Thursday, May 16, 2013

JIFUNZE KUPUNGUZA UZITO MKUBWA AU KULINDA UZITO WA KATI ULIONAO KWASASA

 
SOMA KWA UFASAA NA FATILIA KWA MAKINI MAELEZO HAPO CHINI JINSI VIMIMINIKA VINAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO MKUBWA NA KUA NA UZITO WA KAWAIDA HASA HASA KITAMBI IWE MWANAMKE AU MWAUME KITAPOTEA KABISA.

 KAMA UNAUZITO WA KAWAIDA ITAKUSAIDIA KUTO KUONGEZEKA NA KULINDA UZITO WAKO KWA AFYA NJEMA.

Fatilia kwa makini maelezo hayo hapo chini yatakusaidia sana.
.
1-
Asali inasaidia sana katika kupunguza uzito, Chukua asali 10 grams kisha tia katika maji safi ya vugu vugu yasiwe ya moto kisha kunywa kikombe kimoja kila siku mchana saa 6 na 12 jioni. Hii ni njia bora sanaya kukufanya wewe upunguze uzito bila ya kusababisha madhara katika mwili wao.
·          
2 - Unapokunywa chai ya asubuhi kumbuka kula vipande vya nyanya mbichi unaweza kuziweka katika mkate kama sandwich au unaweza kula tu zenyewe pamoja na mayai au chapati
·          
3  - Hii ndio iwe chai yako ya asubuhi, weka maji moto katika kikombe kisha ongezea vijiko 3 vya limao, pili pili manga 3 gram au chota kwa kwa vidole kidogo sana kwa ladha tu ili iwe kali pamoja na asali kijiko kimoja cha chai changanya vizuri kisha kunywa kila siku asubuhi.
·          
 4 - Kama una matatizo ya gesi tumboni au vidonda vya tumbo usitumie njia hiyo hapo juu namba 3 kwani maji ya limao na pili pili manga zitakuumiza unaweza kunywa chai ain ya (green tea). Inauzwa kila kona  katika maduka ya vyakula na ni nafuu itafanya kazi vizuri tu. 
·          
5 - Baada ya chakula cha jioni kuanzaia saa 2 hadi saa 3 usiku unaweza kunywa juisi nzito yenye mchanganyiko wa papai na karoti hakikisha hutii maji kabisa kwani papai lina maji ya kutosha. Juisi hii kunywa glasi moja kubwa baada ya mlo wa jioni itakusaidia sana kumeng'enya chakula tumboni na wakati wa usiku nakutoa ruksa kwa chai na jusi utakazokunywa kuanzia asubuhi mchana na jioni zifanye kazi.
Tiba Mbadala yakutumia vimiminika bila kujinyima kula fanya hivi kwa miezi 3 mpaka 4 utaona matunda yake. Ilinde familia yako kwa gharama nafuu sana.
 

3 comments:

  1. MBONA ASANTE,MANA NNA HUU UZITO SITAKI KUONGEZEKA ZAIDI YA HAPA NILIPO NAPATA TABU KWELI KU-MAINTAIN HAPA NILIPO

    ReplyDelete
  2. Nimeipenda hìi,hapa nina kg 25 za kupunguza.natumain itanisaidia

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako