SALAD HIZI HULIWA KABLA YA MLO KAMILI KAMA KITANGULIZI
Chemsha spinach au mchicha uive nusu tu kisha weka pembeni upoe
Kata vitunguu vidogo kwa urefu
Changanya mafuta ya maindi ili isaide ukiweka katika friji salad yako isigande
weka chumvi kulingana na ladha yako
weka maji ya limao au vinega ksiah changanya pamoja tayari kwa kula panga kama inavyoo onekana katika
piachasalad hii ni asfi na salama kwa afya yako
SALD YA VIAZI NA MICHIRIZI YA SOSEJI ZA NG'OMBE
Upande wa kulia mwanzo ni michirizi ya soseji, jani la saladi na mwisho ni mchanganyiko wa viazi vilivyochemshwa vikaiva nusu vimechanganya na mayonaise kidogo na pili pili hoho na kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo.
Kwanza weka jani lako la salad kisha weka mchanganyiko wa viazi juu ya jani la salad hakikisha inakaa katika umbo la mlima ili kuvutia zaidi
Mwisho kabisa weka vipande vya nyanya freshi na kati kati weka michirizi ya soseji muhudumie mlaji ikiwa ya baridi
KUMBUKA KUWEKA MAYONAISE KIDOGO SANA KWA AFYA YAKO
asante sana chef,maana unatufanya waume zetu wawahi kurudi kwa msosi wa nyumbani...hahaha ila nilikua na swali na hizi salad ni muda gani muafaka wa kuliwa?ni kabla ama baada ya mlo mkuu?ama ni wakati wowote?
ReplyDeleteJulia.
Jinsi ninavyopenda mapishi? Sijui nimepatwa na nini? Asante kaka, majibu utapata.
ReplyDeletedisminder.
leo ni mara yangu ya kwanza kufungua blog yako ni nzuri sana na inaelimisha kupita kiasi. Naomba unifundishe aina mbalimbali za utengenezaji wa salads za kula baada ya mlo au pamoja na mlo
ReplyDeletekaaazi kwelikweli,tushindwe wenyewe,maana mwalimu ameamua kutufundisha bure bila gharama yoyote,keep it up chef maana kwa jinsi navyopenda kupika..............
ReplyDeleteJamani mimi ninachokuombea ni Mungu akuzidishie zaidi na zaidi uwe na moyo huo huo wa kutoa mafunzo bila malipo. Kwa upande wangu nimefaidika sana.
ReplyDeleteHallow chef nimefurahi sana kupata mapishi kama haya nakushukuru sana na mungu akubariki sana Mungu akulinde na magonjwa.
ReplyDeleteSarah, Arusha
asante sana chef mimi napenda sana kupika nimefurahi sana na mapishi yako Mungu akulinde akuzidishie pale palipopungua asante
ReplyDelete