Monday, August 1, 2011

JIFUNZE KUANDAA PUDING YA WALI NA CHOCOLATE


NAWATAKIA RAMADHANI NJEMA WAPENZI WOTE WA BLOG HII YA MAFUNZO YA CHAKULA BORA NA SALAMA

KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI YA PUDING YA MCHELE NA CHOCOLATE

MAHITAJI

120gram mchele mnene

600 gram Maziwa
5 gram chumvi
120 gram Sukari
2 kijiko kikubwa cha chakula maizena Cornstarch
2 kijiko kikubwa cha chakula maji safi na salama
1 kijiko kidogo cha chai Vanilla
120 gram Semi-Sweet Chocolate chips
Raspberries, majani ya Mint na sukari ya unga kwa kupambia (sio lazima)

JINSI YA KUANDAA FATILI PICHA NA MAELEZO CHINI

Muda wa kuandaa : masaa 4 mpaka 8
Muda wa kupika : dakika 30 mpaka saa 1
Idadi ya walaji :  Watu 4 mpaka 6


Katika bakuli weka mchele na uloweke usiku kucha katika maji ya vugu vugu.

 

Kisha chuja maji na uweke pembeni.

 

Kisha chemsha maziwa angalau yawe ya vugu vugu.

 

Kisha ongeza maziwa na chumvi.


Endelea kuchemsha kwa moto wa wastan. Funika kisha endelea kuchemsha kwa saa 1. Hakikisha maziwa yasichemke sana.

 

Baada ya dakika 30 Huu ndio muonekano wa chakula hiki.

 

Kisha ongeza sukari na ukoroge. Funika kisha endelea kuchemsha kwa dakika 15

 

Changanya maizena (cornstarch) kwenye maji mpaka iyeyuke.

 

Chukua mchanganyiko wa maizena kisha weka katika mchanganyiko wa mchele na maziwa.

 

Funika na kisha endelea kuchemsha kiasi kw amoto wa pole pole kwa dakika 15 tena

 

Kisha weka vanilla. Kisha pika tena kwa dakika 1 na uzime jiko



Kisha weka chocolate chips

 

Kwakua mchanganyiko wa maziwa na mchele una uvugu vugu chocolate itayeyuka haraka jitaidi kukoroga vizuri ichanganyike.

 

Hapa mchanganyiko upo safi kabisa na tayari kwa kuliwa

 

Unaweza mpatia mlaji kikiwa cha moto au ukaweka katika friji ukala cha baridi. Unaweza kupamba na raspberries pamoja na mint.

 

Pia unaweza nyunyizia sukari ya unga kwa juu.

 


muonekano wa sukari ya unga unapendezesha zaidi ingawa sio lazima ni pendekezo la wewe muandaaji au mlaji.''

WAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE



3 comments:

  1. hizi picha ungekua unaweka na maelezo, inakua vigumu sana kujua ingredients zote.asante kaka

    ReplyDelete
  2. KAKA HATUONI RECIPE.
    ASANTE.

    ReplyDelete
  3. mmmh yum yum baada ya futari

    Tweety.

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako