RECIPE SAFI KABISA NA JINSI YA KUETENGENEZA KEKI YA NDIZI MBIVU
MAHITAJI
360gram unga wa ngano
180 gram sukari
1 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/2 teaspoon baking soda
1/4 kijiko kidogo cha chai chumvi
4 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya karanga
6 ndizi za kuiva zigandishe kwenye freezer
1/2 kijiko kidogo cha chai vanilla essence
100 gram korosho au karanga za kuoka
Kwajili ya Honey Cinnamon Frosting (Sio lazima)
300 gram Icing sugar
120 gram siagi isiyo na chumvi iyeyuke kama mafuta mgando yakupaka
1 kijiko kikubwa cha chakula Asali
1/8 kijiko kidogo cha chai unga wa cinnamon (Mdarasini)
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI
Washa oven yako katika moto wa 350 degrees. Chukua backing tray yenye mashimo 12 ya muffin kisha weka zile karatasi maalumu za kuokea au paper liners. Chukua bakuli safi kavu kasha changanya Unga wa ngano, sukari, baking powder na chumvi salt.
Kisha toa ndizi zilizokua katika freezer ziweke nje kwa dakika 20 zitoe barafu.
Menya ndizi na ziweke kwenye blenda saga mpaka upate rojo safi kabisa.
Kisha mwagia mchanganyiko wako wa ndizi kwenye mchanganyiko wa unga pamoja na mafuta ya karanga na vanilla.
Tumia mwiko kuchanganya pole pole mpaka mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.
Chukua kijiko kikubwa au mwiko kisha anza kumimina pole pole kwenye mashimo ya muffin.
Hakikisha umegawanya vizuri mchanganyiko wako utimie maffin 12 na ujazo uwe kama muonekano katika picha.
Oka ukiweka toothpick kati kati ya muffin na ukitoa inatoka safi bila uji uji, kwa dakika 25 hadi 30.
Zitoe muffin zako zikiwa bado katika zile karatasi maalumu za kuokea na weka zipoe ktk wire rack.
Kwajili ya Frosting ya asali: Kisha chukua Asali, sukari ya unga, unga wa mdarasini na siagi ilyoyeyuka kama mafuta mgando ya kupaka.
Nakushauri kutumia mixer ya umeme, piga kwadakika 4 hadi 5 mchanganyiko utakua laini.
Unaweza tumia walnut au karanga au korosho chaguo ni lako kisha zi chop chop.
Nakushauri tumia piping bag kupambia kwajuu. Unaweza tumia hata kijiko kupambia.
Sio lazima kuweka frosting lakini ukiweka inapendeza zaidi na utamu ndio unazidi na harufu safi ya mdalasini.
Mafuta ya karanga yanasaidia sana keki yako isishike na iwe rahisi kutoa wakati wa kula pia kwa wenye matatizo ya kiafya hasa sukari usitumie frosting.
Unaona vizuri spongy kwa ndani? Ipo fluffy, light and very flavorful.
We enjoyed them the day I made them (for evening tea or breakfast the next morning after warming them up slightly. It makes a great breakfast too.
Mwagia kwa juu hizo karanga zitaongeza ladha safi pia
Kama mchanganyiko wako utakua mzito basi unaweza ongeza maji ya vugu vugu 60 gram usitumie maziwa yataifunika ladha ya ndizi.
RECIPE SAFI SANA YA KITAFUNWA HIKI CHENEY LADHA YA NDIZI, MDARASINI NA ASALI