CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, January 11, 2011

JIFUNZE KUPIKA NYAMA YA FIGO KWA NJIA RAHISI NA NAFUU KWA GHARAMA


UNAWEZA PIKA KWA MTINDO HUU NYAMA YA MOYO, FIRIGISI, MAINI NA ZIKAWA LAINI NA TAMU SANA KWA MUDA MFUPI KABISA KAA TAYARI KWA RECIPE

MAHITAJI

500 gram Nyma ya figo
1 kitunguu kikubwa
1 pili pili hoho kubwa
5 gram chumvi
150 gram nyanya ya kopo
20 gram unga wa binzali
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia


JINSI YAKUANDAA FATILIA MAFUNZO NA PICHA HAPO CHINI


Kata kata nyama vipande vidogo vidogo iwe rahisi kuiva, pia kata kata pili pili hoho na kitunguu.


Kisha weka mafuta katika kikaango au sufuri yakishapata moto weka mchanganyiko wako wa kitunguu, pili pili hoho na kitunguu kwa wakati mmoja na uendelee kukaanga.


Mimi huwa natumia chumvi hii iliyochanganywa na mboga majani zilizokaushwa lakini wewe unaweza tumia chumvi ya kawaida inafaa sana tu kaanga kwa dakika 2.


Kisha endelea kukaanga ili chakula kichanganyike safi


Funika kikaango chako kwa dakika 1


Baada ya dakika 2 funua uangalie chakula kinaendeleaje kisha weka unga wa binzali kwa harufu na ladha nzuri.


Kisha weka nyanya ya kopo na uendelee kukaanga



Kisha funika sufuria tena kwa dakika 2 tu


Baada ya dakika 2 funua chakula kitakua kimeiva tayari kwa mlaji kufurahia.






 
CHAKULA HIKI UNAWEZA KULA ASUBUHI WAKATI WA CHAI PIA UNAWEZA KULA NA UGALI, VIAZI VYA KUCHEMSHA, WALI, UGALI AU VIAZI VYA KUKAANGA.

CHAKULA HIKI HASA NA AINA HII YA MAPISHI NI KIZURI SANA KWA KINA MAMA WAJAWAZITO ENDAPO AMEPUNGUKIWA DAMU MWILINI INASAIDIA KURUDISHA DAMU HARAKA SANA IKIWA UTAMPIKIA MAINI YA NG'OMBE. LADHA HII NI SAFI NA NYAMA INAKUA LAINI FAMILIA YAKO ITAFURAHIA SANA SANA.


11 comments:

Sarah said...

kaka Issa mbona hujaweka receipt za hizo figo? umeonyesha tu picha

Anonymous said...

si umeambiwa kaa tayari kwa receipe, au anamaanisha subiri maelezo. Ni recipe sio receipt

Anonymous said...

nyam nyam nyam......., imenoga sana

Anonymous said...

Kaka Issa Mi huwa ni mfwatiliaji mzuri sana wa haya mafundisho yako.
Sasa unaonaje ukatengeneza kitabu cha kiswahili cha mapishi na ukatuwekea picha hata kama zitakuwa ndoto na recepi zake.
Nitashukuru sana.

Anonymous said...

Allkrydda nini ? naomba kufahamishwa na hapa tanzania inapatikana au kama haipatikani ninaweza weka nini badala yake?

Unknown said...

GOOD NEWS! Asante kaka vyakula hivi kwa sisi wafanyakazi uwa ni simple kuvitayarisha!!

Unknown said...

GOOD NEWS! Asante kaka vyakula hivi kwa sisi wafanyakazi uwa ni simple kuvitayarisha!!

Issa Kesu said...

WELL COME BACK BAZIZANE ULIPOTEA SANA SANA MISS YOUR COMENTS.

CHEF ISSA

Anonymous said...

Big up bro Isa,

Nilikuwa siifahamu blog yako nimeijua kwa kutafuta recepe ya kupika njugu mawe ikanidirect kwako.... ila sijafanikiwa kuipata waweza kuirudia please?!!.

Cath

MUMY B said...

ISSA UPO JUU KAKA YANGU ILE RECEIPT
YA KUPIKA WALI WA KAROTI NA NYANYA MWANANGU ANAFURAHIA SANA CHAKULA MUNGU AKUBARIKI

salita said...

kwa kweli we ni balaa,thanx much kaka na andaa kitabu tutanunua.