Tuesday, August 9, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI ZA AINA YAKE


KWA WAKATI HUU WA RAMADHANI JIFUNZE KUTENGENEZA AINA HII YA TAMBI

MAHITAJI

240 gram unga wa ngano au unaweza tumia (Gram Flour)

60 gram unga wa mchele (Rice Flour)
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya moto
1/2 kijiko kidogo cha chai binzali nyembamba ( cumin seeds) pia unaweza tumia hiriki kwa badala ya binzari nyembamba.
60 gram maji safi baridi na salama
5 gram chumvi.



JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa kupika: Sio zaidi ya dakia 15
Ujazo wa walaji: Watu 2 


Chemsha mafuta katika moto.Kisha chukua gram 60 za maji baridi safi na salama, chumvi na binzali nyembamba weka katika blender na usage.



Saga mpaka uhakikishe imelainika kabisa.



Chukua unga wa ngano, unga wa mchele na mafuta moto.



Kisha chukua ule mchanganyiko wa mbegu za binzari nyembaba uliosaga na chuja katika chujio ukimimina kwenye beseni la unga.



Kanda unga wote uchanganyike vizuri sana. Lazima unga huu uwe mgumu wastani na usiwe laini. Kama mchanganyiko umekua mgumu sana basi tumia kijiko cha maji kuoneza maji mapak upate ugumu wa wastani. Ni bora unga huu uwe mgumu kisha uongeze maji kuliko ukiwa laini uanze kuongeza unga.


Kisha tumia pasta maker - Muonekano wake ni kama hapo kwenye picha ina matundu madogo madogo.



Kata donge dogo kisha weka kweny pasta maker.



Kisha weka mafuta katika kikaango na yapate moto wa wastani. Kisha bonyeza mashine yako ya kutengenezea pasta kwa juu huku ukiizungusha kuzunguka kikaango chako (circular motion). Itasaidia pasta zako zisishikane.



Utaona mapovu mengi tu wakati tambi hizi zikiwa zinaiva ndani ya mafuta . Acha zijikaange kwa muda kiasi, ukiona tambi zako zimebadilika rangi na kua kahawia (yellowish red), jua zimeiva. Zigeuze upande wa pili kwa muda mfupi tu kisha zitoe.


Zitoe na ziweke juu ya kitambaa safu au ( paper towel).



Unaweza ukaziacha kama zilivyo au ukazikata katia vipande vidogo. Unaweza zihifadhi katika chombo kisichopitisha hewa ka maisha marefu na ukaendela kufurahia pole pole.



Huu ndio muonekano wa tambi baada ya kuiva

 

Ni tamu sana na ni nafuu na rahisi kuziandaa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani
WAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE


3 comments:

  1. naomba recipe ya upikaji wa tambi maana picha sijazielewa.

    ReplyDelete
  2. NAOMBA RECIPE YA KUPIKA TAMBI.

    ReplyDelete
  3. Kaka siku hizi naona umebanwa sana, tunaomba usiwe unatusahau, Ramadhani njema.
    NB; Nakumbuka nilikuomba recipe ya vitumbua siku nyingi sijui umesahau! ukipata nafasi naomba utuwekee

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako