Monday, August 15, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA ICE CREAM YA MATUNDA BILA KUTUMIA MAYAI


HUU NI WAKATI MUAFAKA KWA WASIO TUMIA MAYAI KULA ICE CREAM PIA ISIYOKUA NA MAYAI NA IKAWEKWA LADHA TOFAUTI ZA MATUNDA.


MAHITAJI

360 gram fresh Strawberries kata ndogo ndogo
300 gram maziwa ya maji
30 gram sukari
360 gram Fresh Cream
1-1/2 kijiko kidogo cha chai Vanilla Essence
5 gram chumvi

 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa kuandaa : Masaa 2 mpaka 4
Idadi ya walaji : 8 mpaka 10


Chukua strawbery zilizokatwa vipande vidogo kisha weka katika bakuli pembeni.




Katika bakuli jingine safi weka maziwa, sukari, vanilla na chumvi changanya mapaka sukari iyeyuke.



Kisha changanya pia na fresh cream.



Kisha chukua strawberries pamoja na mchanganyiko wa maziwa na cream. Funika na weka katika friza gandisha kwa saa 1 hadi masaa 2 au usiku kucha. Mimi huwa nagandihsa kwa masaa 2.



Washa  icecream maker kisha mimina mchanganyiko wa strawberry


Kuanzia hapa andaa ice ceram yako kama mashine inavyokuelekeza ( instruction manual )



Hapa ndio muonekano baada ya dakika 20.



Hahahaaa unaona kuna vijiko viwili hapo mhhh yaani mke wangu alikua anaisubiria kwa hamu sana kwahiyo nilipofunua tu mashine kuchota nae akaja nyuma na kijiko chake na kuchota pia



Huu ni muonekano safi baada ya ice ceram kua imakamilika. Toa katika mashine na weka katika chombo chako funika na karatasi ya plastic. Kisha osha vizuri mashine yako uliotumia.



Kisha igandishe kwa masaa 2 na huu ndio utakua muonekano wake.



Huu ndio muonekano halisi wa ice cream baada ya kupambwa katika bakuli ni laini , nyepesi kuandaa na haina mayai.




• Unaweza tumia strawberries za kopo au za kuagandishwa badala ya fresh.
•Kama hauna ice cream maker, Angalia katika mafunzo yalio pita ujifunze kuandaa bila ya kutumia mashine click link hii hapo chini utapata hatua zote za utenegenezaji bila mashine http://activechef.blogspot.com/2010/01/utengenezaji-wa-ice-cream-bila-ya.html.

JITAIDI TENGENEZA NYUMBANI FAMILIA IFURAHIE NI RAHISI SANA NA NAFUU



3 comments:

  1. samahani naomba ingredients za hiyo icecream

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru sana kaka kwa ufundi wako ila sasa mbona hutuandikii mahitaji? ili tujui tununue nini na nini maana kuangalia picha sometimes huwezi ni nini..

    ReplyDelete
  3. Habari za leo kaka Issa?

    Samahani mbona sjaona maelekezo yoyote kuhusu utengenezaji ice cream, naona picha tu lakini sioni ingredients wala process nzima ya utengezaji wake!

    Naomba uweke ili nasi tuenjoy home made ice cream tafadhali. Nakutakia Saum Maqbul

    Mama Sabrina
    Tzee

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako