CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Friday, May 28, 2010

MAANDAZI YA HILIKI NA TUI LA NAZI

MAANDAZI HAYA YANALADHA SAFI SANA KWA MLAJI NI RUKSA KUONGEZA KIUNGO AU KUPUNGUZA NA ANDAZI LAKO LITABAKI NA UBORA ULE ULE MAANA SIO WATU WOTE WANAPENDA VIUNGO.
MAHITAJI

1 kikombe cha chai kikubwa
2 Amira ya chenga kijiko kidogo cha chai
1 kilo unga wa ngano
1 hiriki kijiko kikubwa cha chakula
1 kikombe cha chai tui zito la nazi na vijiko viwili vya mafuta ya kupikia ya baridi (1 kikombe cha chai mafuta ya moto kamahutumii tui la nazi )
1 chumvi kijiko kidogo cha chai
1 maji ya moto wa wastani kikombe kikubwa cha chai


Hii ni hiriki , sukari na Amira ya chenga

Weka sukari, Amira, chumvi na hiriki katika bakuli kisha weka mafuta yakupikia vijiko viwili

kisha weka tui la nazi

Kisha changanya unga wa ngano kilo moja katika bakuli

kisha weka maji ya moto katika unga

Anza kukanda unga

Kisha sukuma unga mpaka upate unene wa saizi ya andazi unalotaka 

Kisha kata andazi kwa saizi ya andazi la ukubwa unaotaka

Haya ndio maandazi mabichi baada ya kukatwa tayari kwa kuchomwa acha yaumuke kwa dakika 10 ili utakapochoma yasijae mafuta ndani

Weka mafuta ya kupikia katika kikaango kisha yapate moto wa wastani yasiwe yamoto sana maandazi yakaungua pia hayataiva ndani


HUU NDIO MUONEKANO SAFI WA MAANDAZI YA HIRIKI NA TUI LA NAZI ENJOY NA FAMILIA YAKO KWA CHAI YA JIONI AU CHAI YA ASUBUHI KWA KITAFUNWA SAFI NA SALAMA MAANA HAKINA MAFUTA MENGI PIA CHUMVI INAAIDIA KUKIMBIZA MAFUTA KATIKA UNGA.Thursday, May 27, 2010

CHAPATI NA NYAMA YA MBUZI

CHAPATI HIZI NI SAFI KABISA KWA FAMILIA KUBWA KUTOPIKA MARA KWA MARA UNAPIKA NYINGI NA UNAZITUNZA WIKI MOJA NA ZIKABAKI NA UBORA ULEULE, PIA NYAMA HII YA MBUZI INAKUA HAINA HARUFU MTU YEYOTE ANAWEZA KULA KWA AINA HII YA MAPISHI NA AKAFURAHIA SANA 

MAHITAJI

1 kg unga wa ngano
1 kikombe kimoja
1 kijiko kidogo cha chai chumvi
nusu kikombeha chai mafuta ya kupikia
2 mayai kuongeza ladha

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEKEZO CHINI

unga wa ngano

Weka mafuta katika unga

kisha weka moto sana katika unga

kisha changanya kwa kutumia mwiko maana maji ni yamoto sana

weka chumvi

kishaanza kukanda kwa mkono maji yatakua yameshapoa

kanda unga safi kabisa uchanganyike

kisha anza kusukuma unga wote

baad ya hapo mwagia kwa juu mafuta ya kula pakaza eneo lote

hakikisha mafuta yameenea unga wote

kisha kunja pole pole unga wote kutengeneza mduara

kisha kata maumbo madogo ya usawa kwa kutumia kisu

baada ya hapo chuku yale maumbo uliyokata geuza na uyakandamize safi mpka chini

hapa ni baada ya kuzikandamiza


kisha chukua mti wa kusukumia na zisukume mapak upate upana wa kawaida tayari kwa kuzichoma


weka katika kikaango kikavu kisha zungusha chapati hiyo kw kutumia mkono


iache kidogo ichomwe


kisha igeuze baada ya kuiva upande mmoja

ikandamize tena kwa upande wa pili bado ikiwa kavu bila mafuta kama ni yamoto sana basi tumia karatasi kukandamizia


weka mafuta ya kupikia kwa juu hakikisha unasambaza chapati yote ienee


kisha geuza a upande wa pili paka pia mafuta


Toa weka katika sahani itakua imeiva safi kabisa tayari wa kuliwa

weka pembeni zipoe kisha unaziwekakatika sahani unatumbukiza katik mfuko wa plastiki usiweke kwenye friji weka tu nje zitakua safi na laini zinakaa wiki 1 baada ya hapo zitapoteza ubora ukitaka kula unatoa unapasha kwenye kikaango au kwenye micro wave inakua yamoto na laini zaidi na iliyochambuka kwa ubora uleule
MAHITAJI NYAMA YA MBUZI

1 kilo nyama ya mbuzi
1 kitunguu kikubwa
1 nyanya ya kopo
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu
3 viazi ulaya
1 kikombe kilichojaa mchanganyiko w mboga majani
1 kikombe cha maji baridi
1/2 kikombe mafuta ya kupikia

weka mafuta katika sufuri yakishapata moto weka kitunguu maji kaanga


hii ni nyama ya mbuzi ya mifupa inaladha yake ya kipekee sana

kaanaga vitunguu mpaka viwe vya kahawia ili kuleta ladha nzuri katika mchuzi wako na kuondoa harufu ya mbuzi ili mtu yeyote yule aweze kula

baada ya kitunguu kuwa kahawia weka nyama ya mbuzi piaendkea kukaanga

ongeza maji kiasi ili sufuria isiungue pamoja na nyama

kisha weka chumvi

acha mbuzi ichemke na itakua na mchuzi wa kahawia

kisha weka kitunguu swaumu hicho ni kifaa maalumu cha kusagia kitunguu swumu

baada yahapo weka viazi uklaya vilivyomenywa safi na kukatwa katwa vidogo

kisha weka nyanya ya kopo

kisha weka mchanganyiko wa mboga majani ( caroti, njegere na pili pili hoho, mahindi machanga ya njano)

kuongeza ladha zaidi unaweza weka unga wa binzali au rojo la binzali


MAFUNZO SAFI KABISA YA CHAPATI NA NYAMA YA MBUZI WAPIKIE FAMILIA YAKO CHAKULA BORA NA SALAMA WAFURAHIE

RATIBA YA CHAKULA CHA MTOTO

KWA WALE WOTE WALIONIANDIKIA EMAIL KUOMBA RATIBA YA CHAKULA CHA MTOTO SASA RECIPE AU JINSI YA KUANDAA CHAKULA IPO KATIKA MS WORD NIANDIKIE EMAIL KAMA UNAHITAJI NIKUTUMIE ITAKUSAIDIA KUPRINT NA KUWEKA NYUMBANI AU KUMPATIA DADA YUMBANI AWEZE KUMUANDALIA MWANAO CHAKULA BORA NA SALAMA.

WADAU WENGI WAMENIULIZA KWANINI RATIBA INAISHIA SIKU 5 TU? JAMANI SIJASAHAU KUWEKA SIKU YA JMOSI NA JPII  ILA NILISAHAU KUTIOA MAELEZO NI TARATIBU ZA CHAKULA KWA RATIBA MAANA UNAUZOESHA MWILI KUPOKEA AINA ´HIYO YA CHAKULA KWA MZUNGUKO WA SIKU TANO KWAHIYO WEWE MZAZI UNATAKIWA UCHAGUE KATIKA RATIBA HIYO CHAKULA CHA KATI KATI YA WIKI AMABCHO MWANAO ANAKIPENDA SANA KISHA UKIRUDIE KWA SIKU YA JMOSI NA JPILI.

HII PIA HUSAIDIA KUPUNGUZA GHARAMA YA MANUNUZI YA AINA YINGI ZA VYAKULA MAANA IKIWA SIKU 7 UNATAKIWA KUA NA MANUNUZI MAKUBWA ZAIDI LAKINI KWAKUA UNRUDI BASI UNATUMIA MABAK YA CHAKULA AMABCHO ULIBAKIZA SIKU ZA KATI YA WIKI.

Sunday, May 23, 2010

KUKU WA UFUTA NA KARANGA

KUKU HUYU NI RAHISI SANA KUPIKA, UNAWEZA HIFADHI KATIKA FRIJI KWA MUDA WA MWEZI NA CHAKULA BADO KIKAWA NA LADHA SAFI KABISAWAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE

MAHITAJI

1 kitunguu kikubwa
1/2 kuku au 1 kuku mzima
4 nyanya zilizoiva vizuri katakata au saga katika blenda
2 vijiko vikubwa vya chakula nyanya ya kopo
3 ufuta mkavu kijiko kikubwa cha chakula
4 kijiko kikubwa cha chakula karanga ya kusaga iwe mbichi au ilyokaangwa sawa tu
2 kijiko cha chakula mafuta ya kupikia maana karanga inamafuta mengi
1 chumvi kijiko kidogo cha chai
2 fungu la majani ya girigilani ( corrender leaves)
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu

weka mafuta ya kupikia na kitunguu katika sufuri kaanga kidogo kisha weka kitunguu swaumu

Kisha weka nyanya ya kopo endelea kukaanga

kisha weka kaanga iliyosagwa endelea kukoroga vizuri

baada ya kukorogasafi na mchanganyiko wako kua mzito na safi kabisa huu ndio muonekano wake kisha weka chumvi

kisha weka majani ya girigilani au corriender leaves na ukoroge vizuri

kisha weka nyanya uliyokua umesaga

koroga na acha ichemke vizuri ili nyanya iive vizuri

Hapa sasa nyanya imeiva safi na imechemka ya kutosha imeshabadilika rangi na mchuzi wote umekua na ladha ya karanga

Kisha weka vipande vya nyama ya kuku inapendez kama utakua umeichemsha ika iva pia usimwage ule mchuzi au maji uliyochemshia huyo kuku utayatumia hapa badala ya kuongexza maji unatumia mabaki ya mchuzi ulio chemshia huyio kuku ili kulinda ladha ya chakula hik


MWISHO KABISA PAKUA KUKU NA WEKA KATIKA CHOMBO CHA MLAJI KIHA MWAGIA JUU ULE UFUTA MALAJI ATAKAPOKUA ANAKULA UTAUTAFUNA UFUTA LIVE NA KUONGEZA LADHA SAFI KATIKA CHAKULA CHAKE KAMA UNAPIKA KWA FAMILIA AKUBWA BASI BAADA YA KUKU WAKO KUIVAMWAGIA UFUTA NDANI YA MCHUZI NA KOROGA VIZURI ILI UCHANGANYIKE KISHA WEKA MEZANI FAMILIA IFURAHIE