CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Monday, January 25, 2010

NAMNA YA KUTENGENEZA CHAPATIUnga kilo moja weka sukari kijiko kimoja cha chai pamoja na chumvi kijiko kimoja cha chai
weka mafuta ya kupikia yamoto kikombe kimoja cha chai kidogo kisha changanya
Kisha weka maji ya uvugu vugu kikombe kimoja cha chai kidogo na endelea kuchanganyaKanda mpaka upate mchanganyiko mzuri laini na mkavuKata saizi ya unga ambao ukisukuma itatosha kwenye kikaango chakohuu ni muonekano wa chapati ndogo itakayoweza kuenea katika kikaango kidogo hata kwa matumizi ya nyumbani iweke kwenye kikaango cha moto  bila mafuta pika pande zote mbilikisha weka mafuta naigeuze geuze

hii ni chapati yako imekamilika na ni laini na ina lea kama daftari na ni tamu kupita maelezo


NAMNA YA KUTENGENEZA MAANDAZIChukua Amira ya chenga gram 11
Chumvi nusu kijiko kidogo cha chaiSukari gram 250Unga wa ngano kilo moja


Maji ya uvugu vugu nusu lita
Mafuta ya kupikia lita 2 na nusu


Weka pakiti ndogo ya amira yenye ujazo wa gramu 11 yoote kwenye unga wako wa kilo moja

Kisha weka chumvi nusu kijiko kidogo cha chai chumvi hii husaidia kupunguza mafuta ndai yaa andazi baada ya kuiva andazi lako litakua halina mafuta safi na salama kwa mlaji


Weka sukari gram 250 katika unga wakoBaada ya hapo weka mafuta ya moto ujazo wa kikombe kidogo cha chai au gr 250
 changanya vizuri mafuta bado yakiwa yamoto
Kisha weka maji ya uvuguvugu ili kuuwa ngano nakufanya amira kuweza kumuka haraka

Kanda mchanganyiko wako safi kwa kutumia nguvu na umakini mpaka mchanganyiko wako uwe lainiMchangyanyiko wako kama uko bado ni teketeke na ulizidisha maji kidogo weka unga kiasi kisha endelea kukanda mpakja uwe mkavu na laini


Hapa safi sasa Shepu vizuri tayari kwa maandalizi ya kusukuma na kukata


Sukuma unga wako mpaka saizi ya unmene halisi wa andazi lako utakavyopenda liwe


Kisha tumia kitu chechote kile kukatia kwa umbo lolote lile utakalo lipenda

Yaache kwa muda wa dakika 10 baada ya kuyakata yaumuke kisha itakua tayari kwa kuyachomaBaada ya kukata maumbo mazuri ya duara unga unaobakia unaweza viringisha maumbo tofauti kama uonavyo katika picha pia unaweza tengeneza hata herufi


 Pasaha mafuta yako katika moto wa wastani yasiwe na moto mkali utapelekea maandazi yako kuungua kisha yaweke katika moto na geuza kila mara ili yasivimbe upande mmoja na ikawa vigumu kuyageuza


Hili ni anfazi lako safi limeshaiva na halina mafuta ndani na safi kabisa


Tuesday, January 19, 2010

NAMNA YA KUCHONGA NDEGE KWA KUTUMIA TUNDA AINA YA APPLE

Hapo chini ni seti ya aina ya vifaa vinavyotumika kuchongea mboga na matunda katika mitindo tofauti


Hapo chini ni vifaa pekee tulivyotumia katika kuchongea tunda letu hili aina ya apple fatilia picha vizuri utaona jinsi ya kuchonga mpaka mwisho anatokea ndege mzuri aina ya bata mzinga kama utakua na swali lolote uliza.


Ndugu wapenzi wa blog yetu ya mafunzo ya chakula kama nilivyoahidi kuhusu kufundisha mapishi na sanaa ya marembo ya mboga na matunda sasa tunaendelea na mafunzo naimani wengi mtafurahia utaalamu huu pia maoni yenu ndio yananipa mwanga nijue hasa kama mnaelewa na mnafatilia. Mafunzo yanayofuata ni utengenezaji wa maandazi safi na salam pamoja na chapati wapenzi wa vyakula hivyo kaeni tayari kupata utaalamu