CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Wednesday, June 30, 2010

CHOCOLATE SALAMI NI SAFI SANA

CHOCOLATE HUPENDWA SANA NA WATOTO PAMOJA NA WATU WAZIMA WASWIS WANAKULA SANA ILI KUJIBURUDISHA, KUCHANGAMSHA AKILI NA KUONGEZA NGUVU MWILINI

700 gram bittersweet chocolate au ( Chocolate bloc)
4 kijiko cha chakula siagi isiyo na chumvi
2 kijiko cha chakula cocoa powder
60 gram maji ya moto
150 gram korosho zilizo okwa katika oven
150 gram karanga zilizo okwa katika oven
1 box la biskuti ziponde ponde ziwe vipange kama ukubwa wa korosho
4 yai kubwa tumia ute wa njano tu
240 gram sukari ya unga
1kijiko cha chakula champagne au apple juice
1 chungwa kwaruza upate chenga chenga za maganda ya juu


JINSI YA KUANDAA

Fuata maelekezo na picha chini



Katika picha huo ni muonekano wa vitu vyote unavyotakiw akua navyo kabla ya kaunza kutengeneza chocolate salami yako.

Chukua maji moto changanya na cocoa powder pamoja na sukari

kisha chukua ute wa njao wa mayai piga kwa mchapo au mashine kama picha inavyoonyesha chini


Huu ni muonekano wa ute wa njano wa mayai weka na chenga chenga za chungwa ulizokwaruza pamoja na kijiko cha champagne au apple juice


Kisha chukua chocolate yako nyeusi yeyusha katika surufia kwa moto mdogo sana pamoja an siagi mpaka iyeyuke kabisa


Kisha changanya mchanganyiko wako wa siagi na chocolate pamoja na mchanganyiko wa kokoa kisha chukua na mchanganyiko wa mayai changanya pole pole mpaka ichanganyike vizuri


Mwisho chukua mchanganyiko wa karanga, korosho na biscuit chnagnya pia katika mchanganyiko wako wenye chocolate tayari



Kisha unaweza tumia njia mbili, yakwanza mwaga sukari ya unga juu ya meza kisha mwagia mchanganyiko wako wenye karanga na chocolate juu yake na viringisha juu ya hiyo sukari juu ya meza upate mviringo mzuri na kisha weka katika freeza ili ugande kwa masaa 2 baada ya hapo inakua tayari kuliwa na unaweza kukata katiaka mtindo tofauti.

Njia ya pili chukua aluminium foil kisha mwagia kuu yake mchanganyiko wako na kisha vingirisha kwa umbo la duara kwa upana wowote unaopenda wewe kisha weka kwenye freeza kwa masaa mawili itaganda safi nakua tayari kwa kuliwa.



Baada ya kutoa katika freeza unaweza kukata kwa umbo lolote unalopenda wewe ingawa inapendeza zaidi ukikata kwa umbo la duara kama inavyoonekana kwenye picha.

Wapatie familia yako kwa chai ya saa 4 au chai ya saa 10 jioni kwa family na wageni pia unaweza mfungashia mtoto akale shule.


UNAJUA JINSI YA KUTENGENEZA BURGER

WATOTO WENGI SANA WANAPENDA KULA BURGER HATA WATUWAZIMA PIA HUPENDA KULA SIKU MOJA KATIKA CHAKULA CHA MCHANA WATENGENEZEE
FAMILIA WAFURAHI

Kwaujumla napenda sana burger ya kutengeneza nyumbani, na ninapenda kutengeneza mwenyewe au mke wangu lengo ni kuhakikisha viungo na mchanganyikowote unakua sawa. Kwakutmia recipe hii unaweza kutengeneza 8 -10 hamburgers Inategemea utaweka upana gani wa nyama yako.Baada ya kuandaa unaweza kuhifadhi mchanganyiko huo wa nyama kwenye freezer kwa matumizi ya baadae.
MAHITAJI

 1 kg nyama ya kusaga safi 
 240 gram kitunguu kilichokatwa katwa vipande vidogo 
 60 gram bread crumbs ( Unga wa mikate)
 1 kijiko cha chakula Worcestershire sauce
 2 cloves of garlic, peeled and minced
50 gram kitunguu swaumu
 5 gram chumvi
 5 gram pili pili manga
1 lettuce
1 kitunguu
2 nyanya fresh

Katika bakuli kubwa changanya nyama pamoja na kitunguu, bread crumbs, Worcestershire sauce na kitunguu swaumu kisha weka . Kisha changanya safi na gawa katika mafungu 8 au 10 kulingana na ukubwa unaopenda wewe.
JINSI YA KUPIKA

Unaweza ukakaanga kwenye kikaango au ukapika kwa moto wa 160 degrees katika oven. Chukua mkate wa burger kisha kata katika pande mbili kisha paka mayonnaise na tonato  ketchup kwenye mkate upande wa chini, ongezea lettuce, slice kitunguu na nyanya fresh na slice ya tango la kopo. Nyunyizia chumvi kidogo mpatie mlaji ikiwa yamoto





Tuesday, June 29, 2010

SPAGHETI NA NYAMA YA KUSAGA MHHHH YAM YAM!!!!

SOON UTAPATA RECIPE SAFI YA NYAMA YA KUSAGA NA SPAGHETI SAFI KABISA KAA TAYARI

MAHITAJI


1 Kilo nyama ya ng'ombe ya kusaga
2 nyanya kubwa ya kuiva katakata vipande vidogo

1kitunguu kikubwa kata kata vipande vidogo vidogo
1karoti kata kata vipande vidogo vidogo
50 gram kitunguu swaumu
1 leeks kata vipande vidogo vidogo

1 kijiko kikubwa cha chakula unga wa ngano
2 mafuta ya kupikia kijiko kikubwa cha chakula
5 gram chumvi na pili pili manga

1 kopo la nyanya ya kopo


Huu ni muonekano wa kitunguu, leeks na karoti katika mkato wa maumbo madogo


Pasha kikaango au sufuria tayari ukiwa umeshaweka mafuta. Kisha ongeza kitunguu, kitunguu swaumu, karoti na leeks kaanga mapaka zilainike kiasi.

Kisha weka pili pili manga, chumvi na nyama ya ng'ombe iliyosagwa kaanga katika moto mkali zaidi na kumbuka kukoroga koroga marakwa mara ili nyama isishikane na kujibumba madongo madonge hakikisha unakaanga mpaka inaiva.

Kisha weka nyanya ya kopo na kijiko cha unga wa ngano kaanga na koroga ichanganyike vizuri. Mwisho weka nyanya fresh endelea kukoroga. Punguza moto na funika sufuri, pika kwa dakika 10 ukiwa unachungulia na unakoroga pole pole.


Unaweza kupakua na kumpa mlaji spagheti hii kwa staili mbili toafauti moja ni hii chukua spagheti zako ulizochemsha kisha zichanganye katka sufuri uliyopikia nyama ya kusaga kisha pakua weka kwenye sahani tayari kwa kumpatia mlaji ikiwa tayari umeshachanganya vizuri kumbuka kupamba kwajuu kuongeza muonekano thabiti na chakula kivutie.



Staili ya pili ni hii hapa chukua spagheti ulizo chemsha zikaiva vizuri kisha weka katika sahani halafu chukua nyama ya kusaga kisha weka juu ya spagheti hakikisha unaweka staili kama ya mlima na juu ya nyama ya kusaga iliyoiva weka jani la giligilani au parsley au mint au basil ilimradi uwe na mchanganyiko wa rangi nzuri na chakula chako kivutie.

Wednesday, June 23, 2010

INSI YA KUPIKA MAPISHI MBALI MBALI YA WALI

NIMEOMBWA NA WADAU WENGI SANA KURUDIA MAFUNZO HAYA HASA KWA WALE NDUGU ZANGU MLIOKO UGHAIBUNI MCHELE ASILIMIA 90% HAUNA LADHA NA HARUFU NZURI KAMA TULIOUZOEA NYUMBANI CHUKUA UJANJA HUU ILI UFANYE WALI WAKO UWE WA KUNUKIA NA LADHA SAFI KABISA

MAHITAJI
720gram caroti iliyokwaruzwa
480gram Basmati rice ( mchele wa pishori) iliyopikwa
2 vitunguu vikubwa vikate katika size ndogo
1 Nyanya moja kubwa ikate katika size ndogo
1 fungu la majani ya girigilani
2 kijiko kikubwa cha chakula karanga zilizokaangwa kwajili ya kupambia
3 kijiko kidogo cha chai cha mafuta ya kula
Chumvi weka kulingana na ladha na mahitaji yako



Huu ni muonekano wa caroti iliyokwaruzwa safi kabisa pamoja na nyanya na kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo rahisi kwa kuiva


Huu ni muonekano wa wali wa maji ulioiva


Mchanganyiko wa karoti, kitunguu na nyanya katika kikaango chenye mafuta na moto mkali pika kwa dakika 5 tu usiache ziive sana kisha changanya wali wako ambao umeshaiva.



Huu ni wali ulioiva na ukachanyanywa na mchanyiko wako wa caroti, utapata harufu nzuri na ladha nzuri sana kwa kupata harufu na ladha nzuri zaidi unaweza ongezea pilipili hoho au girigilani ( Corriender leaves).


Jinsi ya kuandaa
Pasha moto sufuria lako au kikaango weka mafuta kisha weka vitunguu kaanga kiasi tu visiungue au kua na rangi ya kahawia vilainike tu inatosha.

kisha weka nyanya zikaange mpaka zichanganyike kabisa zitengeneze rojo rojo

Kisha weka caroti zilizokwaruzwa katika mchanganyiko wako kaanga na zichanganyike vizuri
Kisha weka wali wako wa basmati ulioiva katika mchanganyiko wako wa karoti changanya vizuri kisha mimina majani ya girigilani na changanya pole pole mwisho kabisa weka karanga zako ambazo zimekaangwa vizuri kama unatumia.
Mapishi haya unaweza tumia mchele wa aina yeyote ile sio lazima mchele wa basmati



JINSI YAKUTENGENEZA SPINACH AND RICOTTA CANNELLONI

CHAKUL AHIKI KINASAIDIA SANA KUONGEZA MADINI JOTO MWILINI

Mahitaji kwajili ya watu 4


600 gram ricotta cheese
250 gram spinach iliyochemshwa kidogo na kukatwa katwa
20 gram parmesan pamesan cheese
5 gram kila moja chumvi na pili pili manga

6 fresh lasagne sheets 
240 gram mozzarella cheese
25 gram parmesan cheese
1 fungu jani ya basil


 


Huu ni muonekano wa majani ya spinach

huu ni muonekano wa pasta aina ya lasagne zinauzwa katika maduka ya chakula ni rahisi kuzipata na sio ghalia kabisa uliza tu lasagne ( matamshi sema lazania) zipo katika muonekano kama karatasi


Huu ni muonekano wa cheese inaitwa ricotta ikiwa imekwaruzwa vizuri


Katakata na chemsha kiasi spinach katika vipande vidogo kisha changanya ricotta cheese, spinach, mozarella cheese, majani ya basil, parmesan, chumvi na pili pilimanga kisha weka katika mashine ya kusagia nyama saga usitu,ie blenda itakua maji na inatakiwa iwe nzito kabisa kama inavyoonekana kwenye picha.

Kisha chukua lasagne ziweke kwenye maji kwa muda wa saa nzima zilowane zikishalowana zinakua laini toa weka juu ya meza panga kama inavyoonekan katika picha chota mchanganyiko wako wa spinach weka juu na kisha zungurusha na tengeneza mduara.

 
hapa ni baada ya kuzungurusha na muonekano unakua kama huu tayari kwa kuwekwa kwenye oven ili kuokwa tayari kwa matumizi ya chakula



Washa oven kwa nyuzi joto 190°C kumbuka kuweka mafuta kiasi katika tray yako ya kuokea  ili zisishike chini wakati zikiwa kwenye oven. choma katika oven kwa dakika 15 mpaka 20 kisha mwagia juu mchuzi mzito wa nyanya na cheese tena kiasi acha mpaka cheese iyeyuke na kuwa na rangi safi ya kahawia toa na mpatie mlaji ikiwa ya moto.

CHAKULA HIKI NI SAFI SANA KWA KUONGEZA MADINI JOTO KWAKUA KINAMCHANGANYIKO WA AINA TATU ZA CHEESE NA HASA WANAUME UKILA CHAKULA HIKI UNARUDISHA NGUVU SAFI KWA MUDA MFUPI TU HII ITAKUJENGA KUA JASIRI WAKATI WOTE KAM UMEPOTEZA NGUVU KWANI CHAKULA HIKI KINAVIRUTUBISHO SANA NA MAJIBU UTAYAONA BAADA YA MASAA MAWILI TU BAADA YA KULA.


Monday, June 21, 2010

WAPENZI WA SPAGHETI, NYAMA YA NG'OMBE NA SAUSAGE KAAENI TAYARI KWA RECIPE

CHAKULA HIKI NI KIZURI SANA KWA WAPENZI WA SOSEJI NA NYAMA PIA

MAHITAJI

5 soseji zilizoiva tayari
1 kilo fillet ya nyama ya ng'ombe
1 fungu la majani ya korriender
 200 gram uyoga wakopo au fresh sawa tu
100 gram karoti
100 gram pili pili hoho
500 gram za nyanya pika mchuzi wa nyanya saafi mzito kisha weka asali ya nyuki vijiko viwili  cha chakula pamoja na limao 1 kamulia na soya sosi kijiko 1 cha chakula.


Huu ni muonekano wa soseji iliyoivwa na ikakatwa upande wa kushoto, katikati ni nyama ya ngombe iliyochemshwa ikaiva nayo imekatwa nyembembea kwa urefu kama inavyoonekana katika picha na mwisho upande wa kulia ni mkati mwembamba wa karoti, pilipili hoho na uyoga wa kopo.


Huu ni muonekano wa paketi 2 spagheti zilizo chemshwa tayari kwa kuchanganywa na nyama


Huu ni muonekano safi wa mchuzi mzito uliochanganywa na soya sosi, limao na asali


Chukua  mchanganyiko wote wa nyama, soseji na uyoga ulio na mboga kisha kaanga kwenye kikaango pamoja na majani ya korienda ( Giligilani) kwa dakika 2 tu


KIsha weka spagheti iliyochemshwa ndani ya mchanganyiko wa nyama kaanga kwa dakika 1 tu kisha mwagia ndani mchuzi wa nyanya saafi na endelea kuchanganya mpaka mchanganyiko wako wote uwe na mchuzi na unaladha safi ya mchuzi wa nyanya.


Kisha pakua weka katika sahani kwa mtindo wa mlima kama unavyoona kwenye picha kisha mwagia tena majani kisai ya korienda kwa juu ya chakula hiki. Unaweza kula na cheese kwa juu pia inaongeza ladha safi ya chakula choko. Chakula hiki kinauwezo wa kuliwa na watu wa 5 na wakashiba na kufurahi kabisa.

FURAHI ANA FAMILIA YAKO KWA CHAKULA HIKI SAFI



JINSI YA KUANDAA CHICKEN TANDOORI

SAMAHANI SANA KWA USUMBUFU WAPENZI WOTE MLIOKUA MKISUBIRI RECIPE YA CHAKULA HIKI MEMORY CARD YA CAMERA YANGU IMEKUFA NA PICHA ZIMEPOTEA NATENGENEZA UPYA CHAKULA HIKI KISHA NITAWEKA RECIPE PAMOJA NA PICHA ILI KURAHISISHA KWA MPIKAJI




Friday, June 18, 2010

JITAIDI KUA MBUNIFU KATIKA KUPAMBA CHAKULA CHAKO



UBUNIFU WA KUPAMBA CHAKULA KATIKA MUONEKANO WA KIPEKEE INASAIDIA SANA KUONGEZA HAMASA KWA MLAJI HATA KAMA CHAKULA HAKIKUA NA LADHA SAFI MLAJI ANARIDHIKA KWANZA KABLA YA KUKIONJA



Huu ni muonekano wa bata wa kuchonga kwa kutumia tunda nanasi safi sana pamba mezani na mwisho wa chakula unaweza kula kama kikata hamu na familia yako


Ni rahisi sana jinsi ya kuchonga katika muonekano huu


Hii ni keki nzuri kabisa ya vanilla cream na karanga


Pamba vizuri sahani zako hata kama unawageni 100 uhuru wa kila mtu kula kwa sahani yake ikiwa imepambwa inapendeza sana sana


Kata matunda na panga sahani kubwa kwa mtindo huu ikiwa unafamilia kubwa au unawageni nyumbani kila mmoja atachukua aina ya tunda analopenda kutokana na mvuto wa mpangilio


Si kazi ngumu kukata na kupamba sahani ya matunda hakuna kizuri kisicho na juhudi kikubwa ni wewe kupenda kuhudumia chakula chenye muonekano thabiti.

WASANGAZE FAMILIA YAKO KWA KUPAMBA SAFI CHAKULA CHAKO NAWATAKIA WEEKEND NJEMA




TENGENEZA KEKI YA TUNDA TUFAA ( APPLE)

HII NI KEKI NZURI YA TUFAA AU APPLE SAFI KULA BAADA YA CHAKULA AU UNAWEZA KULA NA CHAI YA SAA 10 JIONI

MAHITAJI

170 gram siagi
170 gram sukari
1/2 kijiko kidogo cha chai kwaruza ganda la limao
4 mayai mabichi sawa na (210 gram)
275 gram unga wa ngano
1 kijiko kikubwa cha chakula baking powder
100 gram maziwa ya maji au cream
ca. 20 lavender leaves
3 au 4 apple kata vipande vidogo vidogo
3 kijiko kikubwa cha chakula
60gram majani ya mchai chai (lemon grass)

JINSI YA KUANDAA

Changanya sukari na siagi kwa uwiano wa uzito sawa ile ya gram 170 mpaka ichanganyike vizuri.

Kisha weka chenga za limao ulizokwaruza pamoja na mayai endelea kuchanganya

Kisha weka unga wa ngano na baking powder enedela kuchanganya kiasi

kisha ongeza maziwa na mchai chai ulikatwa vipande vidogo vidogo

kisha mimina mchanganyiko wako kwenye chombo unachotumia kuokea

kisha chomeka katika mchanganyiko wako vipande vya apple safi vienee

mwisho chukua vile vijiko vitatu vya sukari juu ya mchanganyiko wako

choma katika oven kwa moto wa nyuzi joto 175°C kwa dakika 45 mpaka 55 mpaka iwe rangi ya kahawia safi kisha itoe ipoe tayari kwa kuliwa.



Huu ni muonekano wa mmea wa mchai chai na majani yake


Huu ni muonekano wa shina la mchai chai na ndio inahitajika kwajili ya keki yako kata vipande vidogo vidogo sana kisha tumia katika mchanganyiko wako wa keki kwa harufu na ladha safi

Huu ni muonekano wa rangi nzuri ya juu safi wa keki yako baada ya kuiva



Huu ni muonekano safi kabisa baada ya kuikata keki yako unaona vipande vidogo vidogo vya mchai chai na tunda tufaa au apple. Unaweza kula ikiwa ya moto au ikiwa imepoa yote sawa pia unaweza kuhifadhi katika friji kwa muda wa wiki moja tu.





Sunday, June 13, 2010

SALAMU ZA SHUKURANI TOKA KWA MDAU KWA MAFANIKIO YA MENU YA WATOTO

NATUMAINI UMZIMA KAKA PAMOJA NA FAMILIA YAKO

NIANZE KWA KUKUSHUKURU KAKA KWA RATIBA YA MTOTO KWA KWELI NI NZURI NIMEWAPIKIA WATOTO WANAFURAHI AJABU NI HAKUNA AMBACHO NIMEPIWAANDALIA KIKAWASHINDA KWA KWELI KWA UPANDE WANGU NAONA IMERAHISISHIA KWANI NANUNUA VITU VYOTE NA KAMA ULIVYOSEMA VINAJIRUDIA KWA HIYO NIMEIPENDA SANA KAKA SINA CHAKUSEMA HATA ASANTE NAONA NI NDOGO NIKUOMBEE KWA MWENYEZI MUNGU AKUPATIE AFYA NJEMA PAMOJA NA FAMILIA YAKO NA MAISHA MAREFU KWANI BILA WEWE HIVI VYOTE NAONA INGEKUWA NI NDOTO KWANGU KUVIJUA.
UBARIKIWE SANA NA SIKU NJEMA MDAU

NASHUKURU SANA DADA YANGU KWA PONGEZI ZAKO NA PIA KWA KUJITAIDI KUWAJALIA WANAO PIA NAWE HONGERA SANA KWA KUWEZA KUTENGENEZA CHAKULA SAFI KWA WATOTO WAKO MWENYEZI MUNGU ATUBARIKI SOTE AMIIN CHEF ISSA



Saturday, June 12, 2010

JINSI YA KUPIKA BIRIYANI KWA KUTUMIA WALI WA BASMATI NA NYAMA YA KUKU, MBUZI AU NG'OMBE

MAHITAJI

1 kilo mchele wa basmati mrefu

1 kilo nyama iwe ya kuku au ng'ombe au mbuzi kata katika umbo dogo la kutosha kula kisha ichemshe na tangawizi na kitunguu swaumu, unga wa binzari (turmeric powder) pili pili manga na chumvi ili kuweka ladha nzuri. Ikisha iva itoe iweke pembeni na mchuzi wake uweke pembeni utautumia baadae.
1 kilo ya vitunguu kata slice ( mviringo)
1 kilo nyanya nyekudu zilizoiva, osha vizuri kisha katakata saizi ndogo ndogo sana
240 gram ya Mafuta ya kupikia
240 gram ya samli au mafuta yeyote ya kupikia
2 maggi chicken soup cubes
3 kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili mwekundu
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa binzari (turmeric powder)
3 kijiko kidogo cha chai unga wa girigilani (coriander powder)
2 kijiko kikubwa cha chakula mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu swaumu vilivyosagwa (ginger-garlic paste )
50 gram korosho iliyo kaangwa usizisage zibaki nzima
50 gram majani ya girigilani (fresh coriander leaves, washed and chopped)
8-12 mbegu za nzima ya hiriki (green cardamoms)
4 bay leaves ( sifahamu kiswahili chake)
15 mbegu nzima ya pili pili manga (whole black peppercorns)
30 gram majani mabichi ya minti ( mint leaves )
salt kulingana na ladha yako binafsi
Jinsi ya kuanda

Weka mafuta katika sufuria yako iliyo juu ya moto tayari, kisha kaanga nyama yako iliyokwisha chemshwa mpaka iwe na rangi ya kahawia (golden brown)

Kisha itoe nyama hiyo na ichuje mafuta ili mafuta yanayobaki weka kitunguu na endelea kukaanga kwa dakika 7-10 kisha weka unga wa binzali, unga wa pili pili mwekundu, unga wa girigilani, bay leaves, mbegu za hiriki na nusu ya mbegu za pili pili manga.
Changanya vizuri mpaka utapata mchanganyiko mzuri mkavu miminia humo maji uliyotunza baada ya kuchemshia ile nyama yako na kuiweka pembeni ipoe. kisha weka nyanya fresh ndani ya sufuria yako pika mpaka maji yakauke na mafuta yaanze kuoneka kwa juu ndani ya sufuria.
Kisha weka nyama yako ndani ya sufuria pole pole halafu punguza moto acha ijipike kwa muda mpaka mchuzi wako na nyama vikamate ladha pia usisahau kuweka chumvi kulingana na ladha unayopenda.
Chukua sufuria nyingine weka mafuta ya samli na vitunguu ilivyoslice kisha kaanga na majani ya girigilani, majani ya mint na korosho funika kwa dakika 10 picha inaonyesha hapo chini, kisha weka wali wako mkavu uliokwisha oshwa vizuri na uchanganye vizuri ongeza vikombe 5 vya maji na chumvi kidogo mchele ukishaanza kuchemka funika sufuria lako na punguza moto maji yakisha kauka kiasi weka mchanganyiko wa ile nyama yako nusu tu juu ya wali wa basmati acha wali uive kabisa kisha itakua tayari kula na pakua chakula chako kikiwa cha moto,


Wali wa pishori ( Basmati rice) uliokwisha iva


muonekano wa majani ya girigirani wakati wa kukaangwa


 Wali wa pishori ( Basmati rice) uliokwisha iva ukakaangwa na vitungu na korosho


Nyama ya kuku iliokaangwa vizuri na viungo na nyanya ukapata mchanganyiko mzuri mzito




Muonekano halisi wa biriyani yako baada ya kuiva ikiwa imechanganyikana na nyama pia kumbuka kunamchuzi mzito na nyma ilibaki pembeni mlaji ataweza kujongezea kiasi apendacho.
Furahia chakula hiki pamoja na familia yako.

RECIPE HII NIMEIRUDIA KUTOKANA NA MAOMBI YA WADAU WENGI LENGO NI KILA MMOJA AFURAHIE NA AFAIDIKE