Friday, August 26, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA KEKI HII SAFI KABISA YA MCHANGANYIKO WA NAFAKA


KAA TAYARI KWA KUJIFUNZA KUTENGENEZA KEKI HII SAFI KABISA NA RAHISI PIA HATUA KWA HATUA JINSI YA KUPAMBA KEKI

MAHITAJI

Mchanganyiko kwajili ya Cake

720 gram unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai Baking powder
1 kijiko kidogo cha chai chumvi
360 gram sukari
1 kijiko kidogo cha chai  unga wa Cinnamon
4 mayai vunja na ubakize ute mweupe tu
180 gram ndizi ya kuiva iponde ponde
120 gram Vegetable Oil
480 gram ndzi mbivu kata kata vipande
1 kijiko kidogo cha chai Vanilla Essence
120 gram kata kata vipande vya nanasi
240 gram vunja vunja koroshon za kuokwa

Mchanganyiko kwajili ya Cream Cheese

1 lita ya light Cream Cheese isiyo na mafuta
120 gram  Butter au margarine
1 kilo Icing Sugar
1 kijiko kidogo cha chai Vanilla Essence
120 gram chopped koroso za kuokwa katika oven

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAEELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : saa 1 mpaka 2

Muda wa kupika : dakika 30 mpaka saa 1
Idadi ya walaji : 8 na zaidi




Katika bakuli changanya unga wa ngano, chumvi, sukari, baking powder na unga wa mdalasini ( cinamon)



Changanya vizuri mpaka vichanganyike kabisa

 

Chukua bakuli kisha piga ute mweupe wa yai na uchanganye na mafuta, vanilla pamoja na ndizi ya kuiva ulio iponda ponda kisha mimina mchanganyiko huu katika unga wako.



Tumia mwiko kuchanganya mchanganyiko huu pole pole mpaka uchanganyike.



Huu ni muonekano safi kabisa unga wako umechanganyika vizuri kwa kutumia mwiko.



Baada ya hapo weka vipande vya nanasi ulivyo kata kata, 240 gram ya korosho zilizookwa pamoja na vipande vya ndizi mbivu.



Endelea kuchanganya kwa kutumia mwiko mpaka upate mchanganyiko safi kabisa.



Chukua vyombo vya kuokea keki vyenye vya mduara na kina cha 9-inch  kisha mimina mchanganyiko wako sawa kwa sawa katika vyombo vyote vitatu.



Coma keki yako katika moto wa 350° kwadakika 25 mpaka 30 inategemea na oven yako pia unaweza choma mpaka ukiweka katika keki tooth pick na inatoka kavu. Poza keki zako katika wire racks kwadakika 10; kisha toka katika pans ilizo chomea, na kisha ziache zipoe moja kwa moja katika wire racks.



Kwajili ya kupambia: Piga cream cheese pamoja na  butter kwa speed ndogo kwama unatumia mashine ya umeme mpaka ilainike kabisa.



Pole pole na kidogo kidogo mimina icing sugar,



endelea kupiga kwa speed ndogo mpaka iwe nyepesi na inapanda



Kisha ongezea vanilla.



Paka mchanganyiko wako wa Cream Cheese katika kila keki yako kwa upande wa juu tu



Kisha zipandanishe na juu kabisa paka tena kama ionekanavyo katika picha



Kisha paka na pembeni ya keki pia kama picha inavyoonyesha iwe rafu rafu tu



Kisha mwagia juu ya keki yako 120 gram cup za korosho zilizookwa na ukazikata kata.


Kisha iweke keki yako katika friji. Ladha ya ndizi mbivu na nanasi pamoja na korosho inafanya keki hii iwe na ladha ya kipekee na ukiila mara moja utatamani kula kila siku!



Huu ni muonekano wa keki ikikatwa kwa ndani unaona mpangiliona muonekano wake  ulivyosafi?



KEKI HII NI SAFI, RAHISI KUANDAA NA TAMU SANA WAFURAHISHE FAMILIA YAKO NA MAPISHI SAFI YA KEKI HII.

Tuesday, August 23, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA KEKI YENYE LADHA YA MAEMBE


KAA TAYARI KWA KUJIFUNZA KUTENGENEZA KEKI HII YENYE LADHA YA MAEMBE NA MTINDI HALISI.

MAHITAJI

360 gram unga wa ngano 

1 kijiko kidogo cha chai Baking Powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
1 kijiko kidogo cha chai tangawizi ya unga
60 gram siagi isiyo na chumvi (Unsalted Butter) au blue band
60 gram Vegetable Oil (mafuta ya mahindi au ya olive )
240 gram sukari
4 ute mweupe wa mayai
100 ml Mtindi halisi (Natural Yogurt)
1 kijiko kidogo cha chai vanilla essence
60 gram juisi nzito ya maembe
1 limao kwaruza upate chenga chenga ( Zest)



JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa kuandaa : Dakika 30

Muda wa mapishi : dakika 30 mpaka saa 1
Idadi ya walaji : Watu 3


Washa oven iwe na joto la170C (350F). Paka siagi tray yako ya kuokea keki. Weka unga wa ngani kwenye bakuli pamoja na baking powder, chumvi na Tangawizi ya unga kisha weka pembeni.



Changanya zest za limao pamoja na sukari



Kanda kwa mikono ili iweze kuchanganyika.



Kisha chukua bakuli lenye sukari, siagi na mafuta ya olive au ya mahindi.



Kisha chukua bakuli nyingine weka ute mweupe wa mayai piga pamoja na vanilla mpaka itoe povu.



Kisha chukua mchanganyiko wa mayai piga pamoja na mchanganyiko wa sukari na siagi.
  


Baada ya kuchanganya vizuri kisha chukua yogurt na mwiko koroga pole pole mpaka ichanganyike vizuri



Kisha mimina unga pole pole na changanya kwa kutumia mwiko



Koroga mpaka uchanganyike vizuri kabisa endelea kuongeza mtindi mpaka upate mchanganyiko mlaini na mzito kwa ajili ya keki



Kisha ongezea mchanganyiko wa maembe na endelea kuchanganya vizuri.



Kisha mimina mchanganyiko wako kwenye tray ya kuokea  na choma kwa dakika 50 mpaka 60.



Baada ya hapo hakikisha unachoma inakua na rangi safi ya kahawia. Kuiva kwa keki yako itategemea na aina ya kikaango ulichotumia na aina ya oven ukliookea mimi huwa nachoma kwa dakika 35 tu na inaiva.



Acha keki ipoe katika kikaango kwa dakika 5 mpaka 10 kisha toa na weka katika sahani tayari kwa kuliwa.



 Ukiikata kwa ndani inakua laini safi kabisa na muonekano kama huo.



Unaona keki hii ilivyochambuka?




Ubora wa keki unategemea mchanganyiko mzuri, na muonekano wa keki inategemea na aina ya kikaango unachotumia.

 
NI NAFUU NA RAHISI KUTENGENZA WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE


Monday, August 15, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA ICE CREAM YA MATUNDA BILA KUTUMIA MAYAI


HUU NI WAKATI MUAFAKA KWA WASIO TUMIA MAYAI KULA ICE CREAM PIA ISIYOKUA NA MAYAI NA IKAWEKWA LADHA TOFAUTI ZA MATUNDA.


MAHITAJI

360 gram fresh Strawberries kata ndogo ndogo
300 gram maziwa ya maji
30 gram sukari
360 gram Fresh Cream
1-1/2 kijiko kidogo cha chai Vanilla Essence
5 gram chumvi

 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa kuandaa : Masaa 2 mpaka 4
Idadi ya walaji : 8 mpaka 10


Chukua strawbery zilizokatwa vipande vidogo kisha weka katika bakuli pembeni.




Katika bakuli jingine safi weka maziwa, sukari, vanilla na chumvi changanya mapaka sukari iyeyuke.



Kisha changanya pia na fresh cream.



Kisha chukua strawberries pamoja na mchanganyiko wa maziwa na cream. Funika na weka katika friza gandisha kwa saa 1 hadi masaa 2 au usiku kucha. Mimi huwa nagandihsa kwa masaa 2.



Washa  icecream maker kisha mimina mchanganyiko wa strawberry


Kuanzia hapa andaa ice ceram yako kama mashine inavyokuelekeza ( instruction manual )



Hapa ndio muonekano baada ya dakika 20.



Hahahaaa unaona kuna vijiko viwili hapo mhhh yaani mke wangu alikua anaisubiria kwa hamu sana kwahiyo nilipofunua tu mashine kuchota nae akaja nyuma na kijiko chake na kuchota pia



Huu ni muonekano safi baada ya ice ceram kua imakamilika. Toa katika mashine na weka katika chombo chako funika na karatasi ya plastic. Kisha osha vizuri mashine yako uliotumia.



Kisha igandishe kwa masaa 2 na huu ndio utakua muonekano wake.



Huu ndio muonekano halisi wa ice cream baada ya kupambwa katika bakuli ni laini , nyepesi kuandaa na haina mayai.




• Unaweza tumia strawberries za kopo au za kuagandishwa badala ya fresh.
•Kama hauna ice cream maker, Angalia katika mafunzo yalio pita ujifunze kuandaa bila ya kutumia mashine click link hii hapo chini utapata hatua zote za utenegenezaji bila mashine http://activechef.blogspot.com/2010/01/utengenezaji-wa-ice-cream-bila-ya.html.

JITAIDI TENGENEZA NYUMBANI FAMILIA IFURAHIE NI RAHISI SANA NA NAFUU



Tuesday, August 9, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI ZA AINA YAKE


KWA WAKATI HUU WA RAMADHANI JIFUNZE KUTENGENEZA AINA HII YA TAMBI

MAHITAJI

240 gram unga wa ngano au unaweza tumia (Gram Flour)

60 gram unga wa mchele (Rice Flour)
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya moto
1/2 kijiko kidogo cha chai binzali nyembamba ( cumin seeds) pia unaweza tumia hiriki kwa badala ya binzari nyembamba.
60 gram maji safi baridi na salama
5 gram chumvi.



JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa kupika: Sio zaidi ya dakia 15
Ujazo wa walaji: Watu 2 


Chemsha mafuta katika moto.Kisha chukua gram 60 za maji baridi safi na salama, chumvi na binzali nyembamba weka katika blender na usage.



Saga mpaka uhakikishe imelainika kabisa.



Chukua unga wa ngano, unga wa mchele na mafuta moto.



Kisha chukua ule mchanganyiko wa mbegu za binzari nyembaba uliosaga na chuja katika chujio ukimimina kwenye beseni la unga.



Kanda unga wote uchanganyike vizuri sana. Lazima unga huu uwe mgumu wastani na usiwe laini. Kama mchanganyiko umekua mgumu sana basi tumia kijiko cha maji kuoneza maji mapak upate ugumu wa wastani. Ni bora unga huu uwe mgumu kisha uongeze maji kuliko ukiwa laini uanze kuongeza unga.


Kisha tumia pasta maker - Muonekano wake ni kama hapo kwenye picha ina matundu madogo madogo.



Kata donge dogo kisha weka kweny pasta maker.



Kisha weka mafuta katika kikaango na yapate moto wa wastani. Kisha bonyeza mashine yako ya kutengenezea pasta kwa juu huku ukiizungusha kuzunguka kikaango chako (circular motion). Itasaidia pasta zako zisishikane.



Utaona mapovu mengi tu wakati tambi hizi zikiwa zinaiva ndani ya mafuta . Acha zijikaange kwa muda kiasi, ukiona tambi zako zimebadilika rangi na kua kahawia (yellowish red), jua zimeiva. Zigeuze upande wa pili kwa muda mfupi tu kisha zitoe.


Zitoe na ziweke juu ya kitambaa safu au ( paper towel).



Unaweza ukaziacha kama zilivyo au ukazikata katia vipande vidogo. Unaweza zihifadhi katika chombo kisichopitisha hewa ka maisha marefu na ukaendela kufurahia pole pole.



Huu ndio muonekano wa tambi baada ya kuiva

 

Ni tamu sana na ni nafuu na rahisi kuziandaa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani
WAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE