KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABIS A YA KITAFUNWA HIKI CHA DENGU NA SPINACH
MAHITAJI
240 gram dengu (Whole Black Gram)
2 pili pili mbuzi (green chillies)
5 gram tangawizi ya kusaga
1 kitunguu maji kikubwa chop chop
240 gram spinach mbichi ikate kate (chopped Spinach)
5 gram chumvi
majani ya giligilani ya kuongeza ladha (Cilantro)
majani ya curry kwa kuongeza ladha (Curry leaves)
240 gram dengu (Whole Black Gram)
2 pili pili mbuzi (green chillies)
5 gram tangawizi ya kusaga
1 kitunguu maji kikubwa chop chop
240 gram spinach mbichi ikate kate (chopped Spinach)
5 gram chumvi
majani ya giligilani ya kuongeza ladha (Cilantro)
majani ya curry kwa kuongeza ladha (Curry leaves)
JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPA CHINI
Muda wa kuandaa : masaa 3 hadi 4
Muda wa kupika: dakika 30
Idadi ya walaji: Watu 4
Idadi wa vitafunwa : Kiasi cha 8-10 inategemea na upana au umbo
Loweka kwenye dengu kwenye maji kiasi cha lita moja kwa masaa 2 hadi 3 au mpaka utakapo ona zimeshameza maji na kulainika.
Hakikisha unazichuja na kuzikausha vizuri kama picha inavyoonyesha.
Weka dengu zako kwenye blenda ( food processor) pamoja na chumvi, tangawizi na pili pili ila sio lazima kama hutumii pili pili ingawa inaleta ladha ya kuchangamsha.
Hakikisha unasaga mchanganyiko uwe na muonekano kama huo usiweke kabisa maji ila kama blenda yako unaona haiwezi kusaga sababu ya ukavu basi weka maji kidogo sana ili uweze kusaga na kupata mchanagnyiko mkavu kama huo.
Kisha chukua dengu zilizosagwa weka katika bakuli pamoja na kitunguu maji, majani ya gili gilani, majani ya curry pamoja na spinach pia unaweza nyunyizia ndimu kiasi kuongeza ladha sio lazima.
Hakikisha unachanganya vizuri sana.
Kata kidogo na kisha hakikisha unatengeneza umbo la kama mpira.
Tumia karatasi ya Plastic na uipake mafuta kisha weka ule mviringo wa machanganyiko wa dengu na spinach juu yake kisha tumia vidole vyako viwili na ukandamize.
Tumia kidole chako na choma kati kati upate umbo kama la doughnut. Ni jinsi ya kutengeneza umbo zuri lakini sio lazima!
Chukua sufuria au kikaango weka mafuta kisha pata moto wa wastani chukua ile mchanganyiko kisha weka katika sufuria na endelea kukaanga hakikisha mafuta ni moto wasatani ili isibabuke na matokeo yake haiivi ndani (med-hot).
Kumbuka kugenuza mara kwa mara mpka upate rangi hii nzuri ya kahawia.
Kisha toa na weka katika karatasi ili yapoe na kuchuja mafuta pia. Kama ulifata maelekezo vizuri basi itaiva vizuri na wala hazitakau na mafuta kabisa karatasi haitaloana mafuta kabisa.
Hakikisha unampatia mlaji haraka sana ikiwa bado inamoto kwani ndio inakua na ladha nzuri pia unaweza kula na- Coconut chutney, spicy tomato chutney au tomato ketchup! ni nzito sana ukila unashiba kabisa.
Hazipendezi kukaa kwenye friji zaidi ya siku moja zinapoteza ladha na ubora pia
MIMI NA FAMILAI YANGU HUWA NAPENDA KULA NA SPICE TOMATO KETCHUP NA TUNAFURAHIA SANA. NI RAHISI KUTENGENEZA NA FAMILIA ITAFURAHIA SANA KITAFUNA HIKI.
3 comments:
inaelekea ni tamu sana... ila mahitaji na maelezo jinsi ya kutayarisha/kuntengeneza hujaweka, tunakuomba sana sana utuwekee tuweze kufurahia kitafunwa hii
mbona huweki maelekezo na majina ya ingredients?
hapa umeeleza vizuri thats good
Post a Comment