Wednesday, August 25, 2010

WAJUA KUTENGENEZA SWISS ROLLS LADHA TOFAUTI ????


MAHITAJI
3 Mayai

240 gram unga wa ngano ( Self raising flour)

120 gram castor sugar

1 Kijiko kikubwa cha chakula castor sugar

1 Kijiko kikubwa cha chakula maji ya vugu vugu

120 gram  apricot jam, au trawberry jam au chocolate au custard 

1 Kijiko kikubwa cha chakula icing sugar

Siagi kidogo iliyoyeyushwa kwajili ya kubrushia

JINSI YA KUANDAA

Pasha oven kwa moto 200ยบ C. Paka siagi iliyoyeyushwa kwenye chombo utakachotumia kuokea keki yako (flat baking tray) Kisha weka karatasi isiyopitisha mafuta kama huna basi tumia karatasi nyeupe isiyo na mistari kumbuka nayo kuipaka siagi vizuri na uiweke katika chombo utakachotumia kuokea.

Chukua mayai pamoja na sukari tumia mashine ya kuchanganyia changaya mpaka mchanganyiko wako uwe laini na utoe mapovu kabisa.

Baada ya mchanganyiko huo kua laini safi na mapovu chukua unga na anza kuchanganya safi kwa kutumia kijiko fatilia picha hapo chini.

Kisha mimina mchanganyiko wako safi kabisa na usambaze vizuri uenee sehemu zote kwa usawa.
Choma kwa dakika 8 - 10 mpaka sponge iwe imeiva safi 

Kisha chukua karatasi mpya isiyopitisha mafuta (baking paper) kisha ilaze juu ya meza safi. Nyunyiza juu ya  baking paper kijiko kimoja cha castor sugar. Pole pole itoe cake yako kwenye chombo ulichookea na ihamishie kwenye baking paper mpya kisha nyunyiza tena castor sugar.

Hatua inayo fata ni kuweka mchanganyiko wa ladha yeyote ile unayopenda na ndio itakayo beba jina zima la chakula chako hichi mfano ukiweka jam itaitwa jam swiss roll na ukiweka chocolate itaitwa chocolate swiss roll au ukiweka custad itaitwa custad swiss roll.

Baada ya kuweka ladha ya chochote ukipendacho wewe hakikisha tendo hili unafanya haraka haraka kabla cake yako haijapoa itakua vigumu kuikunja, anza na pindo dogo dogo mpka uikunje yote iwe duara kwa kuzungusha na kumbuka karatasi lazima ibaki nje. Acha na karatasi mpaka ipoe ndani ya freezer ili ishikane kabisa ikisha poa kabisa a kushikana toa karatasi.

Unaweza nyunyizia kwa juu icing sugar. Kwakutumia kisu kikali kata slice saafi kabisa tayari kwa mlaji kufaidi.



Chukua mayai na sukari weka kwenye bakuli



Tumia machine ya mkono kwa kuchanyania mpaka iwe safi na laini



Mayai na sukari vimeanza kuchanganyika vizuri na rangi ya kiini cha yai inabadilika toka kwenye njano kali na kua njano iliyofifia



Hapa rangi inazidi kufifia na mchanganyiko unachanganyika safi kabisa



Hapa imechanganyika bado kidogo tu itakua tayari



Sasahapa ipo safi na imekua laini na imeweka mapovu imeshapanda na kuongezeka



Weka unga ndani ya mayai haya na unaze kuchanganya pole pole



Changanya kwakutumia kijiko cha chuma au mwiko wa mbao poe pole ili mayai yenye sukari na unga viweze kuchanganyika safi bila kuweka mabonge bonge



Pole pole endelea kuchanganya



Mpaka mchanganyiko wako sasa unakua laini na umechanganyika safi kisha mimina kwenye chombo cha kuokea na choma kwa dakika 8 - 10 kisha toa



Hapa imeiva safi na inaonekana na rangi nzuri ya kahawia itoe haraka kabla haijapoa na weka kwenye karatasi mpya ya kuokea ukiwa umesha nyunyiza sukari yako nyeupe ya chenga



Sasa hapa ipo safi unaweza kuweka mchanganyiko wa ladha yeyote uipendayo na uanze kukunja



Kama nilivyoelekeza awali kua kunja kwa kuanzia kunjo dogo mpaka unamaliza mduara wote hakikisha karatasi inabaki nje kama picha hii inavyoonyesha ili swiss roll yako ikamilike



Kumbuka usikunje kama picha hii inavyoonyesha karatasi ikabaki ndani ule mchanganyiko wako wa ladha ulioweka ndani utashikana na karatasi na hautaweza kuitoa ukiitoa inamana utakua umesha ikunjua swiss roll yako na haitaweza kurudi katika umbo lake tena na utakua umepoteza maana halisi. Na mlaji itabidi ale na karatasi hahahaaaaaaaaaa!



Ukifata maelekezo vizuri swiss roll yako baada ya kupoa vizuri kwenye freezer na ukatoa karatasi ya juu itakua na muonekano huu na hiii ni swiss roll yenye mchanganyiko wa srawberry na custard.



Tumia kisu kikali kata slice safi wapatie familia wafurahie baada ya chakula au chai ya jioni saa 10



Hii ni swiss roll ya ladha ya machungwa na mchanganyiko wa karanga kati kati.



Huu ni muonekano wa chocolate swiss roll

SIO NGUMU KUTENGENEZA NI UFATILIAJI MZURI TU WA JINSI YA KUANDAA HAICHUKUA MUDA MREFU KUANZIA KUANDAA MPAKA KUPIKA NA KUIVA NI DAKIKA 45 TU IFURAHISHE FAMILIA YAKO KWA UBUNIFU.

ENJOY


 

JIFUNZE KUTENGENEZA FRUIT TRIFLE

SAFI SANA KWA FAMILIA YAKO, INALIWA BAADA YA MLO KAMILI NI NZURI SANA NA RAHISI KUTENGENEZA

MAHITAJI

500 gram Mchanganyiko wa matunda angalau anina nne au tatu
500 gram fresh cream
1 box na Biscuit za aina tofauti aidha nyembemba ndefu au za mduara
1 bakuli la kioo linapendeza zaidi
300 gram Keki
200 gram Caster sugar


JINSI YA KUANDAA

Piga kwa kutumia mchapo au mashine fresh cream yako na sukari  mpaka iwe nzito kabisa kam povu  kisha iweke kweny friji ipoe zaidi na kua rahisi kuitumia

Kata matunda yako yeyote yale uliyonayo nusu ili kua na muonekano safi unapo yapamba kwenye bakuli lako.
  


Trifle hii ni ya mchanganyiko wa matunda menya na katakata vipande vidogo vya nanasi, water melon, chungwa na papai unaweza ongezea na apple.

Chini kabisa ya bakuli weka vipande vya keki aina yeyote ile kutokana na ladha unayopenda wewe kisha juu yake panga matunda ukimaliza mwagia kwa juu ile fresh cream uliyokwisha ipiga  sambaza vizuri isibaki nafasi ifunike kabisa matunda yako.

Baada ya hapo weka tena matunda na mwisho mwagia tena fresh cream na usambaze kama mwanzo juu kabisa pamba vizuri kwa biscuit na matunda kama picha inavyoonyesha.

Hapa inakua tayari kwa kuliwa iweke kwenye friji ipate ubaridi safi kisha wapatie walaji wafaidi.



PEACH AND RASPBERRY TRIFLE

MAHITAJI

1 Peach ya kopo
200 gram Raspberry
200 gram keki
200 gram Fresh cream
100 gram Sukari

JINSI YA KUANDAA

Kama mwanzo piga fresh cream na sukari kisha anga vipande vya keki na kisha weka matunda aina ya peach  na juu yake weka cream. Rudia tena zoezi hilo na mwisho weka mduara wa peach na kati kati weka raspberry na ju u yake weka fresh cream weka kwenye friji ipoe na wapatie familia wafurahie.








 STRAWBERY TRIFLE
( hii safi sana kwa wano ogopa kupata vitambi au kuongezeka uzito lakini wanapenda kula vizuri)

MAHITAJI

5 gram Cinamon
1 Chungwa lililoiva safi
20 gram sukari
5 gram Vanilla essence
 50 gram keki
5 pc Strawberry fresh
100 gram Fat free cream

JINSI YA KUANDAA

Changanya vanilla, juisi ya chungwa, fat free cream, sukari na cinamon ya unga kwenye blenda mpaka upate mchanganyiko safi mzito.

Kisha kata kata vipande vidogo vya keki kwenye glasi yako ya kioo weka nusu ya glasi na kisha panga strawbery kwa juu.

mwisho mwagia ule mchangayiko wako uliosaga kwenye blenda mimina pole pole mpaka ufike chini ya glasi kama inavyoonekana kwenye picha.

Weka katika friji ipoe, wakati wa chakula mpatie kila momoja glasi yake peke yake afurahie.







 MIXED BERRIES TRIFLE

MAHITAJI

200 gram Raspberryies
200 gram Starwberries
200 gram Blue berries
2 box finger biscuits
1 jani la mint
100 gram sukari nyeupe safi
1 lita ya fresh cream


JINSI YA KUANDAA

Kama kawaida piga fresh cream na sukari na kisha weka katika friji ipoe

Chini kabisa ya bakuli lako panga finger biscuit kumbuka kuzikata nusu usiziweke zikiwa ndefu kabisa.

Kisha mwagia cream juu yake na sambaza vizuri kabisa.

Kisha panga strawberru ulizozikata nusu kama inayoonekana katika picha  hapo chini.

Kisha mwagia kwa juu fresh cream.

Juu yake panga blue berries safi kabisa.

Juu yake mwagia fresh creama na sambaza vizuri kabisa kisha juu yake panga biscuit na raspberries pamoja na cream kidogo kati kati kabisa mwisho pamba na jani la mint.







SIO KAZI NGUMU KABISA UKIFATILIA MAFUNZO VIZURI PAMOJA NA PICHA PIA MAHITAJI YOTE HAYA YANAPATIKAMA KATIKA SUPERMARKET AU MADUKA YA VYAKULA NA MBOGA MBOGA SIO GHALI JITAHIDI SIKU MOJA MOJA WAFURAHISHE FAMILIA YAKO.



Monday, August 23, 2010

SALAD NZURI KWA AFYA YAKO WEWE MLAJI

MAHITAJI

1 paketi ya Spagheti
2 Nyanya
1 kitunguu
1 lettuce
150 gram Balsamic vinegar
5 gram Chumvi
5 gram Pili pili manga
1 Tango


JINSI YA KUANDAA

Chemsha spagheti isiive sana iive kiasi tu ili iwe ngumu na ipendeze katika sahani na kuleta ladha safi kwa mlaji

Ikisha iva weka pembeni ipoe na baada ya hapo changanya chumvi, pili pili manga na balsamic vinegar pamoja na hiyo spagheti.

kisha kata slice ya nyanya, tango pamoja na kitunguu kama inavyoonekana kwenye picha.

weka jani la lettuce kwa mbele kisha kati kati ya sahani weka mlima mdogo wa spagheti iliyokwisha changanywa, kwa nyuma weka slice za tango na kwa juu weka slice ya nyanya na kitunguu.



Huu ni muonekano wa salad yako kwa juu ikiwa imekamilika tayari kwa kumpatia mlaji


Muonekano huu kwa pembeni salad safi ya tambi na mboga majani waandalie familia wafurahie.


SPAGHETTI WITH MUSHROOM SAUCE

Tambi na mchuzi wa uyoga recipe hii safi sana pia kwa wanaofunga kwasasa unaweza badilisha mapishi ya tambi zako kwa mapishi haya

MAHITAJI

1 paketi ya Tambi
200 gram uyoga
1 kitunguu maji
50 gram pili pili hoho
20 gram kitunguu swaumu
100 gram fresh cream
50 gram maziwa ya maji
50 gram parmesan cheese
5 gram kungu manga ya unga
1 nyanya
1 jani la basil
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya olive
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga

JINSI YA KUANDAA

Chemsha tambi zako ziive vizuri kumbuka zisiive sana kisha ziweke pembeni zipoe

Kata kata mchanganyiko wa kitunguu maji, uyoga, pili pili hoho kisha weka katika sufuria yenye mafuta ya oilive yamoto kaanga kiasi kisha weka kitunguu swaumu.

kisha weka maziwa ya maji pamoja na fresh cream changanya kwa kadika1 tu ikishapata moto weka tambizako pamoja na parmesana cheese koroga mapaka ichanganyike safi kabisa kisha weka chumvi na pili pili manga pamoja na kungu manga ya unga itakua imeva safi kabisa tayari kwa kuliwa.

kwenye sahani pamba na kipande cha nyanya na jani la basili pembeni unaweka cheese kiasi ukizingatia cheese inapendeza sana kuliwa na tambi.



Huu ni muonekano wa Tambi ya uyoga ni tamu sana inafaa kwa futari na ni rahisi sana kuandaa hasa kwa wafanyakazi au wafanya biashara unarudi nyumbani umechoka chakula hiki ni rahisi sana kuandaa. Unaweza chemsha tambi nyingi na ukahifadhi kwenye friji ukawa unapika kidogo kidogo kwa mitindo tofauti.

ENJOY!!


Friday, August 13, 2010

UNAMPENDA MWANAO!??? KAA TAYARI KWA TAKE AWAY SAFI ZA SHULE AU PICNIC

YAMY YAMY!!!!!! ITS KIDS CORNER

 
TUMA EMAIL KWA issakesu@gmail.com ILI NIKUTUMIE MENU NA JINSI YA KUANDAA TAKE AWAY YA MWANAO WAKATI WA SHULE AU AKIWA NA PICNIC IKIWA KATIKA Ms Word .



Huu ni muonekano wa croisant ikiwa na mchanganyiko wa mboga majani, cheese na matunda



Huu ni muonekano wa matunda mchanganyiko


Huu ni muonekano wa samaki ikiwa safi sana na mboga majani


Huu ni muonekano wa wali ukiwa na dengu safi sana


Inategemea una vyombo vizuri na vikubwa kutosha mchanganyiko huu kwajii ya watoto wako? tuma email upate maelezo zaidi jinsi ya kuandaa.



Huu ni muonekano wa mkusanyiko wa vyakula vyote, nawapenda sana sana watoto!!!


UNAWEZA MFUNGASHIA MWANAO LUNCH BOX SAFI SANA NA ASIHANGAIKE NA NJAA AU KUNUNUA CHAKULA KISICHO SALAMA

Thursday, August 5, 2010

DONUT DONUT MHHHHHH SUPER DUPER!!!!!!

KITAFUNWA SAFI SANA HIKI KAA TAYARI RECIPE SAFI KABISA KWA MTINDO TOFAUTI KAMA UONAVYO KATIKA PICHA HAPO CHINI

MAHITAJI

2 Kijiko kikubwa cha chakula white vinegar
480 gram maziwa ya maji
2 kijiko kikubwa cha chakula siagi yeyote ile
120 gram sukari
1 yai
1/2 kijiko kidogo cha chai vanilla esence
480 gram unga wa ngano
1/2 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/4 kijiko kidogo cha chai chumvi
1.5 lita mafuta kwajili ya kukaangia 
120 gram sukari ya unga kwajili ya kunyunyizia kwa juu

JINSI YA KUANDAA

Mimina vinega kwenye maziwa, acha kwa dakika 5 hadi 10 maziwa yakatike na yawe mazito

Katika bakuli la wastani, changanya siagi na sukari mpaka vilainike kabisa kisha endelea piga yai na vanilla navyo vichanganyike vizuri kabisa.



Huu ni muonekano safi kabisa baada ya mchanganyiko wako kua laini kisha changanya kwa kutumia mchapo unga wa ngano, baking powder, na chumvi; Kisha chukua mchanganyiko wa maziwa na vinega mimina kwenye mchanganyiko huu wenye unga na siagi.



Huu ni muonekano wa mchanganyiko safi kabisa umeshakua mzito na umelainika safi sana


Sukuma mchanganyiko wako kama inavyooonekana kwenye picha na kisha kata miduara safi ya umbo la donut na kati kati toboa pia. Acha ya kae katika joto la chumba kwa dakika 10 iumuke.
Pasha mafuta kwenye kikaango chako kwa 375 degrees F (190 degrees C).



Kaanga donut zako kwenye mafuta moto mapaka upate rangi nzuri ya kahawia, Kumbuka kugeuza mara kwa mara ili yasiive upande mmoja tu. Toa katika kikaango na weka katika wavu au towel ili inyone mafuta.



Kwakutumia unga ule ule unaweza ukatengeneza hizi donut za mviringi (donut rolls) kisha kaanga na ukimaliza kabla hazijapoa zimwagie sukari ya unga zitakua tamu sana na muonekano tofauti


Huu ni muonekano safi sana wa donut yako iliyoiva na isiyo na mafuta kabisa ndani na juu ina gamba safi gumu litakalo kufanya ufurahie sana na usikinai kula hata zikiwa 10.

RECIPE HII NI SPECIAL NAINANI WENGI WENU HAMUIJUI WAPIKIE FAMILIA WAFURAHIE PIA UNAWEKA WEKA CHOCOLATE JAM YA LADHA YEYOTE ILE KATI KATI YA DONUT YAKO ILI KUONGEZA LADHA. MAFUNZO YAJAO NITAONYESHA JINSI YA KUONGEZA LADHA HIZI TOFAUTI.

NAWATAKILA RAMADHANI NJEMA WAPENZI WOTE WA BLOG AMIIN!!!


HII NDIO PASTA TAGLIATELLE NA CARBONARA SAUCE

MAHITAJI

1 paketi ya spaghetti au tagliatelle
1 Kijikokikubwa cha chakula olive oil
8 vipande vya bacon ( ya nguruwe au ya ngombe au Bata mzinga) chop chop
1 tablespoon olive oil
1 Kijikokikubwa cha chakula kitunguu maji chop chop
5 gram kitunguu swaumu kilichosagwa
30 gram dry white wine (Sio lazima)
100 gram fresh cream
4 mayai
120 gram Parmesan cheese ya unga
10 gram ya pili pili manga na chumvi
2 Kijikokikubwa cha chakula chopped fresh parsley
2 Kijikokikubwa cha chakula Parmesan cheese ya unga pia

JINSI YA KUANDAA

Weka chumvi katika maji kisha chemsha, yakisha chemka weka pasta yako iive wastani isirojeke. Kisha chuja vizuri maji yote na weka kijiko kimoja cha olive oil changanya vizuri hii husaidia pasta isishikane, iweke pembeni.

Wakati huo huo pika chopped bacon katika kikaango chenye mafuta kiasi mpaka iwe crisp; Kisha itoe na tumia kitambaa kuikausha kutoa mafuta. Chukua kijiko kimoja cha olive oil kilichoakia, kisha weka kwenye kikaango juu ya moto. Ongeza chopped kitunguu maji, kisha pika katika moto wa wastani mpaka vitunguu vilainike. Kisha ongezea kitunguu swaumu, kaanga kwa dakika moja tu. Kisha weka wine kama unapenda; pika kwa dakika moja tena.

Baaada ya hapo chukua ile bacon iliyoiva weka kwenye kikaango; Kisha weka pasta yako pia. , ongeza tena  olive oil kisai kama inaonekana kukauka au inashikana . Vunja mayai yapige pige na cream kwa mchapo na kisha mwagia ndani ya pasta pole pole huku ukichanganya kwa kutumia uma au tongs mpaka mayai yachanganyikane na pasta yako saafi. QHaraka haraka ongeza 120gram Parmesan cheese, kumbuka kuchanganya tena. Ongeza chumvi na pili pili manga kwaajili ya ladha safi (Kumbuka kua bacon na Parmesan zina chumvi).

Kisha itakua imeiva mpatie mlaji haraka sana rushia kwa juu chopped parsley pamoja na ile Parmesan cheese iliyokua imebakia.
 
 

Huu ndio muonekano wa pasta tagliatelle


Huu ni muonekano wa bacon na brocoli

Huu ni mchanganyiko wa mayai na fresh cream


Huu ni mchanganiko wa mayai yaliyopigwa na cream kisha yakamwagiwa kwenye kikaango chenye vitunguu na bacon chop chop

Huu ni muonekano wa mchanganyiko mzima wa pasta na viuno vyote pia imeongezewa na brocoli kuongeza ladha zaidi unaweza tumia mboga aina yeyote ile


Huu ni muonekano wa pasta tagliatelle imeshaiva na tayari kwa kuliwa juu imerushiwa chop parsley na parmesan cheese ukweli ni tamu sana sana.



Kwa kutumia recipe hii unaweza ukatumia aina yeyote ile ya pasta na ikaiwa jina la aina hiyo ya pasta mfano katika picha hiyo hapo juu inaitwa spaghetti carbonara ukitumia pene pasta itaitwa pene pasta carbonara.

ENJOY NA FAMILIA YAKO CHEERS!!!!


ROAST LEG OF LAMB/ MGUU WA MBUZI AU KONDOO WA KUOKA


CHOMA MBUZI AU KONDOO KISHA KULA NA SALAD YA SPINACH NA VIAZI VYA KUOKA MHHHH YAM YAM!!!!!!!!!!!!!!!!

MAHITAJI

1 Nyama ya mbuzi mguu wa mbele au wa nyuma
2 kilo viazi ulaya ( viazi mbatata)
1 kilo nyanya
1 kilo spinach
1 kopo tomato pest
1 chupa ndogo tomato sauce
200 gram soya sauce
50 gram curry powder
50 gram kitunguu swaumu
50 gram tangawizi
100 gram mafuta ya kupikia
50 gram chumvi
100 gram maji ya limao
50 gram masala spice

JINSI YA KUANDAA

Changanya vitu vyote hapo juu kwa wakati mmoja na kisha paka nyama yako ya mbuzi au ya kondoo kisha iweke kweneye friji kwa masaa 3 hadi 4


Huu ni muonekano wa mguu wa kondoo mbichi


Huu ni muonekano wa nyma hii baada ya kuwekewa marination ( Viungo au vikorombwezo) iweke kweye chombo utakachotumia kuokea kweney oven. kisha funika chombo hicho kwa kutumia aluminium foil. choma katika oven kwa masaa 2 kwa mto wa juu. kisha toa nyama itakua imeiva safi na laini.



Hapa ni baada ya kutoka kwenye oven ina waka waka imeshaita tayari kwa kuliwa. Kama unawageni unaweza kuwashangaza kwa kuwasha jiko la mkaa na ukaiweka juu yake kila mgenia anapita unamkatia kama ndafu vile hahahahahahahaaaaaa!!!


Hapa ni baada ua kukatwasasa muonekano ilivyoiva kwa ndani nyama hii inakua laini sana na tamu hasa si mchezo!!!!


Huu ni muonekano wa viazi vya kuoka, kuviandaa unamenya kama kawaida kisha una vipaka mafuta ya kula na chumvi kisha unaviweka kwenye oven una bake mpaka uone vimebadilika rangi na vimekua laini.


Huu ni muonekano wa spinach ya kukaanga na nyanya za kuoka kwajili ya salad
JINSI YA KUANDAA SALAD HII

Kaanga spinach kwenye kikaanga kwa kutumia mafuta ya kula na chumvi kisha iweke pembeni ipoe.

kisha kata nyanya katika vipande viwili kisha iweke kweney oven oka kwa mto mdogo sana kwa muda wa saa 1 inyauke yu isirojeke.

kisha chukau mchanganyiko wa spinach, tango na nyanya kata vipande vidogo na changanya pamoja na goat cheese ay fettah cheese. Nyunyizia kidogo olive oil, chumvi pamoja na vinegar iweke kwenye friji ipoe tayari kwa kuliwa. 

Huu ndio muonekano wa salad yetu safi kabisa yenye cheese ya mbuzi ( goat cheese) na mchanganyiko wa mboga majani

BADILISHA MLO WA WEEKEND HII KWA RECIPE HII SAFI KABISA