CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, January 8, 2010

UTENGENEZAJI WA ICE CREAM BILA YA KUTUMIA MASHINE

Ice cream ni kifunga hamu ya kula ( Dessert ) moja wapo nzuri sana na inaweza kuliwa na watu wa lika zote pia unaweza kula ice cream muda wowote ule utakaojisikia na ukafurahia hasa ukiangalia hali ya joto inayopatikana nchini kwetu. Fata maelezo hapochini jinsi ya kutengeneza pamoja na mahitaji ili ufanikishe uandaaji wako.

Vitu vya kuandaa.

Maziwa ml 240
Sukari ml 240
Chumvi kijiko kidogo cha chai robo (1/4)
Vanilla ya maji kijiko kikubwa cha chakula 1/2
Vanilla ya mti ml 120
Low fat maziwa ml 120
low fat cream ml 120
Whipping cream yenye ubaridi wa wastan ml 480
Biskuti zilizochovywa Chocolate cream ml 480


Badala ya biskuti zilizochovywa na chocolate cream unaweza weka vipande vya chocolate, unaweza weka mchanganyiko wa ladha mabalimabli mfano matunda kama strawbery, cherry, Embe kwa kuchanganya kiasi cha ml 480 kama inavyoonyehs hapo juu katika mtiririko wa vitu vya kuandaa.




Vunja vunja vipande vya biscuti vilivyochovywa na chocolate weka pembeni safi ukisubiri baadae kidogo kuzitumia.




Weka maziwa katika sufuria nzito kwenye jiko lenye moto wa wastan acha yachemke pole pole mpaka yatakapotoa mapovu pemebi ya sufuria yatoe na weka pembeni yapoe.



Baada ya kutoa maziwa katika moto na kuyaweka pembeni yapoe changanya sukari na chumvi ndani yake



Koroga vizuri maziwa hayo mpaka sukari na chumvi viyeyuke vizuri




Changanya tena whiping cream na vanillah kwenye maziwa yale pole pole kisha changanya maziwa na ile cream vilivybaki ambavyo vyote vinamafuta kiasi ( low fat ) mpaka ichanganyike vizuri.




Kisha mimina mchanganyiko wako wote kwenye bakuli safi la kioo ili uweze kupoa na kuganda


Baada ya kumimina katika bakuli chukua bakuli jingine kubwa kiasi ya lile lenye mchanganyiko wako kwajili ya kugandisha kua ice cream. Weka barafu katika bakuli hilo kisha weka juu yake bakuli lenye mchanganyiko wako. Baada ya mchanganyiko wako kupoa kabisa chukua plastic wrap funika bakuli lako vizuri na weka katika friji kwa masaa 4 au hata masaa 24 kwa kuweka mchanganyijo wako ndani ya friji itasaidia sana kubadilisha mchanganyiko kua rojo rojo au mzito na inakua rahisi kukoroga tena ili upate umbile halisi la ice cream na laini kwa mlaji.





Baada ya masaa 4 au masaa 24 toa mchanganyiko wako kwenye friji kisha koroga vizuri na mwikosafi wa mbao au kijiko kikubwa.



Kisha funika tena na plastic wrap au foil kitu chochote kitakachozui hewa kuingia katika bakuli lako tayari kwa kugandisha kwenye freezer. Baada ya hapo weka bakuli lako katika freezer na ruhusu mchanganyiko wako ukae kwa masaa 2 kwenye freezer kisha utoe.




Baada ya kutoa mchanganyiko wako katika freezer tumia mashine ya kuchapia au unaweza tumia mchapo wa chuma au unaweza tumia uma ya kulia chakula na kukoroga vizuri mchanganyiko amabao utakua tayari umeshaanza kuganda lengo ni kuvunjavunja mapande ambayo yameshaanza kuganda. Kisha funika na plastic wraptena na rudisha katika freezer kwa masaa 2.




Baada ya masaa 2 toa mchanganyiko wako na koroga kwa kutumia mashine au uma yakulia chakula. Ice cream yako itakua nzito safi lakini bado kwa kuweza kuchota na kuliwa, kama mchanganyiko bado haujaganda vizuri kutokana na nguvu ya freezer rudisha kwenye freezer igande tena kwa muda kiasi.




Baada ya ice cream yako kua imeganda vizuri chukua zile bisckuti zenye chocolate tupia katika mchanganyiko wako wa ice cream na uchanganye vizuri sana kwa umakini, aidha inaweza kua ni matunda ya ladha yeyote badala ya biskuti bado itapendeza na utakua umebadilisha ladha.



Kisha chukua chombo cha plastic kisafi na kikavu, weka mchanganyiko wako ndani yake na hakikisha unaacha nafasi ya inchi 1 au 1/2 inchi kwajili ya kutanuka.




Kisha funika vizuri plastic yako na mfuniko safi na uirudishe katika freezer iweze kuganda kabisa mpaka itakapokua ngumu.




Baada ya ice cream kua ngumu toa kwenye freezer fungua chombo chako cha plastik na tumia chombo maalumu cha kuchotea ice cream vipo vingi sana hapa nyumbani tanzania vinauzwa kwenye supermaket. Chota maumbo mazuri sana ya mviringo kisha weka kwenye bakuli au glasi ya udongo na ufurahie ice cream yako!!

NATUMAI MPAKA HAPO MTAKUA MMEELEWA VIZURI SANA SOMO HILI LA LEO NA KUWEZA KUTENGENEZA ICE CREAM SAFI KABISA WATOTO, BABA AU MGENI AKAFURAIA SANA CHAKULA HIKI CHEPESI.

NAOMBA MTENGENEZE KWAKUFATA MAELEKEZO VIZURI HALAFU MNIPATIE MATOKEA KISHA TUENDELEE NA SOMO BAADA YA KUTENGENEZA ICE CREAM HIYO UTAIPAMBA VIPI TUTAFANYA UPAMBAJI WA AINA TOFAUTI ZENYE LADHA MBALIMBALI YA ICE CREAM AINA 10 HADI 20.



5 comments:

Anonymous said...

asante sana kwa somo hakika nitajaribu kutengeneza hiyo ice cream bila mashine, masomo yako ni mazuri sana na asante sana mungu akubariki katika kazi yako.

Anonymous said...

Asante kwa recipe yako but naomba unieleweshe hiyo whipping cream inakuaje. Na inapatikana madukani?

Anonymous said...

asalam alaykum kaka issa,nashukuru sana kwa mafunzo yako haya unayotupatia na lugha nyepesi kabisa inayoeleweka MUNGU akubariki sana na akulipe ujira wako kamili
mm nina swali hii whipping cream ni ya maji coz mm nijuazo ni za unga au hiyo ya unga unaongeza maji kaka sijaelewa hapo naomba unifahamishe
asante
kazi njema

Unknown said...

Jamani mm naomba mnijuze namna ya kutengeneza chostick au wengine wanaiita ramba ramba.
0656550367 namba ya nifundisheni plz

Unknown said...

Nifundishen namna ya kutengeneza ramba ramba au chostick naombeni msaada wakuu wangu