CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, November 24, 2014

CHEF ISSA KUPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA JIJINI LUXEMBOURG KWENYE Villeroy & Boch Culinary World Cup 2014

HABARI NJEMA KWA WAPENZI WOTE WA BLOG HII
 
NAMSHUKURU MUNGU KWA KUCHAGULIWA KUSHIRIKI KAM MSIMAMIZI KWENYE WORLD CUP YA WAPISHI INAYOFANYIKA KILA BAADA YA MIAKA 4 NITAPEPERUSHA BENDERA YA NCHI YANGU TANZANIA NI JAMBO LA KUJIVUNIA SANA.
 
Mpaka sasa Chef Issa Kapande mbali ya kushinda tuzo nyingi tofauti katika fani yake ya upishi pia anashikilia rekodi ya kua Chef Mtanzania Msomi na mdogo kuliko wote aliewahi kufungua na kuongoza hotel ya nyota tano ( Certified Executive Chef) akiwa na umri wa miaka 25 tu. Hili ni jambo la kujivunia sana.
 
Mola ajaliapo natamani sana mwaka 2018 niipeleke Tanzanian national team kwenye mashindano haya na ninaimani tutafanya vizuri tu kwani kuna wapishi wazuri sana nyumbani Tanzania ingawa wamekosa nafasi au muongozo wa kuweza kuonyesha uwezo wao Mungu ibariki Tanzania.
 
 
Hapa chef Issa Kapande akiwa na management team ya East African All suits hotel alipofungua hotel ya nyota tano na kuandika historia ya kua certified Tanzanian Executive chef katika umri wa miak 25 tu. Hotel ilifunguliwa na aliekua makamu wa raisi Dr Shain ambae ni raisi wa Zanzibar kwasasa.
 
 
 
Chef Issa Akiwa kazini anamuwekea kuku wa kuoka viungo tayari kwa kuliwa

 
Chef Issa Akiwa na Mr Wyne aliekua FB manager wakati huo
 

 
Tuzo ya heshima kwa kutambua mchango wa chef Issa kwa chakula cha kiafrica ndio tuzo ya mwisho aliopata mwaka jana mwezi wa 10

 
Chef issa akiwa na jaji mkuu wa mashindano ya kumpata mpishi bora wa mwaka wa Sweden
 
kwa habari zaidi za kombe la dunia la wapishi unaweza zipata hapa http://www.vatel.lu/competitions.php
 
kwa habari zaidi za mapishi na za chef Issa unaweza like facebook page    https://www.facebook.com/pages/Active-chef/509561519067534
 
 
 
 
 
 
 
 


Friday, November 7, 2014

JIFUNZE KUTENGENEZA VITAFUNWA HIVI VYA AINA TATU KWA WAKATI MMOJA

 
KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA VITAFUNWA HIVI VITATU KWA WAKATI MMOJA INAPENDEZA SANA KWA CHAI YA SAA KUMI JIONI AU SAA NNE ASUBUHI
 
MAHITAJI
 
JINSI YA KUANDAA FATA MAELEZO NA PICHA HAPO CHINI
 

 
 


Saturday, October 25, 2014

JIFUNZE KUTENGENEZA BISIKUTI ZENYE MCHANGANYIKO WA KARANGA YA KUSAGA

 
JIFUNZE KUTENGENEZA BISIKUTI ZENYE MCHANGANYIKO WA KARANGA YA KUSAGA NA MAYAI
 
MAHITAJAI
8 kijiko kikubwa cha chakula butter au siagi
120 gram karanga ya kusagwa ilainike
180 gram sukari ya kahawia
2 kijiko kikubwa cha chakula asali
1 yai la kuku ( kama hutumii mayai weka 2 vijiko vya vegetable oil)
1 kijiko kidogo cha chai vanilla essence
360 gram unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai baking soda
120 gram karanga za kumenywa zilizokaangwa
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 

 
 

 
 


Wednesday, October 15, 2014

JIFUNZE KUPIKA KITUMBUA CHENYE MCHANGANYIKO WA UNGA WA NGANO NA UNGA WA MCHELE

 RECIPE SAFI KABISA YA KUPIKA KITAFUNWA AINA YA KITUMBUA KWA MCHANGANYIKO WA UNGA WA MCHELE NA UNGA WA NGANO OOOHH LADHA SAFI SANAA
 
MAHITAJI
250 gram unga wa ngano
120 gram unga wa mchele
1kijiko kidogo cha chai hiliki ya unga au unaweza saga mbegu ikawa chenga chenga
120 gram sukari
120 gram maji ya vugu vugu
nusu kijiko kidogo cha chai amira ya chenga
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
Chukua maji ya vugu vugu changanya na amira ya chenga, sukari pamoja na hiliki.

 
Chukua unga wa ngano na unga wa mchele changanya pamoja

 
Chukua mchanganyiko wa maji mimina kwenye mchanganyiko wa unga wa ngano na mchele na kisha tumia mwiko kukoroga pole pole mapaka ichanganyike vizuri. 

 
Kama mchanganyiko wako ni mwepesi sana basi unaweza tumia mayai au ukaongeza maji au maziwa kiasi hakikisha mchanganyiko huu usiwe mwepesi kabisa na usiwe mzito sana ubora uwe kama unavyoona kwenye picha hapo juu.

 
Chukua kikaango cha vitumbua kisha weka mafuta ya kupikia kijiko kimoja kidogo cha chai.
 

 
Mafuta yakisha pata moto mimina mchanganyiko wako wa unga wa mchele kwenye kikaango.
 

 
Ukishaona rangi ya kahawa kwa chini basi geuza upande wawili na weka mafuta tena. mpatie mlaji chakual kikiwa cha moto atafurahi sana. 

 
 
HUU NI MUONEKANO SAFI KABIS AWA KITUMBUA HIKI CHENYE MCHANGANYIKO WA UNGA WA AINA MBILI SAFI SANA KWA KITAFUNWA CHA NYUMBANI NA RESTAURANT PIA. 
 


Saturday, September 27, 2014

JIFUNZE KUPIKA SUPU YA MAHARAGE AINA YA PINTO PAMOJA NA VIAZI ULAYA

 
JIFUNZE KUPIKA SUPU SAFI SANA YA MCHANGANYIKO WA VIAZI ULAYA NA MAHARAGE AINA YA PINTO
 
MAHITAJI
120 gram pinto beans au maharage ya kitenge
1 kitunguu maji kikubwa chop chop
2 pc za kitunguu swaumu saga
1 kiazi ulaya kikubwa kata kata vipande vidogo
 2 kijiko kikubwa cha chakula tomato paste au nyanya nzima 2
1/4 kijiko kidogo cha chai turmeric powder
1 bay leaf
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
majani ya korienda
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO
 
 
Loweka maharage yako kwa masaa 2 kwenye maji baridi kama utakua unaharaka unaweza kuyapika maharage haya kwenye pressure cooker

 
Baada ya kuyaloweka unaweza kuyapika kwa dakika 20 tu yatakua yameiva na baada ya kuiva hakikisha humwagi maji ya maharage hayo baada ya kuchuja

 
Chukua sufuria na kisha weka katika moto na uweke kijiko kimoja kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia, ikisha pata moto weka kitunguu maji, kitunguu swaumu, turmeric powder, bay leaf na pili pili hoho pamoja na chumvi kanga mapaka vilainike na kutoa harufu safi.

 
Kisha ongezea viazi ulaya pika kwa dakika 4 au mpaka vitakapokua laini. Baada ya kulainika viazi ongeza tomato pest na kumbuka kukoroga ili kila kitu kichanganyike.

 
Chukua yale maji yaliyobaki baada kuchemshwa pamoja na maharage weka kwenye mchanganyiko wako wa viazi na mboga majani unaweza ongeneza maji ya kawaida kidogo ili upate supu. Ikisha chemka tu ongezea maharage na pili pili manga acha ichemke dakika mbili itakua imeiva

 
Unapochemsha maharage hakikisha hayaivi yakapondeka kabisa yawe magumu, mpatie mlaji ikiwa bado ni yamoto na pamba kwa juu na majani ya korienda! Yum!

 
Unaweza maatia mlaji kwenye kikombe na bakupi na ukala pamoja na chapatti au makate na ukafurahia kabisa hasa kwa saubuhi au mchana.
 
 


Monday, September 22, 2014

JIFUNZE KUTENGENEZA SUPU SAFI KABISA YA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI

 
RECIPE SAFI KABISA YA KUPIKA SUPU YENYE MCHANGANYIKO WA LEEKS, BROCCOLI NA ASPARAGUS SAFI SANA KWA AFYA YA MLAJI
 
MAHITAJI
1 kitunguu kikubwa kichop chop
1 leek, isafishe vizuri kasha kata kata
2 viazi vidogo safika vizuri kasha kata kata na maganda yake bila kumenya
1 lita ya maji au unaweza tumia vegetable stock
1 bay leaf
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
500 gram Asparagus osha kisha kata kata 
500 gram broccoli osha katakata
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
Chukua leeks, viazi ulaya, kitunguu maji na bay leaf kisha weka kwenye sufuria lenye maji au vegetable stock na funika chemsha kwa dakika 10.

 
Baada ya dakika 10 kisha weka broccoli na asparagus na uendelee kuchemsha

 
kisha punguza moto uwe wa chini na endelea kuchemsha kwa dakika  10min kumbuka kuweka chumvi na pili pili manga na uonje.

 
Toa kwenye jiko na uache ipoe kiasi baada ya hapo toa bay leaf weka pembeni na mimina mchanganyiko wako kwenye blender na usage.

 
Baada ya kusaga rudishia kwenye sufuria na uendelee kuichemsha kiasi kwa dakika 5 baada ya hapo unaweza mpatia mlaji na kwajuu ukapamba na majani ya giligilani na ukampatia mnywaji akafurahia sana.