Monday, January 31, 2011

JIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA MKATE HUU MWEUPE WA KUKUNJA


MKATE HUU NI MAARUFU SANA NCHINI SWISS NI MKATE MWEUPE WA KUKUNJA PIKA KAMA KITAFUNWA WAKATI WA CHAI ASUBUHI FAMILIA IFURAHIE


MAHITAJI

720 gram unga wa ngano

1 kijiko kidogo cha chai chumvi
1 kijiko kikubwa cha chakula amira ya chenga
1 kijiko kidogo cha chai asali
240 gram maziwa ya vugu vugu
4 kijiko kikubwa cha chakula siagi iyeyushe kidogo 
1 yai
JINSI YA KUJIFUNZA FATILIA MAFUNZO HAPO CHINI KATIKA PICHA



















































JIFUNZE KUTENGENEZA PASTA HIZI ZA AINA YAKE


YAWEZEKANA UNAZIONA PASTA HIZI KILA UNAPOINGIA SUPERMAKET AU DUKA LOLOTE LA CHAKULA LAKINI HUVUTIWI KUZINUNUA SASA JIFUNZE MAPISHI YAKE NA FAMILIA YAKO ITAFURAHIA SANA.


MAHITAJI

1 paketi ya Jumbo Pasta Shells ( tumia 10-15 shells kwa watu 2)

360 gram sauce ya nyanya 
180 gram Cottage Cheese, low fat
240 gram Ricotta cheese, low fat
240 Mozzarella cheese ya unga unga 
60 gram parmesan cheese ya unga unga 
1 fungu la giligilani chop chop 
1 fungu la parsley chop chop
1 kitunguu maji chop chop 
5 gram kitunguu swaumu
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga

JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO HAPO CHINI KATIKA PICHA



Pika Pasta shells katika sufuria kubwa, ili zisiweze kugandiana. Pika kwa dakika 10 tu ili zisirojeke maana zitaenda kuiva zaidi katika oven.


Katika kikaango, pika kitunguu na kitunguu swaumu weka 1 kijiko cha mafuta ya Olive mpaka vilegee kidogo kisha ongeza sauce ya nyanya.




 Kisha ongeza chumvi na pili pili manga na acha iendelee kuchemka.




Changanya aina zote 4 za cheeses pamoja na giligilani na parsley


Paka mafuta katika baking pan kisha weka juu yake sauce ya nyanya kwa chini. Chukua mchanganyiko wako wa cheese kisha weka katika jumbo shells moja baada ya nyingine kisha zipange katika bakin pan. Ukishamaliza, mimina juu ya pasta zako sauce ya nyanya iliyobaki.


Choma katika oven kwa moto wa 350F kwa dakika 15 hadi 20 kisha mpatie mlaji ikiwa yamoto.



CHAKULA HIKI NI RAHISI KUPIKA NA NIKITAMU SANA SANA WAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE

Wednesday, January 26, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA MKATE HUU AINA YA PUTO


MKATE HUU NI MWEPESI SANA NA UNAVIMBA UNAKUA KAMA PUTO KIASI FLANI UNAPENDEZA KWANI UNAKUA KAMA MKATE WA MAAJABU KAA TAYARI KWA RECIPE SOON.

MAHITAJI

240 gram unga wa ngano
1/4 chumvi kijiko kidogo cha chai
120 gram za maji (Usiweke maji yote inaweza zidi hii hutegemea na kiwango cha unga weka maji kidogo kidogo)




Changanya unga na chumvi katika bakuli


Weka maji katika unga kidogo kidogo endelea kukanda


Kanda pole poel mpaka unga wote uchanganyike. Hakikishs maji unaweka kidogo kidogo mpaka unga wote uchanganyike maana kiasi cha maji kitahitajika kutokana na kiwango cha unga. Pia unaweza ongezea kijiko kimoja cha mafuta moto uliyochemsha kwajili ya kuongeza ladha na ubora na uendelee kukanda na mchanganyiko wako usiwe laini sana wala mkavu sana uwe wastan.


Kanda vizuri kwa mara ya mwisho mchanganyiko wako uwe kama unavyoonekana katika picha.


Kisha kata vipande vidogo na zungusha miduara kama inavyoonyesha katika picha ukubwa wa miduara utategemea na ukubwa wa kikaango chako. Hakikisha hupotezi muda kata na sukuma haraka haraka kisha choma ili mkate wako utoke vizuri.


Sukuma kwa saizi ya wastani kama inavyonekana katika picha. Usisukume nyembamba sana zitakakamaa sana na hazitakua nzuri.


Hakikisha unarudia kwa kila miduara yote iliyobaki. Wakati huo huo hakikisha mafuta yanamoto na uanze kukaanga mkate wako.



Kata kipande kidogo cha unga na tupia katika mafuta kuangalia kama mafuta yamepata moto kama mafuta yanamoto kipande hicho kitachemka na kuja juu haraka. Mafuta yawe yamoto lakini sio moto wa kutoa moshi yataunguza mkate wako. Kama ukiweka kwenye mafuta ambayo hayana moto mkate wako utabaki flat na hautavimba na utameza mafuta hautakua mzuri tena.


Baada ya kuhakikisha mafuta yanamoto sasa tupia mkate katika mafuta.


Wakati mkate unapanda juu, Hakikisha unaendelea kumwagia juu ya huo mkate mafuta inasaidia uweze kuvimba.


Kumwagia mafuta inasaidia sana unaona sasa mkate umeshavimba na kupendeza.


Hakikisha una geuza geuza mpaka upate rangi nzuri unayoipenda wewe kahawia ya kawaida au kahawia ya udhurungi.

Weka katika paper towel ili ichuje mafuta. Kama ulikaanga vizuri haita meza mafuta na utakua mzuri sana sana.


Unaweza mpatia mlaji mkate huu na aina yeyote ya chakula utakachopenda au anachopenda. Unaweza mpatia mlaji mkate huu pamoja na Potato Masala (masala ya viazi ulaya) au njegere za nazi. Pia inapendeza sana kusave na sauce za aina mbili mint sauce na tamarind sauce ( Mchuzi wa ukwaju).



MKATE HUU UNAWEZA KULA KWA CHAKULA NA MCHUZI WA AINA TOFAUTI ANGALIA MUONEKANO MZURI WA MKATE HUU KATIKA PICHA TENGENEZA FAMILIA YAKO IFURAHIE SIO KAZI NGUMU.



JIFUNZE KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI KWAKUTUMIA UNGA WA MCHELE


KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA NA JINSI YA KUANDAA KITAFUNWA HIKI


MAHITAJI

240 gram Unga wa mchele

240 gram maji baridi
 2 kijiko kikubwa cha chakula dengu za njano
1 kijiko kidogo cha chai mbegu za Cumin
1 kijiko kidogo cha chai mbegu za ufuta
1 kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya samli
5 gram chumvi
1.5 au 2 lita ya mafuta kwajili ya kukaanga


JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI



Loweka dengu katika maji kwa saa 1



Kisha chukua dengu pamoja na maji uliolowekea weka katika moto ichemke changanya chumvi na samli ichemke pamoja kwa dakika 30 tu.


Baada ya hapo changanya na unga wa mchele ndani ya dengu zinazochemka. Hakikisha unatumia mwiko kuchanganya ili dengu zipondeke na zichanganyike vizuri kati ya maji na unga wa mchele kama unavyopika ugali. Unga ukichanganyika vizuri zima jiko haraka. Funika na kifuniko cha sufuria yako kisha weka pembeni kwa dakika 10 hadi 15.




Mchanganyiko wako ukishapoa changanya unga wa pili pili, mbegu za ufuta, mbegu za cumin kisha endelea kukanda tena kwa dakika 1 tu ili ichanganyike vizuri na kua laini pia unaweza ongezea chumvi kidogo kulingana na ladha upendayo.



Chukua kikaango kisha weka mafuta na weka katika jiko la moto, Hakikisha mafuta yanapata moto ila yasitoe moshi maana hayataivisha yatababua chakula chako. Kata kiasi kidogo cha unga kisha zungurusha kama unafinyanga kwa kutumia mikono miwili upate umbo la duara kama muonekano katika picha.



Kisha zungusha na ikutane ifunge kabisa na upate mduara safi kati kuwe na tobo hakikisha inashikana vizuri ili ukiaanga isiachane.




Huu ni muonekano wa umbo zuri la kitafunwa chetu


Endelea kwa mtindo huu mpaka mchanganyiko wote wa unga uishe. Unaweza tumia kitambaa au mfuniko kufunika ili unga wako usikauke na kuharibika. Weka miduara ya kitafunwa hiki kwakua mafuta yamechemka vizuri vitazama chini kisha vitajitokeza juu baada ya kuiva,



Punguza moto uwe wa stani ili usiunguze vitafunwa vyako


Hakikisha unakaanga mpaka upate rangi ya kahawia safi kabisa


 
Angalia picha ya chini kitafunwa kinapendeza zaidi kuliko kitafunwa katika picha ya hapo juu

Baada ya kitafunwa kuwa cha kahawia toa kwa kutumia mwiko wenye matundu ili kuchuja mafuta na weka katika taulo maalumu kwa jikoni ili ziendelee kujichuja mafuta.


Kisha weka katika bakuli baada ya kupoa kwa matumizi ya muda mrefu!



Kumbuka kua hutakiwi kukaanga kwa moto mdogo kwani kitafunwa kitanyonya mafuta na kua teketeke.



NAIMANI FAMILIA YAKO WATAPENDA SANA KITAFUNWA HIKI