CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, January 6, 2015

JIFUNZE KUTENGENEZA CHACHANDU YA NAZI KUPIKA PAMOJA NA VIUNGO

KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA MUDA SI MREFU LEO LEO PAMOJA NA VYAKULA VINGINE HAPO CHINI
 

 

 

 

 

 

 
 
 

 
 


JIFUNZE KUTENGENEZA MCHANGANYIKO WA JUISI YA TIKITI MAJI NA MAJI YA MADAFU AU NAZI CHANGA

KIPINDI HIKI CHA MAJIRA YA JOTO HASA NYUMBANI TANZANIA NI MUHIMU SANA KUNYWA MAJI MARA KWA MARA ILI KUHAKIKISHA UISHIWI MAJI MWILINI. KINYWAJI HIKI KINAWEZA KUA MMBADALA MAHSUSI WA MAJI NA KUFANYA UFURAHIE SIKU YAKO NA NIRAHISI SANA KUANDAA
 
MAHITAJI
450 grams tikitiki maji kata vipande vidogo weka kwenye friji ipowe
1 dafu au Nazi changa kubwa
1 limao kubwa
Ice cubes, au vipande vya barafu
Majani ya Mint sio lazima
 
FATILIA JINI YA KUANDAA NA MAELEZO HAPO CHINI

 
Chukua kipande cha tikiti maji kasha katakata vipande vidogo weka kwenye friji vipowe
 
Kisha chukua  blender weka vitu vyote kwa mara moja maji na Nazi au dafu pamoja na vipande vya tikiti maji, limao na vipande vya barafu. Kawaida dafu na tikiti maji vyote vinasukari kwahiyo unaweka limao ili kuweka uwiano sawa wa sukari katika kinywaji chako kwa kuwongeza chachu. Kama wewe ni mpenzi sana wa madafu zidisha kipimo tofauti na maelekezo hapo juu.

 
Blend pamoja kama inavyoonekana kwenye picha ukpenda kuna na ladha zaidi weka na majani ya mint inaweka harufu safi sana.

 
Perfect drink for your summer haichukui muda nmrefu tayari una juisi safi sana kwajili ya biashara au family.


Baada ya kumimina kwenye glass unaweza ongozea vipande vya barafu kufanya kinywaji chako kiendelee kua cha baridi na kupoza kiu na koo baada ya kupigwa na jua mwanana la majira ya joto