CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, March 16, 2010

UNATAKA KUFANYA BBQ PARTY SUPER NYUMBANI KWAKO?


JIBU KUBADILISHA UBORA WA CHAKULA NA MTINDO WA MUONEKANO WA SHEREHE UTAYOIFANYA NYUMBANI KWAKO YA AINA YEYOTE ILE IKIWA UMEWAALIKA RAFIKI ZAKO AU NDUGU WA KARIBU WASHANGAZE NA WAFURAHIE IWE HISTORIA FATA MAELEKEZO YA MAANDALIZI KWAUJUMLA HAPO CHINI KAMA PICHA ZINAVYOOELEKEZA.





kata mboga zako aina tano au nne mfano kitunguu, nyanya, bilinganya, zucchini, carroti na pili pili hoho kisha  zipake mafuta na chumvi kisha ziweke kwenye kikaango au kwenye jiko lako la kuchomea nyama na uzichome ziive nusu zisiive sana ziweke pembeni zipoe na zitatumika kama salad wakati wa BBQ lunch au diner.




Hapa ni muonekano wa mpangilio mzima wa salad. Kwakua sherehe yetu ni BBQ basi kila chakula lazima hkiwe na ladha nzuri ya harufu ya moshi wa makaa. Zile mboga ulizochoma zipange vizuri katika sahani na uziweke sehemu moja kama zinavyoonekana katika picha wageni wako watafurahia sana saladi hii.





Katika picha unaona mpangilio wa sauce safi kabisa maalumu kwajili ya kulainisha na kuongeza ladha katika nyama choma zako safi kabisa. Kutoka kushoto katika picha ni Teriyaki sauce, BBQ sauce, vipande vya limao na chilly pickle jinsi ya kutengeneza vyote hivi mwisho kabisa soma recipe yake.




Hizi ni mbavu za nguruwe au (pork spare ribs).

Chukua mbavu za nguruwe kata katika mikato ya wastani ambayo unaweza kushika na kula. kisha chukua kitunguu swaumu na tangawizi iliyosagwa changanya na mafuta ya kupikia kidogo, nyanya ya kopo, soya sauce na chumvi kisha changanya mpaka rojo lote lishike nyama yote kisha weka katika oven iive nusiua narojo lile lishike vizuri kwenye nyama. kisha weka pembeni kwajili ya kuiivisha vizuri kabisa katika jiko lako la mkaa baadae wakati wa sherehe.




Hii ni nyama ya ngombe (Beef fillet)

Kata nyama kwa urefu umbo la kama kidole ili ilingane na iwe rahisi kuiweka katika mti wa mshikaki. Kisha chukua tangawizi na kitunguu swaumu kilichosagwa, chumvi, pili pili manga, mafuta ya kupikia, soya sauce, nyanya ya kopo, tabasco sauce kidogo na Hp sauce kidogo changanya mpaka rojo lote lichanganyike katika nyama yako iweke katika friji kwa muda wa saa nzima au 2 kisha iwe tayari kuchiomwa katika jiko la mkaa wakati wa sherehe mikato ya aina hii inasaidia uivaji na kupunguza gharama maana unatengeneza mishikaki mingi sana kwa nyama kiasi tu.

Mchanganyiko huu unaweza tumia pia unapoandaa kuku wa kuchoma mhhhh!!!!





Hii ni mishikaki ya samaki unaweza tumia fillet ya ( sangara, redsnapper, king fish, barakuda)
Kata fillet ya samaki kwa urefu ilingane kiasia urefu wa mshikaki wako hii inasaidia kuiva haraka na urahisi wa mlaji.
Baada ya kukata chomeka katika miti ya mishikaki. Kisha chukua juice ya limao, unga wa binzali, kitunguu swaumu na tangawizi iliyosagwa, chumvi na pili pili manga pia unaweza weka mtindi changanya mpaka rojolile lichanganyike vizuri kabisa kisha wea katika friji tayari kwa kuchomwa baadae wakati wa sherehe.




Hivi ni viazi mishikaki mhhh safi sana na rahisi kweli kutengeneza.

Chukua kiazi ulaya kimenye kisha kikate nusu, kisha chomeka katika kila nusu mti wa mshikaki kama inavyoonenkana kwenye picha. Kisha chukua sufuria weka maji baridi kisha weka viazi vyako na uchemshe mpaka viive nusu. Ukiweka maji baridi yanasaidia viazi vyako kuchemka pole pole pamoja na viazi hii itasaidia viazi vyako visipoteze umbo lake mongo'nyoka vitaiva na kubaki na umbo lake zuri. weka viazi kwa mtindio wa kusimamisha miti juu viazi chini ndani ya maji.

Tumia mti wa mshikaki kwajili ya kucheki kama viazi mvimeiva ukichoma mti ukaingia kirahisi badi vimeiva kama havijaiva mti hauwezi kuingia. kisha vitoe viazi vyako vikae pembeni visubiri kuchomwa wakati wa sherehe. 







Sasa ndio wakati wenyewe umewadia wageni wameshafika na chakula chako kipo jikoni tayari kwa kuwashangaza wale wote walioudhulia kwa kula chakula chenye ladha safi na kinapikwa live!!

Tenganisha nyama zako kama inavyoonekana katika picha Kiazi kikae mahala pake kisichanganyike na nyama yeyote ile, pia samaki na nguruwe zisiguzane na nyama yeyote ile maana sio kila mtu anakula samaki na ngurue aidha kwa misinghi ya dini au aleji.

Nyama ya ngo'mbe na kuku vianweza kukaa pamoja hakuna neno vyakula vyako vyote katika jiko la mkaa vipake mafuta ving'ae ili vipate rangi nzuri ya kahawia ukiendelea kuvichoma pia mafuta yanapodondokea katika mkaa na ladha ile ya nyama inatoa moshi mzuri wenye harufu ya nyama choma na kuwadondosha mate na kuwazidishia hamu wageni si mchezo wakati bado hawajaruhusiwa kuvamia sehemu ya maakuli yanayopikwa live.




Huu ni mpangilo safi kabisa wa nyama pamoja na viazi katika jiko lako la nyama choma kumbuka miti ya mishikaki iangalie nje ya jiko hii ni kwajili ya usalama wa miti isiungue na wewe mchomaji iwe rahisi kugeuza na wakati mlaji anahitaji ni rahisi kuchukua katika jiko. Huitaji madishi ya kuhifadhia chakula maa chakula chote unapika live katika jiko moja yaani we acha tu ni rahisi na ninafuu sana na itapendeza sana sana. 



Yaani kila kitu kime kaa ki BBQ tu baada ya kupata mlo safi kabisa mwisho ni kikata hamu cha chakula chukua matunda yako ya aina 3 hadi 5 au 6 kulingana na uwezo wako. katika picha huo ni mshikaki wa matunda ya aina 3 tu. chukua nanasi, embe na water melon kata mtindo wa box kisha tunga katika mti wa mshikaki na weka katika sahani yako safi na uweke kwenye friji yapoe kwajili ya kuliwa katika sherehe.




Hahaha samahani jamani huu ndio muonekano wa chakula katika sahani baada ya kujipakulia ni rahisi kula ni rahisi kuandaa na gharama ni nafuu sana na wageni wako hawata chafuka na michuzi kila mtu anaweza kuaanda hivi nyumbani kwa gharama nafuu sana ukiniambia idadi ya watu unaotaka kuwaalika nitakupa kiasi cha mahitaji anaukafanya BBQ party yako iwe safi kabisa.


JINSI YA KUANDAA VIKOLOMBWEZO VYA KULIA NYAMA

Jinsi ya kutengeneza pili pili angalia mafunzo ya mwezi wa pili katika blog archive

BBQ sauce zipo madukani nyingi san tu zinauzwa na ninafuu kununua kuliko kutengeneza

Malimao unakata kama picha inavyoonyesha

Jinsi ya kuandaa teriyaki sauce

400gram Chukua soya sauce
200gram maji
50gram kitunguu swaumu kilichosagwa
50gram tangawizi iliyosagwa

Chemsha kwa pamoja mpaka ipungue na kua nzito kiasi kisha weka ipoe tyari kwa kuliwa na nyama choma

MAHITAJI YA BBQ KAMA UNAWATU 100 HADI 150

17 Kuku ( kuku mmoja kata vipande 10)
5 kilo Fillet ya ng'ombe
5 kilo Mbavu za nguruwe
5 kilo Fillet ya samaki
20 kilo Viazi ulaya

BBQ SALAD
3 kilo Nyanya
3 kilo Kitunguu
3 kilo karoti
2 kilo Bilinganya
2 kilo Zucchini



16 comments:

Hilda said...

Chef Issa hii kitu imetulia kwa sana. Yaani mpangilio uko bomba

Hilda

Anonymous said...

Kaka tupe mambo, jamani tuna mpango wa kufanya BBQ katika mahari ya rafiki yetu.

Asante sana.


disminder.

Anonymous said...

kaka uko juu sana na hili lazima nilifanyie kazi sasa hapo umesahau salad si unajua tena kaka nimekukubalin hope baadae tutapata mengine

g.day

Anonymous said...

Ushauri wangu hebu andaa kijitabu cha mapishi utuuzie!! HONGERA SANAAAAAAA

Anonymous said...

kweli duniani kuna karama na vipawa mbalimbali!! Nakufagilia saana mdogo wangu,tulisoma wote kule nyegezi japo ulikuwa nyuma darasa moja!!

Anonymous said...

pole na kazi kaka, ila me nashukuru najifunza vema kupika chakula kizuri na mume wangu anaenjoy sana,juzi tumekula nyama ya mbuzi na chapati,
sasa ombi picha hii kwa sisi wengine ingependeza kama ungeweka na maelezo japo kwa ufupi ili tujue unaandaaje na salad zake zinakuaje.asante naomba huo msaada kaka.

Anonymous said...

Mhe. Chef Issa, tunaomba maelezo kidogo jinsi ya kutengeneza BBQ ulizozionyesha hapo ili tuweze kufanya practices.
Pia ukipata muda unaweza ukatufundisha jinsi ya kupika mboga mbali mbali za kitanzania kwani huku misosi mingi tunayokula ni ya kichina.

Mdau China

Anonymous said...

Kaka Issa ahsante kwa kutuwekea mapishi safi kabisa ila umesahau kuweka maelekezo baada ya picha.

Anonymous said...

kaka tutajie majina yake na ni vipi vimetengenezwa, nimependa sana. Uko juuuuuuuuuuuuuu

Anonymous said...

mimi ni mdau wa blog yako naipenda sana na naifwatilia sana nilikua naomba uniwekeeunajua jinsi ya kupica prons,kamba koche yaani sea food wengi tunajua tu kukaanga samaki na kula wakati kuna staly nyingi za kutengeneza sea food nitafurahi nikipata maelekezo ya mapishi.mdau miss kilimanjaro finland

Anonymous said...

kaka vipi uko busy sana?
Pole na kazi, tunakusubiri na vitu zaidi.


disminder.

Ruky said...

Asante sana Chef

Bennet said...

Hii kitu imetulia sana, yaani hapo kama una grants inashuka tu

Anonymous said...

Kaka sina la zaidi ila nipe mawazo ninunue vitu kiasi gani kama naalika watu 100 mpaka 150.
Unastahili tuzo kweli.


disminder.

Anonymous said...

Chef Issa, asante kwa kazi nzuri nimejifunza mambo mengi na naendelea kujifunza Big up ISSA!

Mom said...

Jamcjui nilikua wapi ckuwah kupata hii kitu! Chef Issa kweli mapishi unayajua wewe!