CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Sunday, September 30, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA VIAZI VYAKUKAANGA NA BINZARI NYEMBAMBA

 
NIRAHISI SANA UTENGENEZAJI WAKE PAMOJA NA GHARAMA NAFUU NA MUDA WA MAANDALIZI NI MCHACHE
 
MAHITAJI
 
500 grams viazi ulaya
1 kijiko kimoja kidogo cha chai binzali nyembamba
1/4 kijiko kidogo cha chai manjano
1/2 kijiko kidogo cha chai pili pili ya unga (Chilli Powder)
5 gram maji ya limao au Lemon Juice
5 gram chumvi
5 gram majani ya korienda
 
JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi Dakika 15
Muda wa mapishi Dakika 15
Idadi ya walaji :  Watu 2
 
 
 Mimi nimetumia viazi ulaya vyekundu wewe unaweza tumia viazi ulaya vyovyote vile pia na binzali nyembamba.

 
 Kata kata viazi katika vipande vidogo vidogo

 
Washa moto na kisha weka kikaango katika moto na kijiko kimoja kikubwa cha samli au blue band. kisha weka binzali nyembamba na manjano unga wa pili pili na uendelee kukaanga
 
 
 
Kabla viungo havijaungua weka viazi na chumvi kisha endelea kukaanga.

 
Hakikisha unakoroga vizuri vichanganyike kabisa

 
KIsha mwagia maji na ufunike na mfuniko. Maji yanasaidia kuivisha viazi vizuri. Koroga kidogo ili viazi visishike chini.
 
 
 
Inachukua kama dakika10 hadi 12 bonyeza viazi na kidole au mwiko ukiona vimekua laini, basi jua vimeiva. Kisha mwagia majani ya gili gilani na maji ya limao kuongeza ladha safi.
 

 
Mpatie mlaji chakula hiki kikiwa chamoto unaweza kula na wali, pialu au chapati na mchuzi wa nyama.


 
CHAKULA HIKI KINAMUONEKANO SAFI SANA
 


Wednesday, September 26, 2012

 
JIFUNZE KUANDAA KEKI HII SAFI KABISA YA BILA MAYAI KWA MTINDO NA LADHA TOFAUTI NI RAHISI NA NAFUU KWA GHARAMA
 
 
MAHITAJI
 
300 gram unga wa ngano
240 gram sukari ya unga
1 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
3 kijiko kikubwa cha chakula cocoa powder
1/3 cup vegetable oil ( corn oil au olive oil)
1 kijiko kikubwa cha chakula siki au vinegar
1 kijiko kidogo cha chakula vanilla essence
240 gram majibaridi safi na salama
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI
 
Muda wa mapishi : dakika 15
Cook Time: Dakika 30
Ujazo : Keki moja yenye vipande 7"
 
 
Chukua unga wa ngano, sukari ya unga, chumvi na baking powder chekecha katika chujio vizuri kisha hifadhi katika bakuli

 
Kisha changany vizuri uchanganyike

 
Katika bakuli tofauti safi chukua maji, vegetable oil, vinegar na vanilla essence tumia mchapo na changanya vizuri
 
 
 
Chukua mchanganyiko wako wa maji na mafuta kisha mimina pole pole kwenye mchanganyiko wenye unga na hakikisha huweki mabonde.

 
Pole pole mpaka unapata mchanganyiko safi na mzito

 
Kisha paka mafuta na mwagia unga chombo chako la kubekia lenye upana na inchi  7.

 
Mimina katika chombo chako cha kubekia

 
Choma katika oven iliyokwisha washwa kwa moto wa 360F kwa muda wa dakika 30 au mpaka utakapo choma tooth pickkati kati ya keki na itoke safi. Pia baada ya kupika kwa dakika 30 utaona kabisa keki yako inaanza kuachia chombo cha kubekia.

 
KIsha toa keki yako katika ovena na iache nje ipoe kwa dakika 1. Kisha geuza chini juu chombo cha kubekia juu ya waya au wavu iache hapo ipoe.

 
Usiogope kuona keki yako imeungua au kua na rangi mbaya kwa chini hii inatokana unga uliomwagia wakati unataka kumimina mchanganyiko wa keki yako
 
 
 
 
Pia keki hii unaweza weka katika friji kwa matumizi ya baadae
 

 
Mimi na familia yangu huwa tunapenda kukata vipande na tunamwagia sukari yaunga juu

 
 
 
Kipande cha keki kinavyoonekana na ni sponge bombastick kabisa kwa matumizi halali ya chai jioni au asubuhi au wakatai wowote majumbani na mahotelini
 
 
 


Saturday, September 15, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI YA TIKITI MAJI NA LIMAO

 
JUISI YA TIKITI MAJI NA LIMAO NOI SAFI SANA SANA
 
 
MAHITAJI
 
5 kg ya Watermelon
180gram juice ya limao 
80 gram ya asali mbichi
1 fungu majani ya Mint
vipande vya barafu au Ice Cubes,
 
JINSI YA KUTENGENEZA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : dakika 15
Muda wa mapishi : dakika 15
Idadi ya wanywaji : Watu 4
 
 
Kiwango cha limao kinaweza kua gram 120 hadi gram 240 hii hutegemea na kiwango cha sukari katika tikiti maji au
 
 
Kata kata watermelon katika vipande vidogo, menya ngozi na kumbuka kutoa mbegu.

 
Chukua vipande vya watermelon saga pamoja na juice ya limao

 
Kisha ichuje katika chujio safi baada ya kuisaga

 
Kisha weka ice cube pamoja na majani ya mint katika jagi.

 
Kisha mimina juice katika jagi lako lenye barafu na mint

 
Kisha mimina asali mbichi kwenye mchanganyiko wa juisi na ukoroge ichanganyike.

 
Kihsa mpatie mnywaji ikiwa ya baridi weka ice cubes na majani ya mint kwa kupambia.

 
Huu ni muonekano safi kabisa baada ya kupamba kwa jani la mint na kuongeza ice cubes ili mnywaji afurahie kinywaji baridi

 
 
KINYWAJI HIKI NI SAFI SANA NA KINONGEZA HAMU YA KULA WAAANDALIE FAMILIA WABURUDIKE
 
 
 


Thursday, September 6, 2012

ACTIVE CHEF RESTAURANT NYUMBANI TANZANIA

NIMEFUNGUA PAGE YA FACE BOOK ... inaitwa ...... Active Chef

WEWE NI MPENZI WA BLOG HII YA CHAKULA SAFI NA SALAMA NAKUOMBA CLICK HIYO LINK HAPO CHINI KISHA ITAFUNGUKA NA UNAWEZA KUJIUNGA KWA KU CLICK LIKE KATIKA UKURASA HUO ILI UWEZE KUENDELEA KUPATA RECIPE NA MATUKIO MUHIMU YAHUSUYO CHAKULA
 
 
http://www.facebook.com/pages/Active-chef/509561519067534#!/pages/Active-chef/509561519067534

BAADA YA KU LIKE UTAWEZA ONA PICHA MUHIMU NA RECIPE ZA RESTAURANT MPYA YA ACTIVE CHEF ILIYOFUNGULIWA NYUMBANI TANZANIA

 
Hapa iliku bado restaurant inatengenezwa

 
Mpangilio wa sauce na salad na nyama za tayari kwa kuchoma

 
Tunachoma samaki maarufu sana aina ya changu mwekundu na mweupe huwezi amini dakika saba tu chakula kipo mezani na ameivaa saafi


Huu ni muonekano wakati wa usiku

 
VIDEO HII NIMETUMIWA NA JAMAA MMOJA ALIETEMBELEA RESTAURANT NA KUFURAHIA SANA BBQ
 
JE WADAU MNADHANI RESTAURANT HII IPO MJI NA MAENEO GANI? MSHINDI WA KWANZA BBQ BUREEEEE!!!!
 
 
WASALAAM CHEF ISSA
 
 

Sunday, September 2, 2012

JIFUNZE KUTENGEEZA SANDWICH YA CHEESE NA MCHICHA

 
 
KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA SANDWICH YA MCHICHA PAMOJA NA CHEESE NI RAHISI SANA NA NAFUU PIA
 
 
MAHITAJI
 
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI