CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, July 30, 2010

WAPENZI WOOTE WA BLOG HII LEO NI SIKU YANGU YA KUZALIWA!!!

NASHUKURU SANA WAPENZI WOTE WAA BLOG HII KWA DUA ZENU NA SALAMU NZURI SANA SANA KWA KUADHIMISHA SIKU YANGU YA KUZALIWA MWENYEZI MUNGU ANATULINDA TUNAENDELEZA DARASA LA MAPISHI KWA FURAHA

31 / 07 YA KILA MWAKA NI SIKU NZURI SANA KWANGU NAMSHUKU SANA MWENYEZI MUNGU KWA KUNIJALIA AFYA NJEMA, NGUVU, ELIMU NA UJUZI ILI NIWEZE KUKIMU MAISHA KWA KUJITAFUTIA NA KUSHIRIKIANA VIZURI NA KILA MTU.

TOKA NILIPOZALIWA MPAKA LEO NIMEWEZA KUA NA MARAFIKI WENGI SANA SANA HII YOTE NI SHULE NZURI NILIYOPATA KATIKA MALEZI YA WAZAZI WANGU WAPENDWA MUNGU AWAJALIE MAISHA MAREFU YENYE FURAHA NA AMANI.

MKE WANGU, MTOTO WANGU, NDUGU ZANGU NA RAFIKI ZANGU WOOTE   NAWAPENDA SANA NA NINASHUKURU KWA KILA KITU.WASALAAM CHEF ISSA


JINSI YA KUPIKA PRAWNS MASALA

MAHITAJI
1 kg Prawn
5 vitunguu vikubwa chop chop
3 nyanya kubwa za kuiva chop chop
3 kijiko kikubwa cha chakula Ginger-garlich paste
6-7 kijiko cha chakula mafuta ya kupikia
1 kijiko cha chakula Turmeric powder
1 kijiko cha chakula Coriander powder
1/2 kijiko cha chakula Garam Masala
2 kijiko cha chakula maji ya limao
10 gram chumvi
240 gram maji ya baridi
majani ya Coriander chopped kwajili ya kupambia

JINSI YA KUPIKA
1. Safisha prawns  toa magamba kisha iwekee ladha kwa kuchanganya cumvi 10 gram,1/2 kijiko cha chakula turmeric powder, 1 kijiko cha chakula ginger-garlic paste, na maji ya limao kwa dakika 30.
2. Kisha pasha moto sufuria weka mafuta ya kupikia, weka kitunguu maji na endelea kukaanga. Kisha weka  ginger-garlic paste endelea kuchanganya mpaka iwe rangi ya kahawia.
3. Kisha weka garam masalas, na nyanya endela kukaanga mpaka ziive na mafuta yaanze kuonekana kwa juu.
Kisha weka wale prwans waliokua umewaandaa na kisha koroga vizuri ichanganyike na funika na mfuniko kwa dakika 4 mapaka 5 kwa moto wa wastani ili isiungueKisha weka maji na koroga vizuri tena ichanganyike safi kabisa funika kwa dakika 4 na funua ukishaona mchuzi unakua mzito na mafuta yanakuja tena juu itakua imeshaivaHuu ni muonekano safi kabisa wa prawns masala yako ianvutia kwa rangi na inatamanisha sana kwa harufuHapa ni muonekano imeandaliwa kwa mlaji kwa kula na wali pamoja na mboga majani.

MAPISHI HAYA HAYA UNAWEZA TUMIA KWA KUWAPIKIA FAMILIA AU HOTELINI WAGENI WAKO. MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI, NYAMA YA KUKU, NYAMA YA MBUZI AU KONDOO NA PIA NYAMA YA NG'OMBE ILA KWA KUPIKA NYAMA HIZO NILIZOTAJA CHEMSHA KWANZA ZIIVE KISHA NDIO UWEKE KWENYE MCHANGANYIKO WA MASALA SAUCE YAKO. USITUMIE MAJI KUMBUKA KUTUMIA MCHUZI UTAKAO BAKIA KWENYE SUFURIA BAADA YA KUCHEMSHA NYAMA YAKO. NI RAHISI SANA NA INAPENDEZA.


Tuesday, July 27, 2010

JINSI YA KUANDAA KACHORI AU KATLESS

 KACHORI  HUTUMIKA KAMA KITAFUNWA KWAJILI YA PICNIC, CHAI YA ASUBUHI AU SAA 10 JIONI HUPENDWA SANA NA WATU WA LIKA ZOTE. KACHOLI HII NI MAALUMU KWA WALE WENYE MATATIZO WASIOTUMIA UNGA WA NGANO.

MAHITAJI

300 gram nyama ya kusaga
1 kilo ya viazi ulaya (5-6)
1 kijiko cha chakula Mafuta ya kupikia
½ kijiko kidogo cha chai Cumin seeds (Jeera) 
1 ½ kijiko kidogo cha chai Coriander powder (Dhaniya) 
2 pili pili mbuzi au ndefu za kijani 
1 ½ Tangawizi mbichi
¼ Kijiko cha chai Garam Masala
4 kijiko kikubwa cha chakula maji ya limao au ndimu
 ½ chumvi
10 gram kitunguu swaumu
5 mayai ya kuku
Mafuta kwajili ya kukaangia

 
JINSI YA KUTENGENEZA

Chemsha viazi kwenye pressure cooker au sufuria vikiwa na maganda yake.

Chemsha nyama ya kusaga na maji 50 gram, kitunguu swaumu 10 gram na vijiko 4 vya mai ya limao mpka iive kisha weka pembeni.

Kisha menya viazi ulivyochemsha kisha kata katika vipande vidogo. Pasha mafuta ya kupikia kijiko kimoja kwenye kikaango.

Kisha weka mbegu za cumin kwenye kikaango. Mbegu za cumin zikishapasuka, ongeza coriander powder, pili pili mbuzi, Tangawizi, Kisha weka chumvi na viazi. Kaanga kwa dakika 2-3 itakua imeiva vizuri.
Kisha ponda mchanganyiko wako mpaka uwe laini kabisa

Kisha chukua mchanganyiko huo laini wa viazi na tengeneza maumbo madogo ya mviringo ukubwa kama limao kisha bonyeza kwa kutumia kidole kati kati ya umbo hilo utapata nafasi ya kuweka kijiko kimoja cha chai nyama ya kusaga iliyoiva kisha funika kwa kutumia viazi na jitaidi kuviringisha tena kwa kutumia mikono yako miwili ili upate umbo zuri.Baada ya kumaliza kuandaa maumbo safi kabisa ya duara na yenye nyama ya kusaga kwa ndani, piga mayai pembeni kwenye bakuli na chovya umbo moja moja na weka kwenye kikaango chenye mafuta ya moto kaanga ukishapata rangi tu ya kahawia toa maana viazi na nyama vimeshaiva unachotafuta ni kau kau na rangi safi ya kahawia pande zote.

MPATIE MLAJI KACHORI HII IKIWA YAMOTO PIA UNAWEZA USIWEKE PILI PILI NA TANGAWIZI HASA KWA WALE WANOSUMBULIWA NA VIDONDA VYA TUMBO AU MATATZIZO YA GESI TUMBONI NA BADO KACHORI YAKO IKAWA SAFI SANA. UNAWEZA KULA NA TOMATO SAUCE, MAYONAISE, CHACHANDU AU ACHALI.


KITAFUNWA SAFI SANA KWA FAMILIA YAKO

MAJIBU YA MASWALI KUHUSU KATLESI AU KACHORI???
KACHORI NI STAILI YA UPISHI WA CHAKULA CHA WATU WANAOTUMIA MBOGA MAJANI TU NA ASILI YAKE NI INDIA NA KAWAIDA INATENGENEZWA NA UNGA WA NGANO KISHA UNAWEKA KATIKATI MCHANGANYIKO WA VIAZI KAMA HAPO JUU KWENYE RECIPE YATU KISHA UNATENGENEZA MAOMBO SAFI YA DUARA. UNACHOVYA KWENYE UNGA WA DENGU ULICHANGANYWA NA MAYAI NA UNAKAANGA KWENYE MAFUTA MAPAKA UPATE RANGI YA KAHAWIA.

KATLES KWA WATU WENGI NI MCHANGANYIKO HUU WA VIAZI KAMA HAPO JUU KWENYE RECIPE NA KISHA UNAWEKA KATI NYAMA YA NG'OMBE, SAMAKI AU KUKU NA HATA UNAWEZA WEKA MBOGA MAJANI NA BADO UTAITA KATLESI KWAKUA NAMANA YA UTENGENEZAJI NI HIYO HIYO KIKUBWA KATI KUWE NA AINA YEYOTE YA CHAKULA UNACHOPENDA WEWE.

KUTOKANA NA AINA HII YA UTENGENEZAJI WA VYAKULA VYOTE HIVI VIWILI KWA WALE WASIOTUMIA UNGA WA NGANO BADO WANAWEZA KUITA KACHORI INGAWA HAWAJATUMIA UNGA WA NGANO. NA KWA WALE WANAO KULA UNGA WA NGANO INGAWA WAMETUMIA VIAZI TU HII WATAITA KATLESI. HAIBADILISHI MAANA INGAWA UHALISIWA WAJINA NA UPUNGUFU WA RECIPE UNATEGEMEA WEWE MLAJI MAJINA YOTE NI SAHIHI.

NASHUKURU SANA KWA MASWALI YENU NAIMANI MTAKUA MMENIELEWA VIZURI.


Monday, July 26, 2010

JINSI YA KUTENGENEZA ICE CREAM BILA YA KUTUMIA MASHINE KWA MATUMIZI YA NYUMBANI


FUNGUA BLOG UPANDE WA MAFUNZO YALIOPITA YA MWEZI WA 1 UTAONA MAFUNZO YA JINSI YA KUTENGENEZA ICE CREAM BILA YA KUTUMIA MACHINE NI RAHISI NA NI NAFUU FURAHIA NA FAMILIA YAKO.Sunday, July 25, 2010

WAPISHI WA MAJUMBANI NA MAHOTELINI NAWAOMBA USHIRIKIANO WA MAWAZO YENU NA USHAURI NI MUHIMU SANA KWA MAENDELEO YA BLOG YETU YA MAFUNZO YA CHAKULA BORA NA SALAMA

WAPENZI WA BLOG YA CHAKULA BORA NA SALAMA NAWAOMBA RADHI KWA KUTOKUWEPO HEWANI KWA WIKI NZIMA.

SABABU YA KWANZA NI MATATIZO YA INTERNET PILI MEMORY CARD YA CAMERA YANGU ILIPATA VIRUS IMEKUFA NA NIMEPOTEZA PICHA ZOOTE SASA NAANZA UPYA NA TUPO PAMOJA.

NAWAOMBA WADAU WOTE MNAOFATILIA MAFUNZO HAYA MTOE MAWAZO NA USHAURI WENU ILI TUSONGE MBELE. NITAFURAHI SANA  SANA KUPATA PICHA ZA MAPISHI MLIOANDAA HATA MOJA TU NA NITAZIWEKA KWENYE BLOG ILI KUHAMASISHA WOTE WAPENDA CHAKULA KIZURI NA SALAMA.

KWA WALE WANAOPENDA KUJUA HISTORIA NA MAFANIKIO YANGU YA MAPISHI ILIPOANZIA NUNUA GAZETI LA BANG UTAPATA HABARI ZANGU NA PIA UTAPATA RECIPE ZA VYAKULA VINGI KWA KILA TOLEO

BINAFSI CHEF ISSA NAPENDA SANA SANA WATOTO, NAPENDA KUFUGA NA KUCHEZA NA MIFUGO AINA YOOTE, NAPENDA KUVUA SAMAKI.Hapa nilikua nawalisha bata na wamenizoea na ukifika muda huu huwa wansogea hapa wakijua kunarafiki atatuletea chakula.Hapa na weka sawa mti wangu wa kuvulia samaki nikiw andani ya boti dogo


Hapa nimepata samaki wa 4 nikapiga nae picha na kumrudisha katika maji aendelee kuishi cha kushangaza samaki wa chakula huwa sivui huwa na nunua to sokoni wote nao pata napiga picha na kuwarudisha katika maji waendelee kuishi naona uchungu kweli kukatisha maisha yao.

NAWATAKIA SIKU NA KAZI NJEMA WAPENZI WOTE WA BLOG HII.


HII NI BURGER YA KUKU KIFARANGA TAMU KULIKO ZOTE

WENGI MMEKULA SANA BURGER ZA KUKU LAKINI NAIMANI WENGI WENU HAMJAWAHI KULA BURGER HII YA KIFARANGA

NI TAMU SANA NA NILAINI HUSUMBUKI KUTAFUNA ILA UNAHITAJIKA KUA NA ROHO NGUMU MAANA UNACHINJA KWA MENO NA HAINA SAUCE.HAHAHAHAHAAAAAAAA JE UTAWEZA KULA? LADHA YAKE UNADHANI ITAKUWAJE?

JE UNAPENDA KULA BURGER YA NYAMA YA KIFUA CHA KUKU


BURGER HII SI MAARUFU SANA ILA NI NZURI SANA NA NI RAHISI KUTENGENEZA KAA TAYARI KWA KUWAKAMATA FAMILIA YAKO KWA RECIPE HII

MAHITAJI

200 gram kifua cha kuku
1 mkate wa mvirongo kwajili ya burger yako
50 gram vipande vya duara tango
50 gram vipande duara nyanya fresh iliyoiva vizuri
20 gram mayonaise
20 gram kitunguu maji slice
20 gram tomato ketchup au tomato sauce
20 gram BBQ sauce
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
30 gram matango machanga ya kopo ( Ghekins)Huu ndio muonekano wa kifua cha kuku chukua chumvi, pilipili manga na BBQ sauce kipake vizuri kisha weka kweney friji kwa nusu saa au saa moja ili mchanganyiko huo uingie vizuri kwenye nyama na iwe na ladha safi.Baada ya saa 1 chukua kifua hicho cha kuku weka kwenye jiko la kuchomea iwe ni la gesi au mkaa au jiko maalumu kwajili ya nyama choma. Pia kama huna unaweza tumia kikaango washa moto wa wastani kisha choma pole pole mpaka iive na iwe na rangi safi ya kahawia kama muonekano kwenye picha.

 

Nyama ikishaiva chukua mkate ukate kati kati na kisha paka mayonaise kwa juu, kisha paka tomato sauce kwa chini. kipande cha chini panga matango na nyanya pamoja na slice za kitunguu maji. Juu yake weka kifua cha kuku na funika na kipande cha pili kilichobakia.

WAPATIE FAMILA YAKO CHAKULA HIKI WAKATI WA MCHANA HASA SIKU ZA WEEKEND WAFURAHIE KWA KULA CHAKULA CHEPESI KWA KUSINDIKIZWA NA VIAZI VYA KUKAANGA NA SALAD.

JE UNAPENDA KULA BURGER YA NYAMA YA KUSAGA YA KUKU

HII NI BURGER MAARUFU SANA YA NYMA YA KUKU YA KUSAGA KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA

JE UNAPENDA KULA BURGER YA SAMAKI

KAA TAYARI KWA KULA BURGER YA SAMAKI YENYE PILI PILI HOHO NA AVOCADO SAUCE

MAHITAJI

1 kijiko kidogo cha chai mayonaise
1 sauce ya Parachichi
200 gram Nyama ya samaki
1 Jalapeno au Pili pili hoho
1 Mkate wa mviringo kwajili ya burger
1 Nyanya
1 lettuceHuu ni muonekano wa parachichi safi lililoiva

MAHITAJI KWAJILI YA SAUCE YA PARACHICHI

2 parachcichi ndogo
3 kijikocha chakula olive oil
4 kijikocha chakula juisi ya ndimu
¼ kijiko cha chai Tabasco (Silazima)
60 gram cream
60 gram mayonnaise
1 kijikocha chakula kitunguu maji chop chop
¼ kijiko cha chai chumvi
¼ kijiko cha chai pili pli manga
JINSI YA KUANDAA

1. Menya na katkata katika vipande vidogo parachichi. Weka katika chombo parachichi, olive oil and juisi ya ndimu katika blender au food processor.
2. Kisha ongezea mayonaise, fresh cream, Kitunguu maji, Tabasco, Chumvi na pili pili manga nakisha blend mpka iwe laini na imechanganyika vizuri weka katika friji ipoe vizuri.Huu ndio muonekano wa sauce ya parachichi kwajili ya kuweka kwenye burger yako ya samaki


Huu ni muonekano safi kabisa wa vipande vya samaki vilivyokata kwa uzito wa grama 200 kwajili ya burger. ipake chumvi, juisi ya ndimu au limao na pilipi manga.

Kisha ipakae unga wa ngao kiasi tu na iweke kwenye kikaango chenye mafuta na moto wa wastani ikaange kwa muda wa dakika 15- 20 itakua imeiva safi kabisa kwajili ya kuweka kweney burger yako.

pia unaweza kuiweka kwenye oven baada ya kuipaka unga ili kuepuka kutumia mafuta kisha tumia muda huo huo kwa moto wa wastani itaiva na kua tayari kwa kuiweka katika burger

 Huu ni muonekano wa jalapeno ukikosa tumia pili pili hoho hazipishani sana ladha zinapisha maumbo tu

Samaki akishaiva chukua mkate kata kati kati kisha paka mayonaise kwa chini na kisha weka majani ya lettuce, juu yake weka samaki ikiwa bado ya moto.

Juu ya samaki weka sauce ya parachichi ya kutosha maana ndio inabeba ladha ya burger yako pia weka kipande cha nyanya na slice za jalapeno kisha funika ka kipande cha pili cha mkate

Huu ni muonekano safi kabisa wa burger yako ya samaki ni salama kwa mlaji, furahia na familia yako.
 

Saturday, July 10, 2010

MAPISHI MBALI MBALI YA SAMAKI AINA YA TROUT

CHAKULA HIKI NI KIZURI SANA KWA AFYA YAKO WEWE MLAJI KAA TAYARI KWA RECIPE

MAHITAJI

1 fungu la majani ya cerely
2 vikubwa kitunguu maji
3 kubwa karoti
4 samaki anina ya trout
1 fungu majani aina ya dill
50 gram kitungu swaumu
2 limao kubwa kamua maji yake
1 chupa ndogo ya fish masala
250 gram mafuta ya kupikia
5 gram pili pili manga
10 gram chumvi


Haya  ni majani ya cerely yanapatikana popote sokoni au duka la mboga kwa urahisi sana na ninafuu husaidia kukata shombo ya samaki na huleta harufu safi sana


Huu ni muonekano wa mkato unaotakiwa kwajili ya caroti za kupikia samaki wako
Huyu ndie samaki hasa nayeitwa trout hupatikana toka maji baridi kwa nyumbani tanzania utampata Arusha ni mzuri na mtamu sana ingawa anamibamidogo midogo sana

JINSI YA KUANDAA

Chukua samaki wako hakikisha ni msafi umetoa magamba na matumbo yote na umemuosha vizuri kwa maji baridi.

Kisha weka karoti kitunguu na cerely kwenye chombocha kuokea na baada ya hapo muweke samaki juu ya hizo mboga mboga kwenye chombo utakachotumia kuokea changanya mafuta ya kupikia, maji ya limao, fish masala, kitunguu swaumu, pili pili manga pamoja na chumvi.

Kisha mwagia juu ya samaki na mwisho kabisa weka majani aina ya dill juu ya samaki funika kwa juu kwa kutumia aluminium foil oka kwenye oven kwa dakika 20 kisha toa hiyo foil acha wazi choma kwa dakika 10 hadi 15 kisha mtoe samaki atakua tayari kwa kuliwa .


Huu ni muonekano wa samaki wakiwa tayari ameshaiva toka kwenye oven na tayari kuliwa


Jinsi ya kupanga katika sahani chota ule mchuzi weka kwenye sahani iliyo kama bakuli kisha chota samaki muweke ndani ya sahani yako, kisha chota majai ya cererly na karoti zilizoiva pamoja na samaki weka juu ya samaki mwisho pamba na jani fresh aina ya dill. Furahia chakula hiki pamoja na famila yako.

AINA HII YA UPIKAJI UNAWEZA TUMIA KWA KUKU AU SAMAKI AINA YA KIBUA, CHANGU, JODARI, SARADINI, RED SNAPER, SATO AU SANGARA.


JINSI YA KUANDAA SALAD YA MBOGA MAJANI NA SAMAKI TUNA

SALAD YA MAYAI, MBOGA MAJANI NA SAMAKI TUNA

MAHITAJI

1/2 kilo nyama ya samaki tuna
3 nyanya zilizoiva
1 kitunguu kikubwa
1 lettyce kubwa
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
1 chupa ya mayonaise
1 tango kubwa
30 gram vinega ( siki nyeupe)
50 gram corn oil
4 mayai ya kuku


JINSI YAKUANDA FATA MAELEKEZO KWA CHINI KATIKA PICHA
Huu ni muonekano wa samaki tuna akiwa sokoni

Hii ni nyama ya tuna baada ya kuchunwa ngozi


Huu ni munekano wa yai lililochemshwa kisha tumia kifaa hicho hapo katika picha kukatia mayai yako yatakua katika umbo safi la mviringo


Huu ni muonekano wa majani aina ya chive ni jamii moja na majani ya kitunguu cho chop kwa umbo dogo kama inavyoonekana kwenye picha

Huu ni muonekano wa tangu kubwa zuri la kijani


Huu ni muonekano wa kitunguu kikubwa kata skama inavyoonekana kwenye picha maumbo ya duara

Huu ni muonekano wa nyanya nzuri ngumu iliyoiva tayari kwa salad kata umbo kama linaloonekana kwenye picha


Huu ni muonekano wa mayonaise safi ukweli american garden mayonaise ni nzuri na inapatika dunia nzima


Huu ni muonekano wa majani ya lettuce ni kubwa na inaafya safi kabisa kwa kupendezesha salad yako

JINSI YA KUANDAA

Kwanza chemsha mayai kwa dakika 7 , kisha chemsha nyama ya samaki tuna weka vinega, chumvi na pili pili manga ili kuweka ladha safi.

Kisha kata kata mboga zako zote kama inavyoonesha kwenye picha

kisha chukua nyama ya tuna iliyopoa changanya mayonaise na majani ya chives pamoja na mafuta ya mahindi ( corn oil) maana hata ukihifadhi salad yako katika friji huwa hayana tabia ya kuganda.

kisha weka jana la lettuce kwenye sahani juu yake weka nyama ya tuna, juu ya nyama weka vitunguu na pembeni weka mayai pamoja na nyanya na matango.MPATIE MLAJI SALAD HII KABLA YA MLO KAMILI AU UNAWEZA KULA MCHANA KAMA MLO KAMILI PAMOJA NA KIPANDE CHA MKATE AU VIAZI VYA KUCHEMSHA AU VIAZI VYA KUKAANGA NA UKAFURAHIA SANA KWA KUSHIBA CHAKULA KITAMU NA CHENYE FAIDA NA MWILI WAKO.


JINSI YA KUANDAA FISH AND CHIPS

CHAKULA HIKI ASILI YAKE NI UINGEREZA KAA TAYARI KWA RECIPE


JIFUNZE KUANDAA PRAWNS COCTAIL NI NZURI NA TAMU SANA

RECIPE YA SAMAKI KAMBA (PRAWNS) KWA MITINDO TOFAUTI

MAHITAJI

1 Chupa ya Mayonaise
1 chupa ya Tomato sauce
20 gram Chumvi
10 gram Pili Pili manga
1 kijiko kidogo cha chai Tabasco
100 ram Maji ya limao
1 kubwa lettuce
1 kubwa Limao
2 kubwa Nyanya fresh
1 kilo Samaki kambaHuu ni muonekano wa samaki kamba wabichi
Huu ni muonekano wa lettuce

Huu ni muonekano wa prawns waliochemshwa baada ya kumenywa magamba na kusafishwa vizuri


Huu ni muonekano wa coctail sauce


JINSI YA KUANDAA

Chukua prawns wamenye magamba ya juu kisha wasafishe safi na maji baridi, kisha wachemshe katika maji moto kwa dakika 5 - 8 tu watakua wameishaiva watoe waweke kwenye maji baridi wapoe tayari kwa kuandaa salad yako safi kabisa.

Kisha chukua mayonaise, tomato sauce au tomato ketchup, chumvi, pili pili manga, maji ya limao pia kama una white wine unaweza kuweka kisai kisha chukua uma au mchapo tumia kuchanganyia mchanganyiko wako mpaka uchanganyike safi na kupata ladha safi kama muonekano katika picha hapo juu.

Kisha chukua prawns wako waliopoa safi changanya na hiyo coctail sauce vizuri kisha fata maelekezo katika picha hapo chini jinsi ya kupamba kwa matumizi tofauti tayari kwa kumuudumia mlaji.Unaweza kutumia glasi nzuri kama hiyo hapo juu chini weka majani ya lettuce kisha juu yake weka mchanganyiko wa hao prawns na Pembeni pamba na kipande cha nyanya pamoja na limao. Kisha mpatie mlaji.


Huu ni muonekano wa juu ya glasi jinsi ilivyopendeza tayari kwa kumuudumia mlaji.


Huu ni mtindo wa pili jinsi ya kupamba kwenye sahani kama kawaida chini weka majani ya lettuce kisha juu weka mchanganyiko wa prawns na coctail sauce pembeni chora mduara kwa kutumia balsamic vinegar na rushia vipande vya nyanya juu kabisa weka maotea ya mbegu ( sprout) kisha muhudumie mlaji.


Hii ya mwisho ni muonekano wa kisherehe zaidi au familia kubwa unaweka kwenye sahani kubwa kisha unaweka mezani ili kilammoja ajipakulie na kuenjoy kiasi anachotaka. mfululizo ni ule ule weka chini majani ya lettuce kisha juu nakshi prawns wako safi waliochanganywa na coctail sauce.
FANYA UBUNIFU WOWOTE ULE ILIMRADI CHAKULA CHAKO KIPENDEZE NA KIVUTIE KWA WALAJI NA UJIVUNIE KIPAJI CHAKO.