CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Wednesday, April 13, 2011

KUANZISHWA KWA CHAMA CHA KITAALAMU CHA WAPISHI TANZANIA


TAARIFA NJEMA KWA WAPISHI WOTE WA KITANZANIA.

Active chefs Association of Tanzania (acat 2011)

BAADA YA MAFANIKIO MAKUBWA YA BLOG YA ACTIVECHEF SASA NIMEAMUA KUANZISHA CHAMA CHA KITAALAMU CHA WAPISHI TANZANIA. CHAMA HIKI NI CHAMA KISICHO CHA KIBIASHARA.

NATOA WITO KWA NDUGU ZANGU WATANZANIA WAPISHI WA HAPA NYUMBANI NA WALIOKO NJE YA NCHI TUUNGANE NA TUJENGE CHAMA CHENYE NGUVU TUWEZE TAMBULIKA KATIKA ULIMWENGU WA MAPISHI DUNIANI.

KWASASA TAYARI WAMESHAPATIKANA WANACHAMA KUMI WATANZANIA TOKA SAUDI ARABIA, AMERICA, SWISS NA UK. NAWAKARIBISHA WOTE MJIUNGE NI BURE HAKUNA ADA YEYOTE. FOMU ZA KUJIUNGA TUMA EMAIL issakesu@gmail.com KISHA NITAKUATUMIA HARAKA NAWE UNAJAZ ANA KUSCAN KISHA UNANITUMIA. KUANZIA MWEZI UJAO TUTAKUA NA WEBSITE YA CHAMA NA EMAIL YA CHAMA IPO KATIKA MATENGENEZO.

NAWAOMBA SANA NDUGU ZANGU WATANZANIA MUITIKIE WITO ILI TUWEZE KUFAIDI MATUNDA YA TAALUMA HII PIA TUWEZE ANDIKA HISTORIA DUNIANI.

MALENGO BAADA YA KUANZISHA CHAMA KWA MAFANIKIO YA MIAKA 2 KISHA TUTAJIUNGA NA CHAMA CHA WAPISHI DUNIANI ( wacs) World Association of Chefs Societies. KWA KUJIUNGA KATIKA CHAMA HIKI TUTAWEZA PATA WASAHA WA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MAPISHI DUNIANI, KUSHIRIKI MAFUNZO NA MIKUTANO PAMOJA NA WAPISHI WALIOBOBEA DUNIANI NA MWISHO NI KUTAMBULIKA KOTE DUNIANI.

PIA TUNATEGEMEA KUJIUNGA NA CHAMA CHA World Master Chefs Society  HAPA WAPISHI WENYE NGAZI ZA EXECUTIVE WATAPANDA DARAJA NA KUA MASTER CHEF BAADA YA KUA WANACHAMA NA KUPATA MAFUNZO MAALUM.

VYAMA VYOTE HIVI VIKUBWA DUNIANI HUWEZI JIUNGA MPAKA UWE UMEJIUNGA KATIKA CHAMA NDANI YA NCHI YAKO HAWAKUBALI KUSAJILI MTU BINAFSI. KWASASA WANACHAMA WA VYAMA VYOTE HIVI NI NCHI 5 TU KWA AFRICA !! South Africa, Namibia, Egypt, Mauritius na Ghana. TUNAWEZA KABISA KUANDIKA HISTORIA YA MAFANIKIO IKIWA TUTAUNGANA NA KUA KITU KIMPOJA.

CHAMA CHETU KIKIWA THABITI TUTAWEZA KUTETEA HAKI YA MPISHI NA KURUDHISHA HADHI NA HESHIMA YA TAALUMA HII ADIMU NA ADHIMU DUNIANI.

UNAWEZA TEMBELEA SITE HIZI ZA VYAMA HIVI VIKUBWA DUNIANI www.worldmasterchefs.com/ NA  http://www.wacs2000.org/

MWEZI WA 5 KUANZIA TAR 1 NITAKUA DAR ES SALAAM KISHA NITAKWENDA ARUSHA NAIMANI UTAKUA WASAHA MAALUMU KUWEZA KUKUTANA NA WAPISHI WENZANGU TUKAZUNGUMZA KWA UNDANI ZAIDI NA NIKAWEZA JIBU MASWALI YENU KUMBUKENI HAKUNA MAFANIKIO BILA JUHUDI, MIPANGO NA MAARIFA. PIA UMOJA NI NGUVU.



Hii ni moja ya nembo zitakazotumia katika website




Hii ni nembo maalumu ya chama na itatumika katika sehemu zote za utambulisho ikiwemo website
 

Picha hii chef Issa akiwa katika mashindano ya Junior chefs katika kitongoji cha Luzern Switzerland na kuibuka mshindi wa kwanza.



Picha hii chef Issa akiwa katika mashindano ya Junior chefs katika kitongoji cha Luzern Switzerland na kuibuka mshindi wa kwanza.




Picha hii chef Issa akiwa katika mashindano ya Junior chefs katika utengenezaji wa chocolate ktk kitongoji cha Interlaken Switzerland na kuibuka mshindi wa tatu.
  

Picha hii chef Issa akiwa katika Tamasha kubwa duniani la sana zote ikiwemo ya upishi katika kitongoji cha Basel Switzerland.
 

Picha hii chef Issa akiwa katika kongamano la Junior chefs Munich German.

KILA MTU ANAWEZA AKIPEWA NAFASI NA WASAHA. SASA NI ZAMU YA WAPISHI WA KITANZANIA KUFAHAMIKA DUNIANI NA KUJIWEKEA HESHIMA NA MAISHA BORA.

KARIBUNI SANA SANA FOMU NI BURE.

CHEF ISSA

10 comments:

Anonymous said...

Hongera kaka kwa moyo wa uzalendo.
Ni wachache wanaopenda na wenzao wafaidike. Mungu akuzidishie

mama Jeremiah said...

Asante kaka, Tunashukuru sana kwa hili. Ninaamini wapishi wa nyumbani watajiunga. Mimi sio mpishi ila natamani kweil nijiunge na mimi nipate kuongeza ujuzi wangu wa kupika!.

Mungu awatangulie katika kila lililo jema. Ninaamini Hiki chombo kitakuwa mtetezi wa wapishi wote Tanzania

Anonymous said...

Hongera kaka Issa kwa mafanikio yako....Mungu akujaaalie na kukuzidishia na akufungulie milango ya kheri...upate nasi tufaidike.....natamani kukuona kwenye American Chopped chopped!!! lol!!!

Anonymous said...

chef hongera!! sana kwa ubunifu pia juhudi unazo tuonyesha tunakuombea afya njema na baraka tele katika shuguli zako za kila siku ili uweze kuwasaidia pia wale wanaopenda kukuwa katika fani hii lakini hawajui wapi pa kunzia mimi ni ushauri kwa machef wa kitanzania Mnatakiwa kuonyesha moyo na mfurahie kuwa wamepata mtu alie jitoa kuwapa muangaza na kujua Duniani nini kinafanyika katika fani ya mapishi ni wachache wenye moyo kama wake ,mwenyezi mungu akubariki sana na utafika mbali mpaka kwenye level ya master CHEF, we real proud of you ISSA

Dada Aisha said...

Mdogo wangu we real proud of you tunafurahia matunda ya shule yako Mama, Baba na wadogo zako wote wanafurahi kiasi kwamba kila mtu kapata faraja kubwa sana kuwa wakati unaondoka kwenda masomoni swis ulituahidi kuwa after that utafanya wonders kweli maneno yako yameonekana
tunakuombea heri baraka afya na maisha mema kwani unapo rudi likizo nyumbani huwa tunafurahi sana kwani unatufundisha na pia unaingia jikoni mwenyewe na kusema leo nawaandalia mimi chakula cha aina fulani
keep it up dear brother

Anonymous said...

Vipi bakers wanaruhusiwa kujiunga?

Anonymous said...

Duh we jamaa unauliza swali la kishamba kweli kwani baker sio mpishi? na mmeambiwa wapishi wote inamaana sio lazima hata uwe msomi ingawaji ni mpishi upo huru kujiunga kazi kwenu kalagabaho muendelee kua nyuma......lol

Mama Tweve

Anonymous said...

hongera sana Issa.

Na shida moja mie sijawahi kujiunga na shule yoyte inayohusu mapishi. so sijui kupika saana kikawaida chakula cha kibongo. sasa nataka kujifunza mapishi kwa ajili ya familia yangu tu na siku nikiwa na wageni niwapikie mpaka wafurahi. Sasa nianzia wapi jamani. Pia sitaki kukaa darasani muda mrefu kwa ajili ya jambo hili niko busy sana.

Anonymous said...

Kaka umenipa raha sana, naitayarisha nakutumia. Mungu atakuongezea Inshallah.

Shangwe.

Anonymous said...

KAKA VIPI UMESHAKUJA TANZANIA? NIMEKUTUMIA EMAIL UMEPATA?