KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KITAFUNWA HIKI KITAMU CHA MCHANGANYIKO WA CHOCOLATE NA KARANGA
MAHITAJI
175 grams Dark Chocolate, (chopped )
200 grams maziwa ya maji
15 grams siagi isiyo na chumvi
75 grams korosho za kuokwa au ( Karanga za kukaangwa)
5 gram chumvi
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Muda wa kuandaa: 1 saa hadi 2
Muda wa kupika: chini ya dakika 15
Inatosha vipande kwa watu 32 hadi 36
Kata kata chocolate, maziwa ya maji kisha changyana na siagi na chumvi katika sufuria kubwa.
Weka katika moto wa chini ili chocolate iyeyuke pole pole chocolate yako na kisha endelea kukoroga ichanganyike.
Changanya vizuri na uhakikishe imechanganyika vizuri na kua laini.
Baada ya chocolate kuyeyuka hakikisha una tupia ndani yake korosho, au karanga na wengine hutumia pistacho au walnuts.
Baada ya kuweka hizo karanga hakikisha unakoroga pia nazo zichanganyike vizuri pamoja na chocolate
Baada ya hapo mimina kwenye tray ya shepu yeyote upendayo wewe (mimi huwa natumia baking pan iliyowekwa karatasi au greased wax paper)
Hakikisha unaisambaza vizuri na upate uswa na umbo safi.
Acha chocolate yako ipoe, weka katika friji ipoe na igande. Kisha kata vipande vidogo vidogo unaweza kata 6X6 mistari ili upate vipande 32 hadi 36
Hapa ipo tayari kwa walaji kula au hata kuweka kwajili ya zawadi.Hakikisha inakaa kwenye ubaridi wa wastani ili isiyeyuke "Take a bite and experience chocolate heaven" :)
WAANDALIE FAMILIA ILI WAFURAHIE