NDUGU ZANGU MNAOISHI PEKE YENU BILA FAMILIA KUBWA AU UNAISHI UGHAIBUNI KUTOKANA NA MAJUKUMU MENGI NA KUANA NA MUDA MCHACHE WA KUWEZA ANDAA CHAKULA KIZURI KWA NJIA HII UNAWEZA KUANDAA CHAKULA KIZURI KWA MUDA MFUPI KWA KUTUMIA MBOGA MAJANI ILIZOANDALIWA NA KUGANDISHWA KATIKA JOKOFU.
MAHITAJI
2 pc vifua vya kuku (Kata kata vipande vidogo)
60 gram soy sauce kwajili ya marinating
3 pc kwajili ya scrambled eggs ( yai la kuvuruga)
120 gram carrots mchanganyiko na njegere za kwenye mfuko
120 gram kitunguu cha kwenye mfuko au 2pc fresh kata kata
60 gram siagi iliyoyeyushwa
1 kitunguu swaumu kisage au 1 kijiko kidogo cha chai garlic powder
Nusu kilo ya wali uliokwisha pikwa ukaiva safi.
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Huu ni mchanganyiko wa mboga mboga kama unaovyoona katika picha kuna vitunguu mfuko mmoja na njegere na karoti katika mfuko mwingine.
Mwagia soy sauce katika bakuli safi lenye vipande vya kuku.
Kisha weka katika moto kikaango kikubwa, kabla ya kuweka kuku pia unatakiwa uweke mafuta kiasi yapate moto kasha mwagia kuku hao pamoja na mchanganyiko wake wa soya sauce kumbuka hutakiwi kuweka chumvi kwani soya sauce tayari inaladha ya chumvi.
Endelea kukaanga pole pole na hakikisha nyama zinageuka zachini kuja juu ili zote ziweze kuiva ila zisikauke, hakikisha ule mchanganyko wa soya sauce upungue kiasi nao usikaukie. kisha mwagia kitunguu na njegere pamoja na karoti na uendelee kukaanga na kugeuza. Pika mpaka mboga mbga zinukie harufu safi na kua laini.
Kisha weka wali wako uliokwisha iva pamoja na scrambled eggs pamoja na siagi na kitunguu swaumu hakikisha unakoroga vizuri na mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.
Baada ya kuchanganya mchanganyiko wako safi kabisa utapata muonekano huu lakini naimani ladha bado itakua haijakaa safi, Kisha ongezea kijiko kimoja kidogo cha chai soy sauce kuweka ladha sawa kasha wewe na rafiki yako au family enjoy!