwa katika chuzi zito pembeni je umeona utofauti? inapendeza?



Chukua wali iliokisha iva, changanya uviringishe upate umbo la duara kisha lizungushe duara hilo la wali katika unga wa ngano kisha dumbukiza katika mayai yaliyopigwa baada ya hapo weka taika unga wa mikate uliosagwa.

Ukimaliza tumbukiza mduara huo ndani ya mafuta yenye moto kaanga mapaka upate rangi ya kahawia kisha chukua mchicha uliochemshwa zungusha upate mviringo pia.

Kisha chukua sahani weka chatney ya matunda mchanganyiko au a BBQ sosi au teriyaki sauce kwa umbo la mduara pia katika sahani yako.

juu yake weka ule mduara wa mchicha kisha juu yake pia weka ule mduara wa wali kisha muhudumie mlaji ikiwa yamoto kama starter au kitafunwa



KWA WALE WALA MBOGA TU BILA NYAMA HAPA NDIO MAHALA PAO HASA!

Chukua mboga za aina nne pilipili hoho, nyanya, kitunguu na bilinganya kata mkato kama unavyoona kwenye picha kisha weka kwenye jiko la kuchomea griller au kikaango chenye mafuta kiasi na moto wa kutosha kuchoma



Jinsi ya kupanga katika sahani upande wa mboga chini kabisa weka bilinganya, juu yake weka pilipili hoho, juu kabisa weka nyanya na pembeni yake weka kitunguu. wali na mchuzi upo pembei pia na mchuzi upo katika bakuli ili kuongeza utanashati katika sahani ukimwaga mchuzi katika sahani haitapendeza.

Unaweza kula kwa wali au ugali hata na nyama pia kumbuka mboga zako zisiive sana ziive nusu ilia kulinda ubora wake na ziwe na manufaa katika mwili wako.



Huu ni wali na njegere ya nazi kuna vyombo maalumu kwajili ya kutengenezea umbo hilo la wali ukienda katika maduka ya vyombo ya kupikia au vyombo vya jikoni uliza rice mould utapata inashimo katikati weka wali wako safi kisha ukandamize vizuri ili ukiweka katka sahani iweze kukaa vizuri kisha weka njegere katika hilo shimo.

Kisha weka nyanya iliyokaushwa kwa jua na jani la parsley kama pambo muonekano unavutia kabisa kwa mlaji

HILI NI SOMO MAALUMU LITAKALO ENDELEA KILA SIKU MTAPATA VYAKULA VYA AINA TOFAUTI MFAHAMU JINSI YA KUPAMBA VYAKULA KATIKA SAHANI SIO LAZIMA UKITAKA KUFURAHIA CHAKULA MAPAKA UENDE HOTELINI WAKATI UNAWEZA FANYA MAAJABU NYUMBANI RAFIKI NA FAMILIA WAKAFURAHIA KUPITA MAELEZO NAWATAKIA MAFUNZO MEMA ENDELEENI KUSHIRIKIANA CHEERS!!!!



2 comments:

  1. chef Issa nashindwa hata niseme nini maana haya ni kama maajabu ila kwa mafunzo haya hakuna kinachoshindikana...natamani niache field yangu ya kazi niishike field hii..kwa kweli inahamasidha sana...uzidi kubarikiwa.

    ReplyDelete
  2. Nimekuheshimu kaka, unaweza kuonyesha Nama ya kuserve ugali attractively? Waikato mowing one hupenda kuserve ugali kwa rafiki wasio waswahili lakini Sijui Kuandaa kwa Namna ya kupendeza.

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako