Saturday, December 31, 2011

KHERI YA MWAKA MPYA WAPENZI WOTE WA BLOG YA CHAKULA SALAMA NA BORA



HABARI WAPENZI WA BLOG HII SAFI YA CHAKULA BORA NA SALAMA

NASHUKURU SANA KWA USHIRIKIANO WENU NA MCHANGO WA MAWAZO YENU PAMOJA NA KUA WASOMAJI WAZURI SANA WA BLOG HII.

CHANGAMOTO ZIMEKUA NI NYINGI SANA IKIWA MOJA WAPO NI MUDA WA KUKAA CHINI KUWEKA PICHA NA MAELEZO YA MAFUNZO JINSI YAKUNDAA VYAKULA.

TUOMBE UZIMA MOLA AKIPENDA NITIMIZE NDOTO YANGU YA KUANZA KUWEKA VIDEO HII HAITAKUA NA MASWALI MENGI MAANA KILA MMOJA WENU ATAONA NA MNAKIELEWA KISWAHILI KWA UFASAHA KABISA.

PIA WALE WOTE WALIOJIANDIKISHA KUJIUNGA NA CHAMA CHA WAPISHI TANZANIA KAENI TAYARI KABISA KWA MKUTANO MKUU WA CHAMA PIA TUWEZE KUCHAGUA VIONGOZI NA SHUGHULI ZA CHAMA KUANZA RASMI

KWA NIABA YA ACTIVE CHEF ASSOCIATION OF TANZANIA NA CULINARY CHAMBER BLOG NAWATAKIA MWAKA WA MAFANIKIO NA AFYA NJEMA 2012 MOLA ATULINDE SOTE NA ATUSIKILIZE DUA ZETU SOTE AMIIN

WASALAAM

CHEF ISSA


Thursday, December 29, 2011

JIFUNZE KUPIKA KITAFUNWA CHA SPINACH NA DENGU


KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABIS A YA KITAFUNWA HIKI CHA DENGU NA SPINACH

MAHITAJI

240 gram dengu (Whole Black Gram)

2 pili pili mbuzi (green chillies)
5 gram tangawizi ya kusaga
1 kitunguu maji kikubwa chop chop
240 gram spinach mbichi ikate kate (chopped Spinach)
5 gram chumvi
majani ya giligilani ya kuongeza ladha (Cilantro)
majani ya curry kwa kuongeza ladha (Curry leaves)
JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPA CHINI

Muda wa kuandaa : masaa 3 hadi 4

Muda wa kupika: dakika 30
Idadi ya walaji: Watu 4
Idadi wa vitafunwa : Kiasi cha 8-10 inategemea na upana au umbo


Loweka kwenye dengu  kwenye maji kiasi cha lita moja kwa masaa 2 hadi 3 au mpaka utakapo ona zimeshameza maji na kulainika.



Hakikisha unazichuja na kuzikausha vizuri kama picha inavyoonyesha.



Weka dengu zako kwenye blenda ( food processor) pamoja na chumvi, tangawizi na pili pili ila sio lazima kama hutumii pili pili ingawa inaleta ladha ya kuchangamsha. 


Hakikisha unasaga mchanganyiko uwe na muonekano kama huo usiweke kabisa maji ila kama blenda yako unaona haiwezi kusaga sababu ya ukavu basi weka maji kidogo sana ili uweze kusaga na kupata mchanagnyiko mkavu kama huo.



Kisha chukua dengu zilizosagwa weka katika bakuli pamoja na kitunguu maji, majani ya gili gilani, majani ya curry pamoja na spinach pia unaweza nyunyizia ndimu kiasi kuongeza ladha sio lazima.



Hakikisha unachanganya vizuri sana.



Kata kidogo na kisha hakikisha unatengeneza umbo la kama mpira.



Tumia karatasi ya Plastic na uipake mafuta kisha weka ule mviringo wa machanganyiko wa dengu na spinach juu yake kisha tumia vidole vyako viwili na ukandamize.



Tumia kidole chako na choma kati kati upate umbo kama la doughnut. Ni jinsi ya kutengeneza umbo zuri lakini sio lazima!



Chukua sufuria au kikaango weka mafuta kisha pata moto wa wastani chukua ile mchanganyiko kisha weka katika sufuria na endelea kukaanga hakikisha mafuta ni moto wasatani ili isibabuke na matokeo yake haiivi ndani (med-hot).



Kumbuka kugenuza mara kwa mara mpka upate rangi hii nzuri ya kahawia.



Kisha toa na weka katika karatasi ili yapoe na kuchuja mafuta pia. Kama ulifata maelekezo vizuri basi itaiva vizuri na wala hazitakau na mafuta kabisa karatasi haitaloana mafuta kabisa.



Hakikisha unampatia mlaji haraka sana ikiwa bado inamoto kwani ndio inakua na ladha nzuri pia unaweza kula na- Coconut chutney, spicy tomato chutney au tomato ketchup! ni nzito sana ukila unashiba kabisa.


Hazipendezi kukaa kwenye friji zaidi ya siku moja zinapoteza ladha na ubora pia

 



MIMI NA FAMILAI YANGU HUWA NAPENDA KULA NA SPICE TOMATO KETCHUP NA TUNAFURAHIA SANA. NI RAHISI KUTENGENEZA NA FAMILIA ITAFURAHIA SANA KITAFUNA HIKI.

Thursday, November 24, 2011

JIFUNZE KUPIKA DENGU HIZI TAMU SANA


 RECIPE SAFI SANA YA DENGU HIZI ZA AINA YAKE
MAHITAJI


240gram Pigeon Peas ( Dengu)
1/4 tsp Turmeric (manjano)
720 gram maji masafi
3  kijiko kikubwa cha chakula samli (Ghee)
1 kitunguu kikubwa chop chop
1 nyanya ya kuiva kubwa chop chop
1 kijikon kimoja cha chai binzali nyembamba
2 pili pli kavu nyekundu (Dried Red Chilies)
3 mbegu za karafuu
1 tangawizi ya kusaga (grated Ginger)
majani ya Curry na giligilani kwajili ya kupambia
5 gram maji ya limao
5 gram ya chumvi

JINSI YA KUANDAA CHAKULA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa kuandaa : Dakika 15

Muda wa kupika : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 4




Osha dengu katika maji baridi kisha zichuje vizuri.



Unaweza tumia njia mbili ya kuzipika hizi dengu moja ni kuloweka kwa masaa 2 kisha unazichemsha kwa sufuria ya kawaida au unaweza tumia pressure cooker na ukaweka manjano na kutumia maji gram 720.



Kwa kutumia preasure cooker ni dakika 10 tu zinakua zimeshaiva.



Wakati unachemsha dengu weka kikaango au sufuria ipate moto weka mafuta kisha ongeza samli (Ghee), binzali nyembamba, karafuu, pilipili, tangawizi, kitunguu maji pamoja na chumvi endelea kukaanga.



Vitunguu vinapoanza kuiva ongeza nyanya endelea kukaanga zikiiva weka majani ya curry na majani ya giligilani.



Toa dengu zako katika pressure cooker. dengu zako zitakua zimeiva kabisa na kua na ubora safi kabisa.



Maji yatakua yamekauka katika preasure cooker chemsha maji kikombe kimoja na weka katika preasure cooker na ukoroge.



Kisha chukua ule mchanganyiko wako wa vitunguu na nyanya kisha mimina kwenye dengu zako.



Hakikisha unaendelea kukoroga na ongeza maji ya limao pia kwa kuongezea ladha zaidi.



Hakikisha unampatia mlaji chakula hiki safi kabisa kikiwa chamoto unaweza kula na chapati, mkate, Tortillas, Naan or ugali pia hata wali na familia ikafurahia sana.



Binafsi huwa napenda kula ikiwa pamoja na chapati na wali ili kuongeza ladha na ubora huwa naongeza limao kwakua linasaidia kupunguza madini ya chuma katika dengu.








ANDAA CHAKULA HIKI KIZURI UKIWAPUMZISHA NYUMBANI KULA NYAMA MARA KWA MARA NA WATAFURAHIA KUANZA MWAKA NA CHAKULA SAAFI


 

Tuesday, November 22, 2011

HABARI WAPENZI WA BLOG


NIMEUMWA SANA NDUGU ZANGU KWA MUDA WA SIKU 7 SASA NASHUKURU ALLAH SASA NINANAFUU NA NITAENDELEA NA KAZI KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI ZA MWAKA MPYA NA CHRISTIMAS

CHEF ISSA

Thursday, November 10, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA WALI WA MANJANO

KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA NA RAHISI YA KUANDAA WALI HUU WA MANJANO NA KWA GHARAMA NAFUU SANA FAMILIA YAKO IFURAHIE

MAHITAJI

1 au 2 Saffron ( zafarani ya orange)


4 kijiko kikubwa cha chakula Olive oil
1 kitunguu kikubwa kata kata
1 pili pli hoho katak kata vipande vidogo vidogo
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kupondwa
240 gram mchele wa basmati
340 gram za maji ya vugu vugu
5 gram ya chumvi
majani kiasi ya giligilani kwa kupambia na kuongeza ladha
JINSI YA KAUNDAA FATILAI PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi: dakika 15

Muda wa mapishi: dakika 15
Idadi ya walaji: watu 2 

 

Katika kikaango weka kitunguu maji na safron pamoja na mafuta katika moto mdogo kisha endelea kukaanga pole pole. 


Baada ya mafuta kubadilika rangi ya orange. Kisha toa katika moto na acha ipoe kwa dakika 10 kisha yachuje hayo mafuta.


Kisha chukua kijiko kimoja kikubwa cha mafuta na weka katika kikaango. Kisha chukua tena kitunguu maji na kitunguu swaumu endelea kukaanga mapak vilainike. Kisha ongeza pili pli hoho na endelea kukaanga mpaka iwe laini.


Kisha weka mchele na endelea kukaanga pole pole mpaka mchele utaponukia na kubadilika rangi na kulainika.


KIsha ongeza maji na ufunike iendelee kuiva kwa dakika 8-10 kwa moto mdogo mpaka iive.


Baada ya kuiva kataka majani ya corriender na pamba katika wali wako.


Hakikisha unampatia chakula hiki mlaji kikiwa chamoto.



Unaweza kuongeza ladha ya chakula hiki kwa kuweka karanga au zabibu kavu au hata korosho kavu

Monday, November 7, 2011

JIFUNZE KUPIKA MKATE HUU WA UNGA WA ATTA NA KITUNGUU SWAUMU



KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA CHAPATI HII YA AINA YAKE

MAHITAJI

720 gram unga wa atta
3/4 kijiko kidogo cha chai Baking Powder
3 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kusagwa
1 kijiko kikubwa cha chakula sukari
60 gram olive Oil
120gram plain Yogurt
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya samli ( ghee)
60 gram majani ya korriender
5 gram chumvi


JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : saa 1
Muda wa mapishi : dakika 15
Idadi ya walaji : 4 watu
Idadi ya chapati : 10-12 inategemea na upana na ukubwa utakao penda



Weka unga wa atta katika beseni pamoja na baking powder, chumvi na sukari kisha changanya vizuri.



Kisha ongeza majani korienda, samli (ghee) pamoja na kitunguu swaumu na mtindi halisi usio na ladha ( Plain yorghut).



Kisha changanya vizuri.



Kisha chukua maji ya vugu vugu na weka kijiko kimoja kisha unachanganya endela na zoezi hilo mpaka upate mchanganyiko safi.



Endelea kuchanganya mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.



Kisha chukua unga wako weka katika mbao iliyomwagiwa unga na endelea kukanda kwa muda ili ulainike kabisa.



Hapa sasa mchanganyiko wako umekua laini na safi



Chukua mchanganyiko na uweke katika bakuli safi na kavu kisha funika kwasaa 1 hadi 2 na karatasi laini ya nailoni.



kisha anza kukata kiasi cha mduara ya unga ukubwa wowote unaopenda



Tumia rolling pin kisha tengeneza miduara. Usisahau kuweka unga kwenye kibao na kwenye rolling pin.



Mimina kiasi unga wa ngano kwenye kikaango.Kisha mwagia pande zote mbili za chapati yako mafuta na ukitaka ladgha safi tumia samli.



Kisha itaanza kuumuka kwa upande wa chini hiyo chapati.



Kisha geuza upande wa pili kisha chapati yako itaendelea kuumuka mara mbili ya umbo ulilosukuma mwanzo kisha malizia kupika kwa dakika 2.



Hakikisha unampatia mlaji chapati ikiwa yamoto. Mimi binafsi huwa napenda kula na yummy chicken au beef stew.



Huu ni muonekan safi wa chapati




Unaweza kula na soda, juisi, au chai pia hata kahawa na mchuzi mzito