NIRAHISI SANA UTENGENEZAJI WAKE PAMOJA NA GHARAMA NAFUU NA MUDA WA MAANDALIZI NI MCHACHE
MAHITAJI
500 grams viazi ulaya
1 kijiko kimoja kidogo cha chai binzali nyembamba
1/4 kijiko kidogo cha chai manjano
1/2 kijiko kidogo cha chai pili pili ya unga (Chilli Powder)
5 gram maji ya limao au Lemon Juice
5 gram chumvi
5 gram majani ya korienda
JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Muda wa maandalizi : Dakika 15
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 2
Mimi nimetumia viazi ulaya vyekundu wewe unaweza tumia viazi ulaya vyovyote vile pia na binzali nyembamba.
Kata kata viazi katika vipande vidogo vidogo
Washa moto na kisha weka kikaango katika moto na kijiko kimoja kikubwa cha samli au blue band. kisha weka binzali nyembamba na manjano unga wa pili pili na uendelee kukaanga
Kabla viungo havijaungua weka viazi na chumvi kisha endelea kukaanga.
Hakikisha unakoroga vizuri vichanganyike kabisa
KIsha mwagia maji na ufunike na mfuniko. Maji yanasaidia kuivisha viazi vizuri. Koroga kidogo ili viazi visishike chini.
Inachukua kama dakika10 hadi 12 bonyeza viazi na kidole au mwiko ukiona vimekua laini, basi jua vimeiva. Kisha mwagia majani ya gili gilani na maji ya limao kuongeza ladha safi.
Mpatie mlaji chakula hiki kikiwa chamoto unaweza kula na wali, pialu au chapati na mchuzi wa nyama.
CHAKULA HIKI KINAMUONEKANO SAFI SANA