CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, April 30, 2010

HII NDIO FRUIT PIE

PIE YA MCHANGANYIKO WA MATUNDA

Hii ni nanasi ya kopo
Hii ni nanasi ya kopo na aple lililokatwa vipande vidogo vidogo changanya kidogo na mkate uponde ponde changanya na hayo matunda


Hii ni sweet pastry mchanganyiko na vipimo angalia jinsi ya kutengeneza biscuti vipimo na mnchanganyiko ni sawa. sukuma upate wembamba wa kawaida
chukua chombo cha kutengenezea pie yako kisha kata umbo la duara

baada ya hapo weka mchanganyiko ule wa matunda navipande vya mkate, unaweza tumia matunda ya aina yeyote ilimradi upate ladha safi unayoipenda wewe

KIsha sukuma tena upate wembamba wa kawaida na kata kamainavyoonekana katika picha na unaweza tumia kisu kama huna kifaa hicho

Kisha chukua vipande hivyo na weka juu ya pie yako

Endelea kuweka juu ya hiyo pie kwa nafasi

Kisha weka kwa upande pia iwe kama dafti

Huu ndio muonekano safi kabisa wa pie inayoonekana kama drafti


Kumbuka pie yetu ia ladha ya tunda apple na nanasi sasa tunaweka syrup ya trawberry ili kuongeza ladhasafi ya matunda mchanganyiko pamoja na rangi nzuri juu ya pie


Usiweke kwenye unga weka kwenye matundu kama inavyoonekana katika picha


KISHA CHOMA KATIKA OVEN KWA DAKIKA 15 TU NA HUU NDIO MUONEKANO WA PIE YAKO SAFI INAUWEZO WA KUKAA KATIKA FRIJI KWA MWEZI MZIMA NA KUMBUKA KUMPATIA MLAJI IKIWA YA BARIDI


JINSI YA KUANDAA CHAKULA CHA MTOTO SIKU YA ALHAMISI KUTOKA KATIKA RATIBA

CHAKULA CHA ASUBUHI

CHAPATI MAJI YA MDALASINI NA VIPANDE VYA APPLE,

250 gram Unga wa ngano
1 yai
50 gram vipange vya apple chemsha viive
5 gram mdalasini
100 gram maziwa ya maji
20 gram mafuta ya mahindi
10 gram baking powder

Jinsi ya kuandaa chapati maji changanya vitu vyote katika bakulikisha piga na mchapo mpaka upate mchanganyiko safi na laini kabisa kama mchanganyiko bado mzito ongeza maji kiasi.

JUISI YA KAROTI NA EMBE

Jinsi ya kuandaa juisi ya Karoti na embe. Menya embe na caroti safi kabisa kisha kata vipande vidogo vidogo iwe rahisi kusagika katika mashine tumia chombo maalumu cha kusagia juice saga embe pamoja na karoti mpaka upate rojo safi kumbuka kuongeza maji kidogo iwapo mchanganyiko wako bado ni mzito kisha hifadhi katika friji bila kuweka sukari ili ikae kwa muda isiharibike kumbuka kuweka sukari wakati wa kunywa.
CHAKULA CHA MCHANA

BATA MZINGA PARACHICHI NA BACON,

Chukua nyama ya bata mzinga au nyama ya kuku au nyama ya bata kisha ipake chumvi kiasi na limao kwa ladha kisha izungushie Bacon mbichi ya ng’ombe kaanga kiasi kisha weka katika oven iweze kukauka tayari kwa kuliwa. Kata vipande vya nyanya na matango pamoja na parachichi ulilomenya safi kabisa kisha kata vipande vidogo vidogo mpatie mtoto ale pia unaweza mpatia mayonaisi tomato sauce ili kulainisha chakula hiki.

GLASI YA MAZIWA

Mpatie mtoto 200 gram glasi ya maziwa.

Kwa mtoto mdogo asieweza kutafuna vizuri pika nyama ya bata pamoja na bacon kisha saga katika mashine weka maziwa na parachichi uwe uji mzito kisha mpatie mtoto itakua chakula safi kabisa.

KITAFUNWA CHA JIONI

POP CORN ZA ASALI NA MCHANGANYIKO WA MATUNDA

Chukua popcon kisha zichanganye na asali na matunda mchanganyiko uliyokata vipande vidogo vidogo iwe rahisi kwa mtoto kula chagua kati ya matunda haya itataegemea na mwanao anapenda matunda yapi Embe, Ndizi, Chungwa, Apple, Papai, Nanasi, Tikiti maji, na mengine mengi. Kisha mpatie mtoto ale atafurahia sana mseto huu.
CHAKULA CHA USIKU

(COTTAGE PIE) NYAMA YA KUSAGA NA VIAZI VYA KUPONDA NA MAZIWA

MAHITAJI

Mchuzi mzito wa nyama ya kusaga ( Bolognese)
200 gram nyama ya kusaga
50 gram kitunguu chopchop
50 gram caroti
150 gram nyanya ya kopo
50 gram pili pili hoho chop chop
50 gram mafuta ya kupikia
5 gram pili pili manga ya unga

Jinsi ya kuandaa
Weka mafuta katika kikaango kisha weka nyama ya kusaga kaanga mpaka iive kabisa kisha weka kitunguu maji, karoti na pili pili hoho kaanga kwa dakika 3 tu kisha weka nyanya ya kopo koroga vizuri kwa dakika 3 zingine weka na chumvi na pili pili manga kwa mbali mchuzi wako utakua umeshaiva.
KISHA ANDAA VIAZI VYA KUSAGA
MAHITAJI

300 gram viazi ulaya
100 gram maziwa ya maji
10 gram chumvi
Chemsha viazi katika maji mpaka viive kabisa kisha vitoe na uviponde ponde kama picha inavyoonyesha hapo chiki kisha weka chumvi na maziwa koroga mpaka upate mchanganyiko laini kabisa.
KIsha chukua bakuli yako safi inayoweza kutumika kupikia kwenye oven weka mchuzi wa nyama ya kusaga nusu ya bakuli kisha weka juu yake hivyo viazi vyakusaga unaweza weka kawaida au ukatumia mfukowa kurembea ( Piping bag) ukapa mapambo mazuri kwa juu kama picha hapo chini kwenye mafunzo jinsi ya kutengeneza cotage pie inavyooonekana viazi vina mvuto. Ukimaliza weka chedah cheese kiasi kwa juu.


Thursday, April 29, 2010

WAJUA KUWAPIKA PRAWNS

BBQ PRWANS WITH GREEN CURRY SAUCE

Mahitaji

½ kilo prawns
50 gram kitunguu swaumu
100 gram maji ya limao
15 gram chumvi
50 gram prawns masala
20 gram pili pili manga

Kumbuka kuwamenya pwans na kuwasfisha vizuri

Chukua vitu vyote hivyo kwa pamoja changanya kisha weka katika friji kwa nusu saa ili viungo viingie safi katika prawns wako.


Hawa ndio prawns baada ya kusafishwa na kuwekewa viungo vyote safi kabisa


Hapa prawns wapo katika pan wanachomwa pia unaweza tumia kikaango au ukawaqchemsha kwa dakika 10 wankua wameshaiva


Huu ni muonekano wa green curry

Mahitaji

2 majani ya mchai chai
50 gram kitungu swaumu
30 gram binzali ya unga
20 gram mdalasini ya unga
20 gram binzali nyembamba ya unga
100 gram tui zito la nazi
50 gram kitunguu maji
40 gram mafuta ya kupikia
200 gram maji safi ya baridi

weka mafuta katika kikaango kisha weka kitunguu maji na kitunguu swaumu kaanga kiasi kisha weka viungo vyote vilivyobakia kaanga kidogo viive kisha weka majani ya mchai chai na maji acha ichemke kwa dakika 15 hadi 20 kisha weka tui la nazi na kama maji yamepungua basi ongezea kiasi acha ichemke tena kiasi kisha




Huundio muonekano wa prawns baada ya kuiva unaweza kuwachoma katika kkaango au ukawachemsha katika maji lakini kumbuka katika maji weka limao na chumvi ili kulinda ladha. Unaweza kula kwa viazi vya kuponda, wali au ugali


Mwisho kabisa kumbuka kumpatia mlaji na kipande cha limao kama urembo juu ya chakula pia inasaidia kuongezaz ladha kwa chakula chochote cha samaki



 

Tuesday, April 27, 2010

BISKUTI YA MUHOGO INAUWEZO WA KUKAA MIEZI 3 BILA KUPOTEZA UBORA

BISKUTI ZA MHOGO

MAHITAJI:
Unga wa mhogo Vikombe 2

Sukari Robo kikombe

Mafuta( Margarine) Nusu kikombe

Yai Moja

Amira Kijiko cha chai 1

Karanga zilizosagwa Moja kikombe.

NJIA YA KUTAYARISHA:
1. Changanya unga wa mhogo, sukari, mafuta na amira pamoja mpaka vyote vichanganyike vizuri

2. Ongeza yai na karanga kisha changanya mpaka mchanyiko umekuwa laini.

3. Sukuma kwenye ubao ulinyunyiziwa unga kisha kata umbile la biskuti kwa kutumia kikombe.

4. Weka matundu ya kutolea hewa kwa uma au kijiti

5. Weka kwenye chombo cha kuokea kilichopakwa mafuta. Oka kwa muda upatao dakika kumi mpaka biskuti imekuwa na rangi ya kahawia hafifu.


Huu ndio muonekano wa biscuti ya unga wa muhogo pia unaweza changanya ladha kwa kuongezea karanga au korosho zilizokaushwa au kukaangwa pia unaweza weka zabibu kavu.

KAMA HUTUMII SUKARI PIA UNAWEZA KUTUMIA ASALI IDADI SANA NA SUKARI  NA BISKUTI ZAKO ZITAKUA NA LADHA SAFI SANA

MFULULIZO WA MAFUNZO YA UNGA WA MUHOGO YANALETWA KWENU NA HAJAT ASIA KAPANDE



JINSI YA KUANDAA CHAKULA CHA MTOTO KUTOKA KATIKA RATIBA

JINSI YA KUANDAA CHAKULA CHA JUMATANO

KIFUNGUA KINYWA ( BREAKFAST)
Yai la kuvuruga na mkate wa ufuta
1 yai
20 gram maziwa ya maji

hilo ndo yai la kuvuruga kisha unaweka juu ya kipande cha mkate

Piga yai pamoja na maziwa kisha kaanga kwenye kikaango vuruga vuruga kumbuka lisiive sana likakauka liive kawaida tu kisha muwekee mtoto juu ya mkate wa ufuta kama hauna basi weka katika kipande cha makte wowote ule uwe mweupe au wa kahawia nitaweka recipe ya kutengeneza mkate hivi karibuni.

Uji wa soya

100 gram maziwa ya maji
300 gram maji
250 gram unga wa soya
50 gram mtindi usio na ladha ya matunda

Changanya unga wa soya na maziwa katika bakuli kisha chukua sufuria weka maji hiyo gram 300 chemsha yakisha chemka weka mchanganyiko wa maziwa na unga wa ulezi koroga mpaka uchemke na kuchanganyika safi kabisa ili uji wako usishike chini na kuungua. Acha uchemke vizuri kisha onja ukipata ladha ya kuiva kwa nafaka utakua tayari.

Toa jikoni weka kaitka bakuli atakalo tumia mtoto kisha changaya mtindi usio na ladha yamatunda pamoja na sukati tayari kwa mtoto kunywa.
CHAKULA CHA MCHANA

SALAD YA KUKU WA KUKAANGA MCHANGANYIKO WA MBOGA NA JUISI YA PASSION

Mahitaji

100 gram nyama yakuku
50 gram caroti
50 gram brocoli au zuchini
50 gram nyanya mbivu
50 gram pili pili hoho

Kata kata nyama ya kuku katika umbo dogo upana wa kidole isiwe na mifupa kisha weka mafuta kiasi katika kikaango weka kitunguu swaumu kidogo na tangawizi kaanga nyama kwa dakika 7 - 10 itakua imeiva kabisa.

Kisha chukua mchanganyiko wa mboga hizo osha vizuri kisha kata katika umbo dogo pia iwe rahisi kwa mtoto kula kisha weka katika kikaango pia zipate moto tu kwa dakika 5 toa changanya na ile nyama ya kuku kisha weka juisi ya limao kiasi na chumvi mpatie mtoto ale. kama mtoto ni mdogo kutafuna shida chukua mchanganyiko wote huo saga katika mashine ya kusagia nyama kisha mpate mtoto.

Juisi ya passion

Tengeneza kama kawaida tu kamua tunda lako safi kisha toa mbegu na uchangaye na maji kiasi kutoa chachu kisha ifadhi katika friji sukari weka wakati mtoto anataka kunywa ili juisi yako isiharibike.
CHAKULA CHA JIONI

MTINDI USIO NA LADHA YAMATUNDA NA MCHANGANYIKO WA MATUNDA

Mahitaji

100 gram mtindi halisi usio na ladha ya matunda
50 gram embe bivu
50 gram papai bivu
50 gram ndizi mbivu
50 gram apple rangi yeyote ile
30 gram karanga au korosho


Katakata matunda katika maumbo madogo kabisa ili mtoto aweze kula kiurahisi kisha changanya matunda pamoja na mtindi juu yake rushia karanga au korosho mpatie mtoto ale.
CHAKULA CHA USIKU
VIPANDE VYA NYAMA YA NG'OMBE NA TAMBI

Mahitaji
150 gram Nyama ya ng'ombe
150 gram tambi
50 gram kitunguu
50 gram karoti
50 gram maharage mabichi
15 gram soya sauce

Kata kata nyama ya ng'ombe vipande vidogo kisha weka mafuta kiasi kwenye kikaango kisha anza kukaanga nyama ya ngombe weka na chumvi kiasi kaanga mpaka ikauke kabisa itakau imeisha iva. Kisha weka mchanganyiko wa mboga majani hizo nazo unakua umekata mikato midogo midogo ili mtoto isimsumbue kula.
Chukua tambi ulizokwisha chemsha changanya katika mchanganyiko huo wenye nyama na mboga mboga kisha pika kwa dakika 3 tu ili vichanganyike vizuri weka na soya sauce kish mpatie mtoto ale kikiwa cha moto.



Tambi na vipande vya nyama muonekano na harufu yake safi itamvutia sana mtoto na atafurahia chakula

ORODHA YA MANUNUZI

Yai, mkate wa ufuta au wowote ule, unga wa soya, maziwa , sukari, mtindi uio na ladha ya matunda, nyama ya kuku, karoti, pilipili hoho, maharage mabichi, tambi, nyama ya ng'ombe, soya sauce, kitunguu maji, embe, papai, ndizi mbivu, apple, karanga na zucchini.





Saturday, April 24, 2010

JINSI YA KUANDAA CHAKULA CHA MTOTO KUTOKA KATIKA RATIBA

JINSI YA KUANDAA CHA CHAKULA CHA MTOTO KWA SIKU YA JUMANNE

KIFUNGUA KINYWA ( BREAKFAST)
Mtindi wa matunda, mkate wa mayai na nafaka za kukaushwa

Mtindi
100 gram Mtindi wa matunda ya ladha yeyote ile inaweza kua strawberry, passion, Embe, Nanasi au ndizi

Makate wa mayai
Chukua mayai 2
vipande 2 vya mkate

Vunja mayai katika sahani ili iwe rahisi kuupaka mayai mkate wako hakikisha vipande vyote viwili vinaenea mayai safi kabisa kisha chukua kikaango weka siagi kidogo kishaa kaanga mkate uwe na rangi kahawia mpatie mtoto ale ikiwa inamoto wa wastani isipoe itapoteza ladha na ni hatari kwa afya ya mtoto.

Nafaka za kukaushwa ( Cerials)
Unaweza mpatia nafaka za kukaushwa mfano Rice crisp, Coco pops, Wheetebix, Con flakes, All brain, Ban flakes na Muesli.

Unaweza chukua gram 100 ya moja wapo ya hizo nafaka pamoja na maziwa baridi 50 gram kisha changanya au unaweza ukachukua aina mbili za nafaka kila moja gram 50 ukazichnganya na maziwa kwahiyo mtoto anapata ladha ya nafaka aina mbili mfani corn flakes na coco pops.

CHAKULA CHA MCHANA
Chapati ya nyama ya kusaga, na chips au viazi vya kusaga na juisi ya nanasi

Chapati ya nyama ya kusaga
Chukua nyama ya kusaga 150 gram, kitunguu 30 gram , pili pili hoho 30 gram chumvi 5 gram na soya sauce 10 gram saga tena katika mashine ya kusagia nyama kisha changanya na yai moja.

Tengeneza umbo la duara safi kama chapati kisha choma katika kikaango chenye mafuta kiasi mpka iive mtoto anaweza kula na viazi vya kukaanga ( chips)


Hii ndio chapati ya nyama ya kusaga

Kama mtoto ni mdogo chemsha viazi na chumvi kisha viponde na maziwa kiasi mpatie na hiyo nyama atafurahia chakula.

Juisi ya nananasi
Menya nanasi kisha lisage na tangawizi kiasi kweye mashine ya kusagia chakula ( Blender) iweke katika friji bila sukari ili isiharibike weka sukari wakati wa kunya mtoto. Tangawizi inaongeza hamu ya kula.

CHAKULA CHA JIONI
Salad ya kuku wa kuchemsha, mtindi na matunda mchanganyiko

Chukua nyama ya kuku isiyo na mifupa 100 gram ichemshe na chumvi kiasi ikiisha iva iache ipoe. Kisha chukua mtindi usio na ladha ya matunda changanya na kuku pamona na matunda uliokata katika umbo dogo ili mtoto aweze kula.

CHAKULA CHA USIKU
Keki ya spinach, viazi vitamu na juisi ya maembe

200 gram Spinach mbichi
100 gram Maziwa
2 mayai
50 gram kitunguu

Chukua na kitunguu saga katika mashine ya kusagia nyama kisha changanya chumvi na yai na maziwa. Baada ya hapo chukua filo pastry itandaze katika mweza kisha juu yake weka mchanganyiko mzito wa spinach kisha funika na iweke kwenye oven oka kwa dakika 15 tu itakua tayari na rangi safi ya kahawia.


Hii ndio spinach cake filo pastry ipo kama manda inapatikana maduka ya chakula popote duniani na sio ghali
Viazi vitamu
Viazi vitamu unachemsha tu kawaida na chumvi

Juisi ya maembe
Menya embe 1 kisha unasaga katika mashine yakusagia chakula ( Blender) weka katangawizi kidogo kumuongezea mtoto hamu ya kula usiweke nyingi itamuwasha mtoto na hata furahia chakula.

ORODHA KWAJILI YA MANUNUZI

Mtindi wenye ladha ya tunda, Mtindi usio na ladha ya tunda, mkate, Yai, Nyama ya ng'ombe ya kusaga, Kitunguu, Viazi vitamu, Spinach, Maziwa, Embe, Papai, Tikiti maji, Filopastry, Nafaka za kukaushwa, Kitunguu, viazi ulaya, Nyma ya kuku na nanasi.


Friday, April 23, 2010

UNAJUA WASIFU WA UNGA WA MUHOGO

UNGA WA MUHOGO UNAWEZA UKABADILISHA KABISA LADHA NA AINA YA MAPISHI NYUMBANI KWAKO KWA UPANDE WA VITAFUNWA KWAJILI YA CHAI ASUBUHI AU CHAI YA JIONI HATA KATIKA SHEREHE NDOGO ZA MAJUMBANI KWETU KILA SIKU NITAKUA NAWAWEKEA RECIPE YA CHAKULA KIMOJA KIMOJA

RECIPE HIZI ZA UNGA WA MIHOGO ZINALETWA KWENU NA MWALIMU WANGU ALIYENIFUNDISHA JINSI YA KUANDAA CHAKULA TOKA NIKIWA MDOGO KABISA MPAKA LEO NIMEKUA CHEF KAMILI YEYE NI FOOD AND NUTRITION SPECIALIST MAMA YANGU MZAZI ASIA KAPANDE



Mama yangu mzazi Hajati Asia Kapande akiwa Egypt anaelezea bidhaa na matumizi bora ya via zilishe


KEKI YA MIHOGO
MAHITAJI:
Unga wa mhogo Vikombe vitatu

Sukari ¾ kikombe

Mafuta (Margarine) Kikombe kimoja

Amira ya unga Vijiko vya chai vitatu

Mayai Matatu.


NJIA YA KUTAYARISHA

1. Koroga sukari na mafuta pamoja mpaka mchanganyiko uwe laini na mwepesi

2. Piga mayai mpaka yawe mepesi.

3. Chekecha unga na amira pamoja

4. Ongeza unga na mayai taratibu kwenye mchanganyiko wa mafuta na sukari.

5. Mchanganyiko ukiwa mzito ongeza maziwa kidogo au maji. Endelea kuongeza unga na mayai kidogo kidogo mpaka unga wote umekwisha.

6. Ongeza chenga za ganda la limao kidogo ( linaongeza ladha).

7. Paka mafuta chombo cha kuokea kisha weka mchanganyiko wa keki kwa ujazo wa ⅔

8. Oka kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda upatao dk. 20 au mpaka keki imeiva vizuri.


Wednesday, April 21, 2010

MAFUNZO YA KUANDAA CHAKULA CHA WATOTO TOKA KATIKA RATIBA

JINSI YA KUAANDAA CHAKULA CHA JUMATATU KATIKA RATIBA

KIFUNGUA KINYWA ( BREAKFAST)


CHAPATI MAJI NA JUISI YA CHUNGWA

250 gram Unga wa ngano
1 yai
100 gram maziwa ya maji
20 gram mafuta ya mahindi
10 gram baking powder

Jinsi ya kuandaa chapati maji changanya vitu vyote katika bakulikisha piga na mchapo mpaka upate mchanganyiko safi na laini kabisa kama mchanganyiko bado mzito ongeza maji kiasi.

Jinsi ya kuandaa juisi ya chungwa. Menya chunga safi kabisa ili kundoa uchungu wa gesi iliyopo katika maganda. kisha tumia chombo maalumu cha kukamulia juice kamua kisha hifadhi katika friji bila kuweka sukari ili ikae kwa muda isiharibike kumbuka kuweka sukari wakati wa kunywa.

UJI ULEZI NA MTINDI

200 gram unga wa ulezi
100 gram maziwa ya maji
350 gram maji
100 gram mtindi usio na ladha ya matunda

Changanya unga wa ulezi na maziwa katika bakuli kisha chukua sufuria weka maji hiyo gram 300 chemsha yakisha chemka weka mchanganyiko wa maziwa na unga wa ulezi koroga mpaka uchemke na kuchanganyika safi kabisa ili uji wako usishike chini na kuungua. Acha uchemke vizuri kisha onja ukipata ladha ya kuiva kwa nafaka utakua tayari.
Toa jikoni weka kaitka bakuli atakalo tumia mtoto kisha changaya mtindi usio na ladha yamatunda pamoja na sukati tayari kwa mtoto kunywa.

 CHAKULA CHA MCHANA


 GLASI YA MAZIWA NA MKATE WA NYAMA ZA KUSINDIKA

Mpatie mtoto 200 gram ya maziwa swa na glasi moja ya uvugu vugu au ya baridi lakini kumbuka yawe yamechemshwa vizuri na yakapoa kwajili ya usalama.

Kisha chukua vipande viwili vya mkate paka siagi au mayonaisi. Kisha chukua beef salami na beef backon weka kati kati pamoja na slice ya nyanya na tango mbichi mpatie mtoto ale.

 KITAFUNWA CHA JIONI


 SAHANI YA MCHANGANYIKO WA MBOGA MBICHI

chukua caroti, tango, pili pili hoho  nyekundu na ya kijani zote mbichi na zuchini ichemshe kidogo kisha weka mtindi wenye ladha ya matunda kwajili ya kulia hizo mboga.



Huu ndio muonekano wa sahani ya mchanganyiko wa mboga kama mtoto ni mdogo sana zisage kwenye mashine ya kusagia nyama kisha utapata mchanganyiko laini mpatie mtoto asieweza kutafuna hizo mboga mbichi.

 CHAKULA CHA USIKU


 SUPU YA UYOGA, KUKU MAZIWA wa MIHOGO NA NJEGERE


Mahitaji ya Supu ya uyoga

300gram Uyoga fresh au wa kopo
50 gram kitunguu maji
10 gram kitunguu swaumu
10 gram tangawizi
50 gram leeks
100 gram viazi ulaya
100 gram maziwa fresh
50 gram mafuta ya kupikia
300 gram maji

Kaanga katika mafuta ya kupikia vitunguu maji na vitunguu swaumu pamoja na tangawizi. kisah weka viazi ulaya, leeks na uyoga kaanga tena kiasi kisha weka maziwa na maji acha ichemke mpaka viazi viive kisha toa na saga kwenye blenda rudisha jikoni kama nzito san ongeza maziwa au maji kiasi kumbuka kuweka chumvi kkulingana na ladha.

Mahitaji ya kuku wa maziwa, muhogo na njegere

200 gram nyama ya kuku isiyo na mifupa
100 gram njegere
200 gram maziwa
150 mihogo iliyochemshwa kwanza
300 gram maji



Hii ndio machine ya kusagia nyama utakayoitumia kwajili ya kusagia chakula mbali mbali.

Chemsha vyote kwa pamoja kuku na njegere mbichi pamoja na muhogo uliokwisha chemshwa kwanza mpaka ikaribie kukauka mchuzi  kisha toa chuja mchuzi weka pembeni.

Chukua mchanganyiko wa njegere, kuku na muhogo tumia machine ya kusagia nyama weka saga upate rojo zito kisha rudisha katika sufuri changanya na ule mchuzi uliochuja ongeza chumvi kulingana na ladha mpe mtoto ale chakula kikiwa cha moto.

Kama hauna mashine ya kusagia nyama tumia mwiko kuponda itakua safi kabisa kisha unachangaya na ule mchuzi uliochuja.

Kwa mtoto mkubwa usisage baada ya kuchemsha ikaiva oneza chumvi kisha mpakulie ale chakula chamoto atafurahia sana mchanganyiko wa ladha ya chakula hiki.

ORODHA KWAJILI YA MANUNUZI SIKU YA JUMATATU

Uyoga wa kopo au fresh, Mihogo mibichi, pili pili hoho, tangawizi, Unga wa ngano, Mayai, Maziwa, Sukari, Chumvi, Njegere, Nyama ya kuku, Tango, Zucchini, Mtindi usio na ladha ya matunda, Mtindi wa ladha ya matunda, Baking powder, Viazi ulaya, Mafuta ya mahindi na leeks.

Vitu hivi vyote sio vingi na unaweza kuvitumia siku inayofuata maana menu yetu inauwiano safi kabisa vitu vingi vinatumika baribu kila siku na manunuzi yake sio ghali kabisa mpe mwanao raha kwa kula chakula safi na salama.

MAFUNZO YA JNNE YANAKUJA MUDA SI MREFU KAA TAYARI.


Tuesday, April 20, 2010

HII NDIO SHEPHED PIE

KIHISTORIA CHAKULA HIKI KINALIWA SANA NA WAINGEREZA

MAHITAJI

Mchuzi mzito wa nyama ya kusaga ( Bolognese)

200 gram nyama ya kusaga
50 gram kitunguu chopchop
50 gram caroti
150 gram nyanya ya kopo
50 gram pili pili hoho chop chop
50 gram mafuta ya kupikia
5 gram pili pili manga ya unga

Jinsi ya kuandaa

Weka mafuta katika kikaango kisha weka nyama ya kusaga kaanga mpaka iive kabisa kisha weka kitunguu maji, karoti na pili pili hoho kaanga kwa dakika 3 tu kisha weka nyanya ya kopo koroga vizuri kwa dakika 3 zingine weka na chumvi na pili pili manga kwa mbali mchuzi wako utakua umeshaiva.

Huu ndio mchuzi wa nyama ya kusaga

KISHA ANDAA VIAZI VYA KUSAGA

MAHITAJI
300 gram viazi ulaya
100 gram maziwa ya maji
10 gram chumvi

Chemsha viazi katika maji mpaka viive kabisa kisha vitoe na uviponde ponde kama picha inavyoonyesha hapo chiki kisha weka chumvi na maziwa koroga mpaka upate mchanganyiko laini kabisa. 



Hii ndio mush potato au viazi ulaya vya kusaga

KIsha chukua bakuli yako safi inayoweza kutumika kupikia kwenye oven weka mchuzi wa nyama ya kusaga nusu ya bakuli kisha weka juu yake hivyo viazi vyakusaga unaweza weka kawaida au ukatumia mfukowa kurembea ( Piping bag) ukapa mapambo mazuri kwa juu kama picha hapo chini inavyooonekana viazi vina mvuto. Ukimaliza weka chedah cheese kiasi kwa juu.



hii ndio piping bag unaweka viazvi vyako vya kuponda ndani yake kisha unapambia juu ya huo mchuzi wa nyama ya kusaga ukimaliza unaweka katika oven kwa dakika chache tu upate rangi nzuri ya kahawia na cheese iweze kuyeyuka.



Ni nyama ng'ombe yakusaga na viazi vya kuponda safi sana kwa mtoto pia mtu mzima



JE UNAIJUA POTATO ROSTII

HII NDIO POTATO ROSTII NI CHAKULA MAARUFU SANA KWA WASWISS

MAHITAJI

4 Viazi vikubwa
50 gram siagi
10 gram chumvi
5 gram pilipili manga ya unga

Chukua viazi vimenye maganda kisha viweke katika maji baridi na vichemshe kwa dakika 15 - 20 kisha vitoe vitakua vimeiva ingawa vitakua vigumu kumbuka visiwe laini au visiive sana viweke pembeni vipoe.






Kisha chukua kwaruzo la caroti ( greater) vikwaruze viazi upate vipande vidogovidogo safi na vigumu



baada ya hapo changanya chumvi na pili pili manga



kisha weka siagi katika kikaango chenye leya nyeusi inayosaidia chakula kisiungue na kunga'nga'nia katika kikaango kinaitwa ( non stick pan) weka ujazo wa kikaango kidogo au kama ni kwa chakula cha watoto tumia chombo cha kukatia umbo la aina yeyote ile utakayopenda kisha weka viazi ndani ya umbo hilo kaanga upande wa kwanza kisha kaanga upande wa pili kuwe na rangi ya kahawia safi.





Rostii potato itakua tayari na utafurahia chakula chako pia unaweza kwaruza viazi hivyo na ukahifadhi katika freezer hata kwa miezi miwili na visiharibike kumbuka uwe tu umeviweka katika saizi unayopenda kupika kwa baadae usiviache vitawanyike lazima uwe umevitengeneza katika umbo.

Kama utakua umevitengeneza katika umbo lolote lile na ukaviweka katika freezer ukivitoa unaweza kuvipika kwa mitindo tofauti kabisa unaweza ukavioka katika oven au uka vikaanga kwenye mafuta mengi maana vinakua vimeshikana.

FURAHIA CHAKULA HIKI NA FAMILIA YAKO.


FAMILIA YAKO WANAPENDA KEBAB? WATENGEZEE HII WATAFURAHIA SANA

CHAKULA HIKI NI KIZURI SANA NA ANAWEZA KULA MTOTO KUANZIA MWAKA MMOJA MPAKA MTU MZIMA NI LAINI, SLAMA NA TAMU SANA.

MAHITAJI

1 kilo ya nyama ya kusaga
100 grama kitunguu chop chop
100 grama pili pili hoho chop chop
50 grama tomato pest
15 gram chumvi
10 gram pili pili manga
2 yai
100 gram unga mkavu wa mikate (bread crumbs)
50 gram soya sauce
15 gram tabasco sauce
2 majani ya korienda au parsley
50 gram kitunguu swaumu na tangawizi iliyosagwa


JINSI YA KUANDAA

Chukua nyama ya kusaga changanya na vitu vyote hivyo kwa mara moja



Kisha tengeneza miviringo ya nyama kama inavyoonekana katika picha kisha chukua miti ya mbao ya mishikaki iwe mirefu



Chukua mviringo mmoja wa nyama kisha uzungushie kwenye kijiti cha mshikaki kandamiza vizuri na tengeneza umbo refu zuri


kandamiza pole pole ili nyama ishike katika mti wa mshikaki



Kisha zungushia mti huo wa mshikaki aluminium foil ili isungue kwenye oven kisha paka mafuta kidogo kebab zako na weka katika oven choma kwa dakika 15 hadi 20 itakua imeiva.

Chakula hiki ni safi na salama hakina mafita mengi na unaweza kula na viazi aina tofauti nitakuletea recipe soon na au uanweza kula na ugali na wali pia.

KAMA HAUNA OVEN BASI FATA MFULULIZO HUO JISNI YA KUTENGENEZA KISHA TENGENEZA UMBO LOLOTE ZURI UNALOPENDA USITUMIE TENA MTI WA MSHIKAKI PIAGA MAYAI PEMBENI CHOVYA HIYO NYAMA KWENYE MAYAI KISHA KAANGA KWENYE MAFUTA YALIOCHEMKA VIZURI SIO SAANA MAANA ITABABUKA NA HAITAIVA NDANI YAWE NA MOTO WA WASTANI ILI IIVE POLE POLE KAMA UNAKAANGA MAANDAZI UTAPATA KABAB SAFI KABISA.

Friday, April 16, 2010

JE HUPENDI KULA MBOGA MAJANI? HII UTAIPENDA SANA TU!!


HATA KAMA WEWE SIO VEGETARIAN MBOGA MAJANI NI MUHIMU SANA KWA AFYA YAKO NA HASA ZIKIANDALIWA VIZURI.

Mahitaji

1 nyanya frsh ya kuiva safi
1 kitunguu
1 zucchini au baby marrow
1 pili pili hoho
1 kiazi kitamu
1 carrot
150 gram njegere mbichi
100 grm mtindi halisi usio na ladha ya matunda
150 gram Maharage mabichi

Jinsi ya kuandaa

1- Chemsha njegere kisja maharage mabichi kwa dakika 4 katika maji na chumvi yaliyochemka hasa ziive safi zisiwe na rangi ya njao zibaki na rangi znuri ya kijani
2- Chemsha kiazi kiive vizzuri ndani ya maji na chumvi
3 - Kata nusu kitungu, slice ya karoti, Nyanya, zucchini na pili pili hoho chona kwenye kikaango cheney mafuta kiasi kwa dakika 10 tu ziive ziwe na rangi ya kahawia wastani zisiungue.

kisha panga kama inavyoonekana katka picha usisahau mtindi weka kwenye bakuli dogo kwa pembeni na kiazi kikate slice na panga saafi njegere weka katika bakuli pia.

CHAKULA HIKI NI KIZURI NA UTAKUA UMEUWEKA MWILI AKO KATIKA HALI NZURI KIAFYA KWA KUZINGATI AMAPISHI BORA YA MBOGA


Wednesday, April 14, 2010

CHICKEN STIR FRIED RICE

WALI HUU NI MTAMU SANA TENGENEZA FAMILIA YAKO IFURAHI WEEKEND HII

MAHITAJI

1 kilo wali uliopikwa
150 gram kitunguu
150 gram karoti
250 gram kabechi
150 gram pili pili hoho
5 mayai mabichi
150 gram soya sauce
1 kuku mzima au kifua chakuku 500 gram
160 gram mafuta ua kupikia

Pika kwanza wali wako na usiweke chumvi maana wakati unaukaanga utaweka soya sauce na inachumvi kweli.


Kata mchanganyiko wa mboga kama inavyoonekana katika picha



Kisha chukua kuku mzima mtoe nyama yote na mifupa weka pembeni



Huu ni muonekano wa kuku baada ya kutenganishwa na mifupa kisha ikate nyama hii katika vipande vidogo vidogo kwa urefu



Huu ni muonekano wa nyama ya kuku ikiwa katika mkato wa urefu tayari kwa kupikwa




Weka mafuta kaika kikaango yakishapata moto weka mboga zote kwa wakati momoja na uendelee kuzikaanga


Hii ni chupa ya light soya sauce ni nzuri na mtu yeyote yule anaweza kula na akafurahia chakula kilichochawnganywa pia inapatikana maduka ya chakula yote nyumbani tanznaia na bei yake ni sh 800 tu.



Kumbuka mboga zisiive kabisa ziive nusu tu bado ziwe ngumu kisha kuku kaanga mpaka aive haichukui muda kwakua tayari umekata mikato midogo ikishaiva kuku weka mayai kaanga nayo yasiive kabisa ila yawe magumu kiasi yasikauke kisha weka wali uliokwaisha iva kaanga kisha weka soya sauce changanya mpaka wali wote uwe na rangi ya soya sauce.




Huu ndio muonekano wa wali wako ukiwa na rangi safi kabisa chukua nyanya zilizokatwa kwa urefu pamboa chakua chako kitamu kabisa




Mwisho kabisa juu unaweza pamba na majani yeyote yale ya kijani mi nimetumia maganda ya tango unamenya kisha unakata katika umbo hilo dogo chakula hiki nirahisi sana kuandaa pia ni nafuu na unaweza lisha familia ya watu 10 na wakashiba.

WALI HUU HAULINI NA MCHUZI UNAJITOSHELEZA KABISA NI LAINI WEEKEND NJEMA