CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, February 28, 2011

HABARI WAPENZI WA BLOG


NASHUKURU SANA KWA WALE WOTE MLIONIPIGIA SIMU KIPINDI NIKIWA ARUSHA NA DAR ES SALAAM TUTAONANA TENA MWEZI WA TANO NITAKAPOKUJA LIKIZO FUPI.

PIA NAMPONGEZA SANA MAMA YANGU MZAZI ASIA KAPANDE KWA KUPATA TUZO YA HESHIMA KWA MWANAMKE ALIETOA MCHANGO MKUBWA SANA UPANDE WA MASWALA YA KILIMO FAMILIA NZIMA YA RAMADHANI KAPANDE TUNAFURAHIA SANA NA TUNAJIVUNIA SANA MAFANIKIO YAKO MAMA YETU MPENDWA



MAMA YANGU MZAZI NI WA PILI TOKA KUSHOTO WALIOSIMAMA MBELE AMEVAA NGUO YA RANGI YA BLUE NA HIJAB NYEUPE KASHIKA CHETI NA TUZO BIG UP MAMA.

TUZO HIZI ZILITOLEWA JANA UKUMBI WA MLIMANI CITY IKIWA NI SIKU YA MWANAMKE DUNIANI.

NAWATAKIA SIKU NJEMA

CHEF ISSA

Monday, February 14, 2011

HAPPY VALENTINE KWA WAPENZI WOOTE WA CULINARY CHAMBER


NAWATAKIA KHERI YA SIKUKU YA WAPENDANAO. UPENDO NI MUHIMU SANA KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIMU. LEO NIMEADHIMISHA KWA KUONYESHA UPENDO KWA WATU WOOTE TUNAOFAHAMIANA PIA NIMEWEZA KUWAPATIA CHAKULA RAFIKI ZANGU BATA WANAOISHI KATIKA MTO ULIO JIRANI NA NYUMBANI KWANGU WALIFURAHI SANA SANA MAANA LEO NIMEWAPATIA ZAIDI YA KILO 2 ZA CHAKULA.

PIA NAWAOMBA RADHI WAPENZI WOTE KWA KUCHELEWA KUWEKA MAELEZO AU RECIPE BAADA YA KUANDAA CHAKULA NA KUWEKA PICHA. SABABU YA KUCHELEWA NI KUBANWA NA KAZI PIA NACHUKUA MUDA MWINGI SANA KUANDIKA KISWAHIKLI FASAHA NA CHEPESI KILA MTU AWEZE KUELEWA KWA URAHISI.

MIKAKATI YANGU NI KUANZA KUWEKA VIDEO ZA MAPISHI HAPA ITAHITAJIKA RECIPE TU MAELEZO WATU WATAKUA WANAANGALIA KATIKA VIDEO. NIKIJAALIWA KUPATA CAMERA NZURI NITAANZA KUWEKA VIDEO.

NATAMANI SANA KUONA PICHA ZA VYAKULA MNAVYOTENGENEZA MAJUMBANI KWENU BAADA YA KUSOMA RECIPE TAFADHALI NAOMBA MNITUMIE JAMANI MHHHH  !!!!!??? NIWEKE KATIKA BLOG.



Nimewazoesha nawarushia chakula wakiwa mtoni kila siku jioni kama nipo nyumbani



Leo chakula kilikua kingi sana kiasi wamekuja mpaka darajani kwenye barabara wakifurahia kula nafaka. Bata hawa wanapendeza sana kwa rangi zao na tabia pia.


Friday, February 11, 2011

JIFUNZE KUPIKA BIRIYANI SAFI NA RAHISI YA KUKU

 RECIPE SAFI SANA YA BIRIYANI YA KUKU

MAHITAJI

 ( Chakula hiki kinatosha watu 3 hadi 5 )



 600 gram mchele wa basmati basmati
 1 kuku mzima ( toa ngozi na kata vipande vikubwa kama kwenye picha)
6 Vitunguu umbo la kati
15 gram kitunguu swaumu cha kusagwa
10 gram tangawizi ya kusagwa
3 Nyanya katakat vipande vidogo
3 pili pili mbuzi za kijani
1 fungu la majani ya Mint
1 fungu la majani ya Coriander (giligilani)
3 kijiko kidogo cha chai Garam masala
100 gram Yogurt
1 kijiko kikubwa cha chakula juisi ya limao
3 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya samli
3 kijiko kikubwa cha chakula maziwa ya maji

VIUNGO VIZIMA VIZIMA PIA VINATAKIWA:

3 vipande vya mdalasini cinnamon stick
6 vipande vya karafuu
2 vipande vya hiriki ya kijani

KWA KUPAMBIA BIRIYANI YAKO:

Mafuta ya kukaangia
1 kitunguu kata slice
10 vipande vya korosho (Cashew nuts)
15 vipande vya zabibu kavu (Rasins)

JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI



1. Loweka mchele kwenye maji kwa masaa 3.
2. Kisha chemsha mchele katika maji, chumvi na 1 kijiko cha garam masala kwa dakika 15, kisha toa mchele wako uchuje na weka pembeni. Wali huu ukiubonyeza kwa mikono utavunjika ingawa utakua haujaiva vizuri. Huu ndio ubora unaotakiwa kwani ukiivisha kabisa utakua umekosea.

3. Safisha kuku na kata katika vipande vikubwa.Kumbuka kukata kata mikato katika nyama ili iweze kuja kuiva haraka.



4. Chukua sufuria kubwa linaloweza kuingia mchele na kuku yoote wakati unapika. kisha weka samli iyeyuke
5.  Kisha weka viungo vyoote na kaanga mapaka upate harufu nzuri (aroma).
6. Kisha weka kitunguu na chumvi. Pika mapaka vitunguu vilainike. Kisha punguza moto uwe wa wastani.


7. Kisha weka kitunguu swaumu na tangawizi kaanga mpaka upate rangi ya kahawia.
8. Kisha weka nyanya na pili pili mbuzi. Acha mchanganyiko huu uive mpaka nyanya ipondeke .



9. Kisha weka majani ya mint na coriander . Funika na mfuniko na pika kwa dakika 10.



10. Kisha weka yogurt na unga wa garam masala.
11. Kisha ongeza limao juice na chumvi kidogo.


12.   Kisha chukua vipande vya kuku na weka katika mchanganyiko wako katika sufuria, funika na uache inaendelea kuiva.



13.   Kisha chukau wali na weka juu ya mchanganyiko wako wa kuku na mchuzi
14. Kisha mwagia maziwa juu ya wali.

15. Funika sufuri a yako hakikisha inafunika kabisa mvuke usitoke nje.
16. Baada ya hapo weka moto uwe mkali kabisa kwa dakika 2. KIsha punguza moto na acha ichemke kwa dakika 45.
17. Wakati huo huo pasha moto kikaango ili uweze kukaanga vitu utkavyopambia.




18. Choma vitunguu katika mafiuta mpaka upate rangi ya kahawia.
19. Kisha kaanga korosho mpaka rangi ya kahawia.
20. Kisha kaanga zabibu kavu kwa dakika 1 tu.
21. Baada ya kusubiri kwa dakika 45 sasa zungusha wali wako pamoja na nyama ya kuku vichanganyike pole pole.



22. Pakua chakula chako na ukipambe kisha mpatie mlaji kikiwa cha moto.

MBINU ENDAPO UNATAKA KUTUMIA NYAMA TOFAUTI:
1.Kama unataka kutumia nyama ya ngombe au ya mbuzi au yakondoo.

Unatakiwa nyama uiwekee viungo hivi na ikae usiku kucha katika friji ili iweze kua laini ( 100 gram yogurt, 1 kijiko cha chakula white vinegar- 1 kijiko cha chai garam masala powder).
Kwa mtindo huu wali itabidi upike kwa dakika 10 pembeni.
Katika sufuria ya mchanganyiko wa nyama kwa kufata hatua zile ziule kitakachoongezeka ni muda wa kupika ikiwa ni nyama pika kwa saa 1 na dakika 15.





CHAKULA HIKI NI KITAMU SANA NA NIRAHISI KUKITENGENEZA WAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE CHAKULA HIKI.

JIFUNZE KUPIKA MCHUZI SAFI WENYE VIUNGO PAMOJA NA VIAZI NA MCHANGANYIKO WA PRAWNS


MCHUZI HUU WENYE MCHANGANYIKO WA VIUNGO, VIAZI MBATATA (ULAYA) NA PRAWNS NI SAFI SANA KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI SANA


MAHITAJI

 ½ kg ya prawns

 3 viazi vikubwa menya kisha katakata vipande
 2 vya ukubwa wa wasyani chop chop
5 gram kitunguu swaumu
5gram tangawizi
1 Nyanya ya kuiva  kubwa katakata
 2 Pili pili mbuzi ya kijani katakata
 1 kijiko kidogfo cha chai Coriander powder
 1 kijiko kidogo cha chai Turmeric powder
 ¼ kijiko kidogo cha chai  Fennel seeds powder ( sio lazima)
 ¼ kijiko kidogo cha chai Garam masala powder
  1 fungu la Coriander ( giligilani) chop chop
3 kijiko kikubwa cha chakula Coconut milk powder
3 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia
1 lita ya maji ya kupikia
 ½ kijiko kidogo cha chai sukari
5 gram chumvi

 



JINSI YA KUANDAA FATILIA MAELEZO HAPA CHINI

 
1. Chukua prawns wawekee maji ya limao pamoja na chumvi, pili pili manga kidogo na kitunguu swaumu kidogo kisha weka katika fridge kwa dakika 15 hadi 20.

2. Baada ya dakika 20 toa limao itakua imeingiza vizuri katika prawns.

3. Weka mafuta katika kikaango au sufuria kisha yapate moto wa wastani.

4. Baada ya mafuta kupata moto weka kitunguu na endelea kukaanga.

5. Kisha ongeza kitunguu swaumu na tangawizi endelea kukaanga mpaka harufu ya ubichi iishe.

6. Kisha weka pili pili mbuzi, turmeric powder endelea kukaanga mpaka mpaka upate harufu safi ya kunukia.

7. Kisha weka coriander powder, turmeric powder and fennel powder koroga ichanganyike vizuri. Viungo vingi ni vya unga weka maji kidogo kulainisha ili mchanganyiko wako usiungua na kushika sufuria. Acha iive pole pole mpaka ubichi na harufu ya masala upotee.

8. Kisha ongeza nyanya na piaka kwa muda.

9. Kisha ongeza vipande vya viazi, maji kiasi tena pamoja na chumvi.

10. Pika kwa moto wa wastani mpaka viazi viive na maji yapungue.

11. Wakati huo huo chukua wale prawn na uwakaange katika kikaango chenye mafuta kiasi kwa dakika 3.

12. Kisha chukua hao prawns na waweke katika ule mchanganyiko wenye viazi.

13. Chukua glasi na weka maji ya vugu vugu nusu na uchanganye na ile coconut milk powder hakikisha unakoroga vizuri kutoa mabonge mabonge.

14. Punguza moto tena na mimina na ukorogr coconut milk katka mchanganyiko wenye viazi na prawns.

15. Nazi ikisha iva ndani ya mchanganyiko wako hapo chakula kitakua taari kuliwa chukua majani ya coriander chop chop unaweza mpatia mlaji chakula hiki pamoja na wali au mkate au chapati na ikapendeza sana na familia ikafurahia sana.





CHAKULA HIKI KINATOSHA KWA WATU WA 5  AU ZAIDI INATEGEMEA NA UWEZO WA WALAJI.


 

JIFUNZE KUPIKA SAMAKI TIKKA TAMU KULIKO ZOOTE

KAA TAYARI KWA KUJIFUNZA JINSI YA KUPIKA FILLET YA SAMAKI KWA KUTYUMIA SAUCE AINA YA TIKKA

MAHITAJI

 (Chakula hiki kinatosha watu 4 mpaka 5)



Salmon, Changu, Red snapper, Sangara au Sato - ½ kg fillet toa ngozi
Siagi - 1 spoon (Sio lazima)


 Mahitaji kwajili ya tikka sauce

 1 Kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili
 ½ Kijiko kidogo cha hai unga wa manjano
1 Kijiko kidogo cha chai Garam masala
 1 Kijiko kidogo cha chai pili pili manga
 1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kusagwa
1 kijiko kidogo cha chai tangawizi ya kusagwa
 1 Limao kubwa kamua maji yake
5 gram chumvi



JINSI YA KUANDAA FATA MAELEZO HAPA CHINI

1. Changanya katika bakuli viungo vyote kwa pamoja kwajili ya Tikka sauce utapata mchanganyiko mzito sana ili uweze kushika katika fillet ya samaki.

2. Chukua fillet ya samaki uliokwisha kata kata vipande na uzitumbukize kwenye mchanganyiko wa tikka.

3. Baada ya vipande vyote vya samaki kuenea mchanganyiko huo kisha chukua cling film au plastick wrap funika vizuri bakuli kako.

4. Kisha weka katika friji kwa masaa 5 au 6 ili ule mchanganyiko wa tikka ukolee katika fillet ya samaki .

5. Baada ya masaa 6 toa katika friji mchanganyiko wa tikka utakua umeshika vizuri sana samaki wako.

6. Pole pole toa kipande kimoja baada ya kingine na weka katika oven au kama unajiko la mkaa juu ya waya wa kuchomea tayari kwa kuchoma au kuoka.

( Pia unaweza tumia microwave oven kwajili ya kuchomea maelezo yapo hapo chini namba 7.)

7. Choma pole pole kwa moto wa 100⁰C dakika 12 moto wa kawaida kisha badilisha ongeza moto wa  (200⁰C) choma kwa dakika 2 mpaka 3 kisha zima oven yako ila usitoe samaki nje ya oven.

8. Baada ya kuzima oven acha kwa dakika 15 samaki akauke vizuri baada ya hapo unaweza mpatia mlaji.

9. Hapa sasa unatakiwa uyeyushe siagi kisha mwagia kwa juu ili kuongeza ladha.

 


MBINU ZAIDI:

 
Ili uweze pata ladha safi ya tikka jitaidi kata fillet ya samaki wako kwa upana wa inchi 1 tu.