KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA CHAKULA HIKI YA NAZI NA MBOGA MBOGA MCHANGANYIKO
MAHITAJI
120 gram Mtindi (yogurt)
1 kilo ya Mchanganyiko wa mboga ( karot, kiazi ulaya, njegere, pilipili hoho, bilinganya, kabichi na kitunguu)
1 kijiko kikubwa cha chakula cha mafuta ya nazi (coconut oil)
1 kijiko kidogo cha chai binzali nyembamba ( cummin seeds)
1 pili pili ya kijani mbichi
120 gram tui la nazi, ( Pia nazi ya kopo au ya paketi inafaa ingawa mimi napendelea nazi fresh)
0.5 kijiko cha chai unga wa manjao (turmeric powder)
5 gram chumvi
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Muda wa kuandaa: 30 dakika mpaka saa 1
Muda wa kupika: Chini ya dakika 15
Idadai ya walaji : Watu 2
Saga kwa pamoja machicha ya nazi, pilipili ya kijani na cumin seed upate tui zito.
Baada ya kupata tui zito kisha weka pembeni.
Weka mchanganyiko wa mboga zako katika sufuria yenye maji moto kisha chemsha kwa dakika 3 mpaka 3 kumbuka kuweka unga wa manjano na chumvi.
Baada ya kuchemsha kwa dakika 3 au 5 mboga zako zitakua zimeiva na maji yatakua yamepungua ongezea tui la nazi na endelea kuchemsha.
Wakati inaendelea kuchemka chukua mafuta ya nazi kisha weka katika kikaango na kaanga manjani ya giligilani au coriender leaves .Ikishatoa harufu safi tu toa katika moto
Chukua kikaango na mimina majani hayo kwenye sufuria ili ichemke.
Kisha toa sufuria katika moto. Baada ya chakula hiki kupoa kiasi kwa 37C ongeza mtindi (yogurt)
Hakikisha unachanganya vizuri.
Mchuzi mzito wa mboga mboga na nazi upo tayari! Hapa unaweza kula na wali au chapati au chochote upendacho wewe.
Lengo la kusubiri ipoe kiasi ni kusaidia mtindi usikatike ikiwa utachanganya wakati chakula bado ni cha moto
WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE SANA