CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, July 11, 2011

WEWE NI MPENZI WA CHOCOLATE NA MCHANGANYIKO WA KARANGA?


KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KITAFUNWA HIKI KITAMU CHA MCHANGANYIKO WA CHOCOLATE NA KARANGA

MAHITAJI

175 grams Dark Chocolate, (chopped )

200 grams maziwa ya maji
15 grams siagi isiyo na chumvi
75 grams korosho za kuokwa au  ( Karanga za kukaangwa)
5 gram chumvi

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa kuandaa: 1 saa hadi  2

Muda wa kupika: chini ya dakika 15
Inatosha vipande kwa watu 32 hadi 36 
Kata kata chocolate, maziwa ya maji kisha changyana na siagi na chumvi katika sufuria kubwa.Weka katika moto wa chini ili chocolate iyeyuke pole pole chocolate yako na kisha endelea kukoroga ichanganyike.Changanya vizuri na uhakikishe imechanganyika vizuri na kua laini.Baada ya chocolate kuyeyuka hakikisha una tupia ndani yake korosho, au karanga na wengine hutumia pistacho au walnuts.

 


Baada ya kuweka hizo karanga hakikisha unakoroga pia nazo zichanganyike vizuri pamoja na chocolate

Baada ya hapo mimina kwenye tray ya shepu yeyote upendayo wewe (mimi huwa natumia baking pan iliyowekwa karatasi au greased wax paper)Hakikisha unaisambaza vizuri na upate uswa na umbo safi.Acha chocolate yako ipoe, weka katika friji ipoe na igande. Kisha kata vipande vidogo vidogo unaweza kata 6X6 mistari ili upate vipande 32 hadi 36
Hapa ipo tayari kwa walaji kula au hata kuweka kwajili ya zawadi.Hakikisha inakaa kwenye ubaridi wa wastani ili isiyeyuke "Take a bite and experience chocolate heaven" :)

WAANDALIE FAMILIA ILI WAFURAHIE

Sunday, July 10, 2011

NASHUKURU SANA WAPENZI WA BLOG KWA KUNIPIGIA KURA


HABARI NJEMA NDUGU ZANGU. NAWASHUKURU SANA KWA JUHUDI ZENU KATIKA KUNIPIGIA KURA NA PIA KATIKA KUTAMBUA MCHANGO WA MAFUNZO NAYOWAPATIA. BILA NYINYI WASOMAJI BLOG HII ISINGEKUWEPO NINGAKATA TAMAA KUWEPO KWENU NDIO UHAI WA BLOG HII. NAWASHUKURU SANA NA NAWAAHIDI KUENDELEZA LIBENEKE LA CHAKULA.


MATOKEO NDIO HAYA HAPA CHINI PAMOJA NA CHETI NILICHOTUMIWA

 


Okay guys here are the results for this year.....Congratulations to all finalists, winners and runners up.
The list for Best Food Blog was.

Best Food Blog

http://activechef.blogspot.com/ 51.77%
http://mapishimatamu.blogspot.com/ 28.37%
http://tasteoftanzania.com/ 11.35%
http://mrokim.blogspot.com/ 5.67%
http://www.bartycake.blogspot.com/ 2.84%..