Wednesday, May 22, 2013

MUDA SI MREFU NITAWEKA MAFUMNZO MBALI MBALI YA JINSI YA KUPIKA SAMAKI MAARUFU SANA AINA YA CHANGU

 
KAA TAYARI KWA MAFUNZO YA KUPIKA SAMAKI MAARUFU SANA AINA YA CHANGU KWA KUTUMIA MBINU MBALI MBALI ZAIDI YA 10 NA UTAALAMU WA KUMPAMBA KATIKA SAHANI AWEZE KUVUTIA WALAJI
 
 
 
Samaki changu mbichi akiwa ameshasafishwa safi kabisa
 

 
Samaki changu wa kuchoma kwa kutumia foil

 
Jinsi ya kuachanisha kati ya mifupa na nyama ya samaki changu

 
Jinsi ya kumchoma samaki changu katika jiko la mkaa

 
Jinsi ya kumuoka samaki changu katika ovena
 
 


Thursday, May 16, 2013

JIFUNZE KUPUNGUZA UZITO MKUBWA AU KULINDA UZITO WA KATI ULIONAO KWASASA

 
SOMA KWA UFASAA NA FATILIA KWA MAKINI MAELEZO HAPO CHINI JINSI VIMIMINIKA VINAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO MKUBWA NA KUA NA UZITO WA KAWAIDA HASA HASA KITAMBI IWE MWANAMKE AU MWAUME KITAPOTEA KABISA.

 KAMA UNAUZITO WA KAWAIDA ITAKUSAIDIA KUTO KUONGEZEKA NA KULINDA UZITO WAKO KWA AFYA NJEMA.

Fatilia kwa makini maelezo hayo hapo chini yatakusaidia sana.
.
1-
Asali inasaidia sana katika kupunguza uzito, Chukua asali 10 grams kisha tia katika maji safi ya vugu vugu yasiwe ya moto kisha kunywa kikombe kimoja kila siku mchana saa 6 na 12 jioni. Hii ni njia bora sanaya kukufanya wewe upunguze uzito bila ya kusababisha madhara katika mwili wao.
·          
2 - Unapokunywa chai ya asubuhi kumbuka kula vipande vya nyanya mbichi unaweza kuziweka katika mkate kama sandwich au unaweza kula tu zenyewe pamoja na mayai au chapati
·          
3  - Hii ndio iwe chai yako ya asubuhi, weka maji moto katika kikombe kisha ongezea vijiko 3 vya limao, pili pili manga 3 gram au chota kwa kwa vidole kidogo sana kwa ladha tu ili iwe kali pamoja na asali kijiko kimoja cha chai changanya vizuri kisha kunywa kila siku asubuhi.
·          
 4 - Kama una matatizo ya gesi tumboni au vidonda vya tumbo usitumie njia hiyo hapo juu namba 3 kwani maji ya limao na pili pili manga zitakuumiza unaweza kunywa chai ain ya (green tea). Inauzwa kila kona  katika maduka ya vyakula na ni nafuu itafanya kazi vizuri tu. 
·          
5 - Baada ya chakula cha jioni kuanzaia saa 2 hadi saa 3 usiku unaweza kunywa juisi nzito yenye mchanganyiko wa papai na karoti hakikisha hutii maji kabisa kwani papai lina maji ya kutosha. Juisi hii kunywa glasi moja kubwa baada ya mlo wa jioni itakusaidia sana kumeng'enya chakula tumboni na wakati wa usiku nakutoa ruksa kwa chai na jusi utakazokunywa kuanzia asubuhi mchana na jioni zifanye kazi.
Tiba Mbadala yakutumia vimiminika bila kujinyima kula fanya hivi kwa miezi 3 mpaka 4 utaona matunda yake. Ilinde familia yako kwa gharama nafuu sana.
 

Friday, May 10, 2013

JIFUNZE KUPANGA RATIBA YA MLO WA NYUMBANI KWA WIKI NZIMA

 
BAADA YA MAOMBI YA WANAFAMILIA WENGI WA KITANZANIA SASA NIMEAMUA KUFANYIA KAZI PIA RATIBA YA CHAKULA YA WIKI NZIMA KWA FAMILIA KUANZIA CHAI ASUBUHI, CHAKULA CHA MCHANA NA CHAKULA CHA JIONI.
 
KITABU KITAZINGATIA SANA MBINU ZA MAPISHI BORA KWA GAHARAMA NA FUU NA LADHA SAFI KWA CHAKUAL KITAKACHOKUA NA FAIDA NA MWILI WAKO.
 
PIA NITATENGENEZA NA DVD ITAKAYOKUA INAELEKEZA MAFUNZO YOTE YALIYOKUWEPO KWENYE KITABU HIKI. KITAKAPOKUA TAYARI NITAWAFAHAMISHA KUPITI UKURASA WA FACEBOOK.COM Active Chef NA www.activechef.blogspot.com
 
 
TUOMBEANE UZIMA, AFYA NA MAISHA MAREFU AMIIN ILI KILA ZURI NILILOJAALIWA TUWEZE KUGAWANA KWA NJIA MOJA AU NYINGINE AMIIN
 
 


JIFUNZE KUANDAA CHAKULA BORA NA SALAMA KWAJILI YA MWANAO

 
HABARI NJEMA WAPENZI WA BLOG www.activechef.blogspot.com MAMA YANGU MZAZI NI MTAALAMU WA CHAKULA NA LISHE NAMI NI MTAALAMU WA KUPIKA CHAKULA BORA NA SALAMA.
 
TUNASHIRIKIANA KUANDAA KITABU KITAKACHOKUA NA RATIBA YA WIKI NZIMA YA CHAKULA CHA WATOTO WA UMRI TOFAUTI, MAELEZO JINSI YA KUKIANDAA CHAKULA NA MAELEZO YA FAIDA YA CHAKULA HICHO KATIKA MWILI WA MTOTO KWA LUGHA YA KISWAHILI FASAHA NA VYAKULA VINAVYOPATIKANA POPOTE KWA URAHISI.
 
KITABU KITAKAPOKUA KIMECHAPISHWA TAYARI NITAWAFAHAMISHA WAPI VINAUZA NA KIASI GANI BADO TUPO KATIKA MAANDALIZI KWA HABARI ZAIDI USIACHE KUJIUNGA KATIKA UKURASA WETU WA FACEBOOK KWA HABARI ZAIDI NI facebook.com Active Chef
 
 
 
 
 

Wednesday, May 8, 2013

HABARI NJEMA ZITAWADIA MUDA SI MREFU LEO HII

 
 
HABARI WAPENZI WA BLOG HII YA CHAKULA BORA NA SALAMA NIMEKUA KIMYA KWA MUDA KUTOKANA NA MAJUKUMU YA KIMAENDELEO LEO
 
 
NIMERUDI TENA NDUGU ZANGU NA HABARI NJEMA KWENU KWANZA ANGALIA CHAKULA HIKI KISHA NIAMBIE UMEGUNDUA NINI?
 
 
KAZI KUBWA NI YA UTAFITI WA CHAKULA, MIMI NA WENZANGU TUNAFANYA UTAFITI WAKUCHANGANYA UTAALAMU WA UPISHI WA MATAIFA YA SCANDINAVIA NA AFRIKA NA KUONA WALAJI WATAIPOKEAJE BAADA YA HAPO TUTAANDAA KITABU CHA MCHANYIKO HUO WA TAALUMA SIPATI PICHA NITAKAVYOWALISHA WAZUNGU UGALI, KISAMVU, MLENDA NA MAKANDE HAHAHAAAAA
 
 
HALI YA HEWA NI NZURI SANA HAPA KISIWANI
 
 
SAFARI YANGU YA KUELEKEA KISIWANI ILIANZIA HAPA NIKAPANDA BOAT NA KUELEKEA KISIWANI KWAJILI YA KUANZA KAZI